nakumbuka kiwanja chetu cha mtaa kilichukuliwa na wakubwa kwa mda baada ya uwanja wao mkubwa kuchukuliwa kufanyiwa mikutano ya kidini pande za kawe home,, sasa wakawa wanatunyanyasa kila ikifika saa kumi tu, wanakuja kutufukuza wacheze wao.. tukaunda tume ya kuwaondoa hawa ma bro,, tukakubaliana twende beach tukachukue mbigili za kutosha tukazimwage uwanja mzima mpaka magolini.. tukaenda tukajaza mifuko na mifuko, tukazimwaga usiku zote,,, kimbembe kesho yake, wakubwa wanakuja kucheza hawajatukuta wakaona mtelezo,, sie tumekaa tunawaangali tu,, maana wengine walikua na viatu wengine hawana,, wengine walioanguka wanakutana nazo,, mpira haukuchezeka siku hiyo, wakaanz kutusaka tukazoe miba tuliyoimwaga uwanja mzima. hakuna aliyekubali kama kamwaga mbigili.. na wao ndo ikawa mwisho wao kucheza pale wakahamia uwanja mwengine,, vijana tukarudi tukaanza kuzitoa mojamoja japo hatukuzimaliza,, ila shuhuli nasi ilitupata ya kuchomwa nazo maana hatukuzimaliza,, zilikuja kuisha kwa kutuchoma, unaiokota unaenda kuitupa..