Watoto wa kishua hamuwezi kuielewa hii picha

Watoto wa kishua hamuwezi kuielewa hii picha

Hahah unakuta eti Sabrina anaenda shule na school bus na kurudi nalo then anakua ndani ya geti,,muache Sabrina akacheze madange huko ,akacheze kibaba na kimama ,[emoji12] [emoji12]
Mi nimechezaa hivyo vyotee kibaba na mama nilikuwa naolewa kweli [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Katika vitu ambavyo ninajivunia kwa sasa ni kupitia kwenye maisha hayo,,,,hawa watoto wa sahiz hata wakikua sijui watasimuliana nini yani

Youtube, Facebook, instagram, tamthilia za kiphilipino na bongo movie. Tatizo kubwa litakalo wakabili ni magonjwa ya uzito wa ziada na presha katika umri mdogo, hawana shughuli za kuwachangamsha.
 
Hapo pensi umeifungia kamba ya kiatu, mfukoni una goroli mbili, hapo mpira unauliga kwa Ndore/Dole gumba hadi kucha linangoka upaka mchanga habar kwisha.

Fainali ni kutoa njunja/Funza vidolenj
Wewe utakuwa msukuma "unauliga"
 
[emoji23][emoji23][emoji23] yani ilikua ni noma sana aisee....kucha zilikua zinapona within three days tu tena kwa mchanga......kwenye magoli mmejaza viatu na mabegi kibao
Tena ilikuwa kidonda chochote unaweka mchanga na kinapona chenyewe.
Daaah fanya sahv uone balaa lake kweli dunia inabadlika.
 
hahahahaaa we ulikua wakishua mwanangu na hapo lazma mpira unaozungumzia ni gozi,,,,, mana hii ya makaratasi ilikua haiitaji idadi ya wachezaji ndani....hata mkiwa 30 mnakipiga tu[emoji16]
Duuuh umenkumbusha mbali xn aisee, mwaweza kua watu 6,14 hata 40 mtakacho kifanya ni kupanga folen then anatoka mmoja mmoja kupata timu 2...ko timu haikua na idadi rasmi ya wachezaji

Basi wakat huo Ronald ndo anahit nami nkapachikwa ilo jina

Nlikua nasakata mpira Pekupeku nikiwa pekupeku
 
Me kuna siku nilifunga magoli 75!
Halafu kuna ile kitu inaitwa tobo, ukipigwa tobo aisee ilikuwa unakimbizwa, ukikamatwa unakula kisago...ponea yako ilikuwa unapaswa ukimbie hadi ushike kisiki au mti uliopangwa!
Mimi nilijifanya bingwa wa kukimbia badala ya kushika mti nikawa nashndana mbio wala sishiki mti nilipigwa mtama nikadondoka chini wacha raia wanishambulie nilijuta sanaa siku hiyo.
 
Youtube, Facebook, instagram, tamthilia za kiphilipino na bongo movie. Tatizo kubwa litakalo wakabili ni magonjwa ya uzito wa ziada na presha katika umri mdogo, hawana shughuli za kuwachangamsha.
Lakini mkuu mimi kuna jambo najiuliza,kama sisi tulipitia maisha Yale kwanin leo hii tuwakataze watoto wetu wakirudi shule wasitoke nje ya geti ,,yani tunataka mtoto weekend ashinde kufanya homework na kuangalia tu katuni,kwamba tumebadilika sisi wazazi,au tuna upendo sana na watoto au nn yani
 
Na ule mchezo wa kijiti kikianguka tu inabd utoke mbio uende ukashike mti.
 
Lakini mkuu mimi kuna jambo najiuliza,kama sisi tulipitia maisha Yale kwanin leo hii tuwakataze watoto wetu wakirudi shule wasitoke nje ya geti ,,yani tunataka mtoto weekend ashinde kufanya homework na kuangalia tu katuni,kwamba tumebadilika sisi wazazi,au tuna upendo sana na watoto au nn yani

Sio kwamba tunawakataza, zama zimebadilika. Hata kama akienda nje, atacheza na nani? Wengine wamejifungia wanakula runinga na tamthilia kama sio homework. Ni mabadiliko tu wala sio jambo la kuwazuia.
 
Mimi nilijifanya bingwa wa kukimbia badala ya kushika mti nikawa nashndana mbio wala sishiki mti nilipigwa mtama nikadondoka chini wacha raia wanishambulie nilijuta sanaa siku hiyo.

Pole sana mkuu, huo mchezo wa kuingiziana tobo ilikua wakinizonga nainua mguu mmoja juu mmoja unabaki umekanyaga chini. Haina namna utaniingizia tobo. Walikua wanadunda utasema wote ni ukoo wa Matumla
 
Lakini mkuu mimi kuna jambo najiuliza,kama sisi tulipitia maisha Yale kwanin leo hii tuwakataze watoto wetu wakirudi shule wasitoke nje ya geti ,,yani tunataka mtoto weekend ashinde kufanya homework na kuangalia tu katuni,kwamba tumebadilika sisi wazazi,au tuna upendo sana na watoto au nn yani
Tatizo hakuna mfumo maalumu wa malezi kila mzazi analea anavyoona yeye ni sawa wazazi wenyewe ndo hawa ASANTE SHULE,anapata rizki kutokana na cheti,bila cheti maisha hayaendi. unategemea atafikiria kumtengenezea mtoto ratiba ya michezo na kumpa sapoti kwenye sanaaa na extra caricular activities nyengine,alafu shida nyengine sawa unaweza ukataka acheze sawa,swali linakuja akacheze wapi?,viwanja vya wazi vingi vimeuzwa na vilivyo wazi havifai ama ndo maskani ya wahuni.
 
Pole sana mkuu, huo mchezo wa kuingiziana tobo ilikua wakinizonga nainua mguu mmoja juu mmoja unabaki umekanyaga chini. Haina namna utaniingizia tobo. Walikua wanadunda utasema wote ni ukoo wa Matumla
Hahahahaha inaonekana ulikuwa mbabe.
 
Hahahahaha inaonekana ulikuwa mbabe.

Sikuwa mbabe mkuu, jamaa kama mpira ni mdogo wanakuja wanakulazimishia kwa nguvu, ukifungua miguu kidogo tu kosa.
Na ule wembamba, nikaona isiwe kesi, wakinisogelea tu,nainua mguu au nakaa chini kabisa. Unaweza kutema ulimi kwa zile ngumi.
 
Mtu akishika hiyo faulo mkabaji yupo zero distance na chandimu. Kupiga na vidole tuliita dochi
 
Back
Top Bottom