TheChoji
JF-Expert Member
- Apr 14, 2009
- 5,771
- 17,849
Sidhani kama kuna mtu anaekataa kusaidia wazazi wake kwa kadri ya uwezo alio nao. Ishu hapa ni kwamba tunalaumiwa watoto wa kiume kwamba hatuwajali wazazi ukilinganisha na watoto wa kike wanavyowajali. Ndio tukasema moja ya sababu inayopelekea hilo ni wanaume kusongwa na majukumu mengi kuliko wanawake.KAma wazazi wako wamekufukuza maana yake hawawezi kukuhudumia,so unatakiwa uwaze kwamba kama hawawezi kukuhudumia maana yake inatakiwa uwasaidie.
Lakini pia kama wamekufukuza kwa roho mbaya zao,unatakiwa ujiulize kwa nini hawakukufukuza wakati unanyonya ? Ni kwa sababu wakati huo usingeweza kujitegemea.
So usijekuleta propaganda yoyote ili ujitoe kwenye ustaarabu wa kuwasaidia wazazi pale unapopata uwezo,kuwasaidia wazazi ni jambo la mtoto.
UNadhani nani atamsaidia mzazi anapokwama ?
Haya mambo ni kubadilishana,mzazi humkuza mtoto na mtoto amsaidie mzazi anaposhindwa.
huo ni ufahamu wako mkuu.
Lengo hapa nikuwainua wazazi kwanza then unaoa.
Unakuta wazazi kula shida mahitaji ni tatizo,kama kuna means yoyote ya kuwafanyia inatakiwa uifanye ili kula isiwe tatizo kwao na mahitaji madogomadogo then ndio unavuta jiko.
LEngo sio wazazi uwafanye wawe matajiri hapana lakini kuna ile kuwasapoti na kuhakikisha kwamba kula kwao hakuwapi shida,na mahitaji madogo madogo ya kila siku sio tatizo.
Lakini mtu anapapatua ndoa huku wazazi kula ni kwa mashaka,huu sio uungwana.
Ikumbukwe kuwa kila mtu anapofikia umri fulani inabidi awe na familia yake regardless ya uwezo wa kifedha. Hata wazazi wenyewe wanatambua hilo. Ndio mfumo wa maisha ulivyo. Na ukishakua na familia automatically majukumu yanaongezeka na msaada lazima utapungua.
Sidhani kama kuna mwanaume awe kweli ana maisha mazuri anaishi kifahari halafu wazazi wake wanakosa chakula au pakulala huo utakua ni utaahira.