Kesi hiyo iko relevant kabisa NA hii ya watoto WA Marehemu Mzee Mengi.
Hapo kwenye post yangu ys awali Mimi nimejaribu kufafanua motives zilizomsukuma huyo Mzee kuandika wosia, lakini wosia wenyewe halisi WA mzee huyo ulikuwa mfupi kabisa .Yeye kwenye wosia wake alieleza KWA kifupi kabisa.Nakumbuka baadhi ya maneno yaliyoandikwa kwenye wosia wake yalielekeza kama hivi:-
"akiwa NA AKILI zake timamu, bila ya kulazimishwa au kushawishiwa NA MTU yeyote yule, NA KWA mapenzi yake ya dhati kabisa dhidi ya mjukuu wake, ameamua KWA hiyari yake mwenyewe kukabidhi urithi WA Mali zake zote KWA mjukuu wake huyo endapo kama yeye atafariki dunia. Asitokee MTU mwingine yoyote kumwingilia haki yake hii"
Kumbuka, Wosia huo haukueleza sababu yoyote ile ya kuwanyima urithi WA Mali watoto wake, licha ya kwamba alikiri kwenye wosia huo kuwa ana mke NA watoto NA watoto watano.
Nakumbuka Kesi hiyo ilipofikishwa Mahakama Kuu ilikuwa chini ya Jaji Mihayo, NA mwishowe iliamriwa kuwa urithi wote wa Mali za marehemu akabidhiwe mjukuu wake, na watoto WA marehemu walinyang'anywa Mali zote.