Shule ya chekechea mjini Huzhou mkoani Zhejiang, mashariki mwa China Novemba mosi ilifanya shughuli ya “Darasa la mashambani”, ambako watoto walikwenda mashambani kujifunza ujuzi wa kilimo kupitia njia ya kuchora picha za mavuno, kutambua mimea ya mpunga na kutengeneza sanamu ya kuwinga ndege.