Watoto wa Tanzania wafanyiwa upasuaji wa moyo kwa mafanikio kwa kutumia teknolojia mpya iliyoanzishwa na China

Watoto wa Tanzania wafanyiwa upasuaji wa moyo kwa mafanikio kwa kutumia teknolojia mpya iliyoanzishwa na China

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
微信图片_20250220100102.png

Machozi ya furaha yalitiririka mashavuni bila kujizuia baada ya Husna Shabaan Kingwande alipofahamu kwamba upasuaji wa moyo wa mtoto wake Ikram mwenye umri wa miaka mitatu ulifanyika kwa mafanikio.

Upasuaji huo uliofanyika katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyojengwa na Wachina, jijini Dar es Salaam, jiji kubwa katika mwambao wa Bahari ya Hindi nchini Tanzania, ulionesha hatua kubwa katika kuleta teknolojia ya juu ya matibabu ya China nchini Tanzania.

Ikram alikuwa mmoja wa watoto watano, wenye umri wa kati ya miaka mitatu na saba, ambao walifanyiwa upasuaji wa mishipa ya moyo kwa kutumia “PAN-Procedure”, mbinu ya uvamizi mdogo iliyoanzishwa na Profesa Pan Xiangbin wa Hospitali ya Fuwai ya China.

Upasuaji huu wa kimapinduzi, ambao unategemea picha ya ultrasound badala ya mbinu ya zamani ya fluoroscopy, hutibu magonjwa ya mishipa ya moyo kupitia mishipa ya pembeni ya damu bila kuhitaji upasuaji wa moyo wa kuchanwa wazi au kupigwa na mionzi.

Upasuaji huo ulifanywa na timu ya wataalam watano wa afya kutoka China, wataalamu sita wa Tanzania kutoka JKCI, na mjumbe mmoja wa timu ya 27 ya madaktari wa China waliopo katika taasisi hiyo.

Kwa Husna, mwenye umri wa miaka 22, mzaliwa wa mkoa wa Pwani nchini Tanzania, upasuaji wa mtoto wake wa mafanikio unamaanisha mustakabali mwema kwa mvulana huyo ambaye aligunduliwa kuwa na tatizo hilo miezi tisa iliyopita.

“Nawashukuru kwa dhati madaktari wa China na wenzao wa Tanzania kwa kumpa maisha mapya mwanangu,” alisema huku machozi yakimtiririka mashavuni.

Mwingine aliyewashukuru madaktari hao ni Ajili Anthony Msunza, baba wa watoto wawili kutoka mkoani Mbeya, ambaye mtoto wake Noreen mwenye umri wa miaka mitano alikuwa miongoni mwa watoto wagonjwa.

"Teknolojia hii mpya imefufua matumaini kwa wagonjwa wa moyo nchini Tanzania," alisema.

Violet Samuel Mkonwa, mama mwenye umri wa miaka 40 kutoka Shinyanga, kaskazini mwa Tanzania, alieleza kufarijika kwake kwamba mtoto wake Emmanuel mwenye umri wa miaka mitano sasa ataweza kwenda shuleni bila matatizo ya kiafya.

Upasuaji kwa kutumia njia ya PAN unawakilisha maendeleo makubwa katika matibabu ya moyo.

Wakati darasa la mafunzo katika hospitali ya JKCI, Pan alieleza kuwa mbinu hiyo inaruhusu wagonjwa kuwa macho wakati wa matibabu, na kuondoa hitaji la kutumia maabara ya catheter yenye mionzi.

"Upasuaji huu sio tu kuwa ni salama na wenye ufanisi zaidi bali pia hufanya matibabu ya moyo kupatikana katika kliniki za jamii," alisema.

Mafunzo hayo yalishirikisha madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo wapatao 50 kutoka Tanzania akiwemo Theophylly Ludovick, daktari wa watoto wa JKCI ambaye hivi karibuni alipatiwa mafunzo ya mbinu za “PAN-Procedure” nchini China.

Ludovick alisisitiza uwezo wa utaratibu huo katika kukabiliana na mzigo mkubwa wa Tanzania wa magonjwa ya mishipa ya moyo, ambapo mtoto mmoja kati ya 100 ana matatizo ya moyo aliyozaliwa nayo.

"Ushirikiano huu kati ya China na Tanzania ni hatua muhimu katika kuokoa maisha na kuimarisha uhusiano wa nchi hizi mbili," alisema.

Mkurugenzi mtendaji wa JKCI Peter Kisenge alielezea ushirikiano wa muda mrefu wa taasisi hiyo na China uliorasimishwa kupitia maelewano ya makubaliano na hospitali ya Fuwai.

Makubaliano hayo yanajumuisha kupima na kutibu watoto wenye magonjwa ya moyo ya kuzaliwa na mafunzo ya juu kwa wafanyakazi wa JKCI. Zaidi ya watoto 1,000 wamepimwa, na wengine kadhaa wakifanyiwa upasuaji wenye mafanikio wa “PAN-Procedure”.

Kisenge alisema teknolojia hiyo mpya inaweza kuongeza uwezo wa taasisi hiyo kwa kiasi kikubwa, hivyo kuongeza idadi ya upasuaji kwa mwaka kutoka 783 hadi 2,000.

"Uvumbuzi huu sio tu unashughulikia kiwango kikubwa cha maambukizi ya magonjwa ya mishipa ya moyo, bali pia unaimarisha uhusiano kati ya China na Tanzania," alisema.

Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2013, kwa msaada wa serikali ya China, JKCI imekuwa kituo kikubwa na cha juu zaidi cha matibabu ya mishipa ya moyo katika Afrika Mashariki. Kuanzishwa kwa teknolojia ya kisasa kama vile “PAN-Procedure” kunaendelea kujenga urithi wake, kutoa matumaini kwa maelfu ya familia za Kitanzania na kukuza uhusiano wa kina kati ya mataifa hayo mawili.
 
Back
Top Bottom