Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Hili tabaka la wapigiwa kura na wapiga kura linazidi kuonekana. Rafiki yangu siku nyingi aliniambia wapigiwa kura hata wakiugua hawatibiwi katika zahanati zetu zilizojaa paracetamol.
Watoto wao wanasoma Feza na hata ikitokea watoto wao wakumbane na mkono wa sheria, polisi atalala kwenye ofisi ya Mkuu wa kituo na jioni atapelekewa kiepe, mishikaki na soda ya baridi.
Mtoto wa huku kwetu Kwamtogole angemtamkia l Askari maneno yale, sasa hivi tungekua tunatoa maamuzi ya kuzika au kusafirisha.
Lakini hii ndiyo Tanzania yetu.