Watoto wa wasanii na ushoga! Kipenga kimepulizwa rasmi

Watoto wa wasanii na ushoga! Kipenga kimepulizwa rasmi

Hizi familia zina siri kubwa,ukiona mosh unafuka ujue.....all in all kila mtu anayatafsir maisha yake kwa moyo wake ndo maana tupo hapa tulipo
 
Wazazi tuombeana sana. Na tuwaombee sana watoto wetu, vijana wetu.. Kuna walakini mkubwa sana kwenye ile kampeni ya wakataa ndoa. Tuwe karibu mno na vijana wetu wa jinsia zote wakike na wakiume .. Wote wanaharibika. Wote wanaharibikiwa jamii inaingia kwenye mtanziko mkubwa.. Kizazi kijacho kiko mashakani

Wasanii wetu ni role models wa vijana wetu. Vijana wetu, watoto wetu hutamani, huwa na ndoto za kuwa kama fulani, kuna hatari kubwa sana kupotosha na kupoteza wengi kama msanii ama mtu maarufuvakiongea kitu

Hapo mwanzo tulizoea vijana barobaro wakijitangaza mitandaoni kuwa wao ni mashoga..haikuwa mbaya sana kwakuwa hawakujulikana na wengi.. Leo hii anjitokeza kijana wa kiume wa msanii maarufu anajitangaza hadharani kuwa yeye ni shoga ana anajivunia (ushoga[emoji24]). Huyu ana followers wangapi Yarab toba!

Kipenga cha kujitangaza live kimepulizwa rasmi Tanzania, viongozi wanapiga kimya kama hawaoni.. Tunapoteza kizazi kijacho.

Ushoga umetamalaki nchini lakini mamlaka hazina nguvu hata chembe ya kukemea.. Madhara ya kukubali mikopo na misaada yenye masharti kificho

Lifestyle wanayowalea na kuwakuza watoto wao hawa tunaowaita wasanii maarufu Tanzania ni janga kubwa.. Hafundishwi kuwa wanaume kamili hawafundishwi ukakamavu.. Wanalelewa kuwa wanaume wa kike ama wanawake wa kiume... Wengi wakilelewa na mzazi mmoja.

Hakuna wa kukemea.. Zaidi ya sisi wapiga kelele mitandaoni. Tuhamasishane sisi wazazi wa huku kuwalinda vijana wetu, tuongee nao tuwe nao karibu tuwachunguze kwa karibu mienendo yao, marafiki zao nknk

Tunataka nasi tuache mbegu itakayomea na kuendeleza kizazi.. Tupunguze harakati za kimaisha tutenge muda wa kutosha kuwa na vijana wetu... Hali ni mbaya sana.

Kampeni ya kataa ndoa ni kampeni ya kishenzi, isipewe nafasi haina malengo mazuri kwa maisha ya kesho na wengi wameivamia kwa ujuaji tu wa kitoto. Hawajui matokeo yake!

Madhara ya hii kampeni ikiachwa imee yataonekana soon.. Huko mavyuoni hali ya ushoga na usagaji ni mbaya sana huko kwenye mitandao ya kijamii ndio usiseme.

Kijana anamaliza chuo ni msagaji, kijana anamaliza chuo ni shoga! Kuna familia tena hapo? Kuna ndoa tena hapo? Kuna future tena hapo?

Kama mtoto wa Monalisa kajitangaza akamewe wazi na awe ni wa mwisho. Hili likiachwa janga kubwa linakuja. Zamani tuhuma za aibu za ushoga zilikuwa maeneo ya mwambao .. Siku hizi mpaka chuga ni kama fasheni

Inauma sana!
Mtoto akielekezwa kuzifuata njia zinazompndeza Mwenyezi Mungu akikua atazifuata.

Siku hizi single parent imekuwa kama fasheni. Malezi ya pande mbili ni muhimu sana aiseee.
 
Kimbe na humu wamo? Jamani si miwataje majina waone aibu.

Mama asiposema chochote kuhusu ushoga vijana wa kiume wanaisha.
Connection ya Zenji inatisha[emoji24][emoji24][emoji24]
 
Kiukweli kuna Watu mnapenda kujipa kazi sana,
Hivi hata mambo ya mitandaoni mnaumizwa nayo kiasi hiki jamani!?
Kama wakerwa sana na kitu jiepushe nacho, hupendi kuwaona hao humu JF basi jitoe wewe ili ubaki na Amani,

Dhambi ya Ubaguzi ni mbaya na hua haina kikomo,
Kuna single moms humu hutukanwa kila leo, kuna wale wa Dini hutukanana kila leo, huko kwenye Siasa ndio balaa, sasa wewe kuliko kuamrisha wenye Forum wawafungie watu usiowataka ni aidha wewe ujitoe au usishiriki kabisa kwenye mada za namna hiyo,

Ila ajabu kila Mada za Ushoga nawe umo, sijui wataka tukueleweje.
Vp mkuu? Ile mimba tayari ishaingia?
 
Back
Top Bottom