Watoto wa Wasira waliojiunga CHADEMA watoa ufafanuzi juu ya uhusiano wao na Waziri Wasira

Watoto wa Wasira waliojiunga CHADEMA watoa ufafanuzi juu ya uhusiano wao na Waziri Wasira

Political promo hiyo wameshapata, baadae watakuwa na kazi ndogo tuu kuwakumbusha wa TZ pindi watakapokuwa na nia ya kugombea nafasi yoyote, wasiwalaumu waandishi kama ni kweli wana nia ya kufika mbali kisiasa.
 
Dr. Wassira aka mtemi wa Mahale Pangua hoja hiyo.......watoto wa kaka yako ni nani kwako?
..Yule mzee oppportunist tu hana lolote kwa jinsi alivyo-appear kwenye TV anavyowakana hao mabinti utadhani ametenda dhambi ya kula nyama ya mtu wakati ni watoto wa mdogo wake waliyezaliwa pamoja kisa kuwaogopa magamba!!....Bure kabisa bora arudi gombe tu!!
 
Political promo hiyo wameshapata, baadae watakuwa na kazi ndogo tuu kuwakumbusha wa TZ pindi watakapokuwa na nia ya kugombea nafasi yoyote, wasiwalaumu waandishi kama ni kweli wana nia ya kufika mbali kisiasa.

Umenena vyema
 
Nam support Wassira kuliweka wazi kuwa wale sio wanawe na kwamba wa ndugu yake... ingawa kauli yake inaonesha wazi ni namna gani amekereka; .

Wasira atueleze mashambulizi aliyoelekeza kwa Dr Slaa ya kutafuta umaarufu kwa mgongo wa jina lake anayasemeaje? Au ataomba radhi?
 
Wasira atueleze mashambulizi aliyoelekeza kwa Dr Slaa ya kutafuta umaarufu kwa mgongo wa jina lake anayasemeaje? Au ataomba radhi?

Omulangi, hivi hilo nalo la kuomba radhi? Mie naona la kuomba radhi ni lile la kumbwa Dr. Slaa ache kuita wake za watu chumbani... Nimeshangaa sana kuwa mtu unasimama mbele ya media na kuzunguza kuwa anatoa ushauri kwa Slaa kuwa makini anaopoita wanachama kuwapa card. That was way too low...
 
hawana lolote hawa wanatafuta umaarufu tu. pengine ukute wametumwa na baba yao kuja kuivuruga chadema tu hawa ni wa kuwaangalia kwa umakini sana
 
430526_451646281552922_1087214431_n.jpg

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI UFAFANUZI KUHUSU SISI KUJIUNGA NA CHADEMA NA MALUMBANO KUHUSU MAJINA YETU


Tarehe 30/09/2012 mimi Esther Wasira na dada yangu Lilian Wasira tulijiunga na CHADEMA na kukabidhiwa kadi na Katibu Mkuu wa CHADEMA Mh. Dr Willibrod Slaa. Tulielezea kwa kirefu sababu za sisi kujiunga CHADEMA na tukasisitiza kuwa tumeridhika kuwa CHADEMA ni chama chenye dhamira safi ya kuiongoza Tanzania na kwamba ni chama kinacholeta matumaini mapya ya kuijenga Tanzania mpya yenye neema. Waandishi wa habari walijaribu sana kutudodosa kujua tuna uhusiano gani na Waziri Steven Wasira.

Tulielezea wazi kuwa mahusiano yetu ya kifamilia hayahusiki na sababu na dhamira yetu ya kujiunga CHADEMA. Hata hivyo tulielezea kuwa Waziri Steven Wasira ni baba yetu mdogo ambaye alinyang'anyana ziwa na baba yetu mzazi, wakili George Wasira. Tulidhani hiyo ilitosha na lisingekuwa swala tena la kujadili na badala yake hoja ya kujadiliwa ingeweza kuwa sababu tulizozieleza za kujiunga CHADEMA. Tunasikitishwa sana na malumbano yaliyofuata baada ya hapo kuhusu kama sisi ni watoto wa Wasira au la.

Kama tulivyoeleza, tumejiunga CHADEMA kwa sababu tulizozieleza hapo awali na wala si kwa sababu nyingine yeyote. Hatujajiunga CHADEMA kumdhalilisha mtu, kumfedhehesha mtu au kukipatia umaarufu CHADEMA kwa vile tu tunatumia jina la Wasira.

CHADEMA ni chama cha siasa tena chenye wanachama na wafuasi wengi Tanzania hivyo si kashfa bali ni fahari kubwa mtu kujiunga CHADEMA na tena ni ushahidi wa mtu kujitambua. Pia CHADEMA ni Chama maarufu sana Tanzania kwa sasa hata pengine ni maarufu kuliko CCM hivyo hakihitaji kujipatia umaarufu kwa mgongo wetu. Sisi tunawaheshimu sana wazee wetu na tutaendelea kuwaheshimu ila linapokuja swala la chama cha kujiunga linabaki kuwa hiari yetu kwa kuzingatia sera za chama na uwezo wa chama husika katika kujenga Tanzania tunayoitaka na hilo ndilo lililotupeleka CHADEMA. Na hii ni haki yetu ya msingi kabisa inayolindwa na Katiba ya nchi hii chini ya ibara ya 20(1).

Ikumbukwe kuwa mmoja wa Waanzilishi wa CHADEMA ni Mzee Wasira. Dhamira ya kuanzisha CHADEMA ilikuwa ni kushika dola na hili ndilo CHADEMA imekuwa siku zote inajaribu kuwashawishi Watanzania kuwa sasa wamekomaa na wanastahili kuchukua dola. Kwa vile kuchukua dola ilikuwa ndio ndoto ya baba yetu mzazi Mwanzilishi wa CHADEMA, sisi kama watoto tumejiunga na M4C ya CHADEMA ili tuweze kutimiza ndoto ya baba yetu kuwa CHADEMA siku moja ichukue jukumu la kuiongoza Tanzania.

NB. Wameweka namba zao za simu kwa busara nisingependa kuzianika hapa.

Kwa hisani ya Mjengwa Blog.
 
Nimeona nitoe ufafanuzi kwa umma......! Hawa sio watoto wangu wa kuzaaaa.......! Hili zee linasikitisha sana! Yaani unawakana wanao kwa sababu ya chama? watoto wa kaka yako ni watoto wa nani? After all nani alitaka ufafanuzi huo!
 
Mkuu hii habari ilishawekwa na namba zao ziliwekwa. Asante kwa taarifa
 
Nafikiri siku mke wake akijiunga na cdm, atasema huyo sio mke wangu wa ndoa, kwikwi kwii! Wanasiasa wa Tanzania kila walipö ni siasa tu, akipewa nafasi ya kusalimia hata msibani usishangae kidumu.......malizien!
 
Nimeona nitoe ufafanuzi kwa umma......! Hawa sio watoto wangu wa kuzaaaa.......! Hili zee linasikitisha sana! Yaani unawakana wanao kwa sababu ya chama? watoto wa kaka yako ni watoto wa nani? After all nani alitaka ufafanuzi huo!

Imagine huyo ndio kiongozi anayetegemewa na CCM!...No wonder kuna madudu mengi ktk uongozi wa nchi hii.
 
Hata kwa muonekano wa sura wanaonesha tu kuwa si wa kwake wa kuzaa bana................
 
Back
Top Bottom