Watoto wa Wasira waliojiunga CHADEMA watoa ufafanuzi juu ya uhusiano wao na Waziri Wasira

Watoto wa Wasira waliojiunga CHADEMA watoa ufafanuzi juu ya uhusiano wao na Waziri Wasira

Hata kwa muonekano wa sura wanaonesha tu kuwa si wa kwake wa kuzaa bana................

Whether wanafanana hawafanani na Wasira ni watoto wa kaka yake! What is wrong with you! Kitendo cha kujitokeza kwenye vyombo vya habari na kusema hawa sio watoto wangu........ simply wamechukua kadi za CHADEMA
 
Nilimuona Esta Wasira jana akihojiwa na EATV kuhusu vikwazo katika maendeleo ya vijana. Huyu dada ni jembe anazungumza kwa kujiamini na ana uwezo mkubwa sana wa kujieleza. Nape hafiki hata robo yake. Alieleza kuwa kikwazo kikubwa cha maendeleo ya vijana ni sera mbovu za CCM.

Alisema CCM inatoa majibu rahisi kuwa vijana wajiajiri na kulaumu kuwa vijana ni wavivu bila kujibu swali kuwa taifa la vijana linajengwa. Ujasiriamali, maadili, uzalendo, utaifa na ubunifu unajengwa si kwamba unatokea kwa bahati mbaya. CCM imeshindwa kujenga hayo hivyo vijana si wakulaumiwa.

Alisema ukiwaangalia wamachinga wanaouza vitu vidogovidogo wana jitihada sana ila uwezo wao wa mtaji, ubunifu, elimu ya ujasirilimali inaishia pale. Serikali inastahili kulaumiwa kwa haya.

Ameelezea pia kuwa rushwa katika ajira kwa maana ya kujuana ni kikwazo pia cha maendeleo ya vijana kwamba kazi zinatangazwa kama formality lakini watu walishapatikana. Hii inafanya vijana wasio na brains kushika nafasi za kazi wasioziweza wakati wale wanye brains wapo mitaani.

Aliwaasa vijana kujiunga na M4C kwamba sasa ni wakati wa mabadiliko na vijana hawapaswi kulala ila waamke na wahakikishe 2015 wanabadilisha mfumo wa uongozi, wana "reclaim their Country from CCM" Kipindi hicho kitarudiwa:

Today (4/10/2012) at 2pm (1400hrs)
Sunday (7/10/2012) at 4pm(1600hrs)..
 
Mzee wa Gombe akimsikia atamlaani huyo mtoto.
 
hii reference ya nape uliyoitoa imenichefua .... intake radhi
 
Ndio maana mzee wake alianza kumkana mapema nahisi anamjua vizuri.
 
Nilimwona ,wakipatikana warembo wenye akili kama wale itasaidia sana M4C.
 
Nimeipenda, Chadema inazidi kusajili majembe inauza vilaza kina Diwan.i kule Aton.
 
..hiki ndicho mnachoambiwa kila siku utamuitaje jembe wakati ndo kahamia juzi tu,mtakuja kuwapokea kina chibuda wengine,fikiri kabla ya kutenda amuwezi jua wamekuja kufanya nini mtawakana muda si mrefu
 
Tunataka wapiganaji wa ukweli CDM co wa kuongeza idadi tu. tnx god for that
 
Ukitaka kumlaani mtu, kwanza unavua nguo zote unabaki uchi wa mnyama, halafu ndiyo unatoa laana yako.

Swali Je Wassira yuko tayari kuachia nyeti zake nje? Taking into consideration waandishi wa habari watakuwepo, maana Mzee Wassira ni mtu wa media?

I cant see this happening! I stand to be corrected.
 
nahisi anataka kua mbunge huyu..aliona ccm hakukaliki akaamua kuswitch sides sio
 
.....
Ameelezea pia kuwa rushwa katika ajira kwa maana ya kujuana ni kikwazo pia cha maendeleo ya vijana kwamba kazi zinatangazwa kama formality lakini watu walishapatikana. Hii inafanya vijana wasio na brains kushika nafasi za kazi wasioziweza wakati wale wanye brains wapo mitaani.


Hapo kwenye red amenigusa sana, ukiweza kubadilisha hiyo, hakika kuna ajira nyingi sana zitakuwepo, hasa kwa hawa wanoitwa Expatriates. We real need changes in this country, thank u Esther!!
 
Huyu Stephan Wasira asijifanye msafi sana na kuwakana wanawe ambao ingekuwa wanaolewa yeye ndiye angekuwa mstari wa mbele kupokea mahari. Ikumbukwe pia mwaka 1990 alikuwa waziri wa kilimo lakini cha ajabu Mwaka 1995 aligombea jibo la Bunda kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi.

Sikumbuki ilikuwaje akarudi tena CCM. naamini aliona kwa wakati ule NCCR imekuwa na nguvu kubwa kiasi ingeweza kuchukua dola. hata sasa hivi naamini sana kuwa yeye ndiye aliyewashauri hao watoto waende CHADEMA kwani ameshapima upepo akaona ccm hakuna matumaini ya muda mrefu.

Kwa hiyo ili asiwaudhi wezake anajifanya kuwakana, na hao watoto kwa vile wana akili sana wanatoa ufafanuzi ambao hautaudhi upande wowote, kama ikitokea chadema wakachukua dola, mmoja wa hao watoto atakuwa na post kubwa tu kama huyo baba yao mdogo atakua hai kuna siku atasema hadharani kuwa ushauri wake kwa watoto umewaletea mafanikio, tusubiri tu.
 
Back
Top Bottom