Watoto wafundishwe; nature inamtaka mhanga ajihami kwani ndiye anayepata madhara

Watoto wafundishwe; nature inamtaka mhanga ajihami kwani ndiye anayepata madhara

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
WATOTO WAFUNDISHWE; NATURE INAMTAKA MHANGA NDIYE AJIHAMI KWANI YEYE NDIYE ANAYEPATA MADHARA

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Katika Jambo lolote lazima uangalie Nafasi yako ni Ipi. Je wewe ni mshika mpini au mshika Makali. Je wewe ni Mhanga au unayesababisha madhara.
Hii itakusaidia kuishi Kwa tahadhari na Maisha yako yanauwezekano Mkubwa wa kuwa ya Amani.

Mhanga ni Mhusika au Mtu yeyote àmbaye anapatwa na madhara mengi au Makubwa hanayoonekana kirahisi ukilinganisha na aliyemsababishia.

Mfano no 1; kwèñye suala la mapenzi na Ngono. Mwanamke ni Mhanga huku mwanaume akiwa siô Mhanga. Mwanamke Kabla ya kuingia kwenye mapenzi au Kabla hujafanya Ngono lazima ujue Nafasi yako ni Ipi kwèñye huo mchezo.
Wewe ni Mhanga Kwa sababu baàda ya kufanya Mapenzi au ngono Matokeo mengi hutokea kwèñye mwili wako Kuliko Mwanaume hivyo lazima wewe ndiye uhakikishe unajihami.

Kama hautaki Mimba ni Bora ujikinge mwenyewe pasipo kumtegemea Mwanaume. Tumia uzazi wa mpàngo.

Madhara ya kutokujihami utaanza kuyaona baàda ya tukio kufanyika.
Kama vile ukipata Mimba ukatelekezwa atakayelaumiwa siô Mwanaume Bali wewe.

Majina Mabaya na kejeli za kîla namna zitakuwa juu yako upende usipende.

Nature ya huu ulimwengu haitambui utashi wa binadamu katika kutunga Sheria za kuwafanya Watu wawe waungwana. Nature haijui kuhusu kuwa Dini au Imani inakataza Jambo Fulani. Nature haijui hayo. Nature haijui kama serikali Kwa utashi waô walitunga Sheria za namna Ipi. Nature haidanganyi.

Nature inajua kuwa kûna Predator (mwindaji au MLA nyama) na Prey (kitoweo au anayeliwa) Nature inatambua kuna Mwenye Ñguvu na kûna dhaifu. Kûna watawala na watawaliwa.

Wale dhaifu lazima wajihami zaidi Kwa sababu nature haipo upande waô.

Unapokuwa katika ushirika na Mtu aliyekuzidi Ñguvu hata kama mnauhusiano wa namna Ipi chukua tahadhari kuwa wewe Nafasi yako ni Ipi wewe utabaki kuwa Mhanga tuu hivyo lazima ucheze kete zako Vizuri.

Wanawake hulalamika pale wanapoona wanakejeliwa kwèñye baadhi ya ishu hasahasa Mapenzi na ngono wakiitwa majina Mabaya, kama makahaba, Malaya, single mother na Kejeli nyinginyingi huku Wanaume wakiwa hawatukanwi.

Ndivyo ilivyo ukiwa upande wa chini lazima ukandamizwe. Hiyo ni Nature. Ndîo maana lazima umwambie Binti yako na kumfundisha ajue Nafasi Yake kuwa kama ni mwanamke basi atabaki kuwa mwanamke tuu na yupo upande wa Chini hivyo yeye ndiye atakuwa Mhanga.

Lazima umwambie ajitunze, ajiheshimu na asijilinganishe na Wanaume Kwa sababu Wakati yeye akibeba Mimba huyo aliyempa Mimba atakuwa akipewa Sifa kemkemu huku yeye akikejeliwa na kupondwa kuwa ni Malaya na asiyeweza kukataa.

Wakati aliyemzalisha na kumtelekeza akiendelea na Maisha yake Kwa amani na utukufu wewe Binti utakuwa unahangaika kutafuta Mwanaume Mwingine huku ukiitwa Majina ya dharau na Kejeli na kudhihakiwa kama single mother.

Wewe unayepatwa na madhara mengi ndiye unatakiwa ujihami zaidi kuliko kutegemea msaada wa Sheria zilizoundwa Kwa utashi wa binadamu àmbazo nyingi zîpo kinyume na Nature.

Hakuna Dini Wala serikali àmbayo utaweza kuzuia Mhanga asipatwe na maswahibu Kwa Yale aliyoyafanya.

KISIASA Huwezi kupambana na serikali (mwenye Ñguvu) hata kama serikali inakosea nature haitambui Jambo Hilo ila utashi wa binadamu àmbao wameunda Sheria za kidini na Kisiasa ndîo huweza kuona Makosa. Ikitokea unapambana na serikali elewa kuwa wewe ndiye utakuwa Mhanga na utaumia hata kama baadaye Watu waseme hiyo haitabadili ukweli kuwa utakuwa umeumizwa vilivyo.

Hivyo Jua Nafasi yako. Jitambue.
Haki Sawa lakini hazilingani.

Nawatakia Sabato Njema

Acha nipumzike sasa

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam
 
Mfano no 1; kwèñye suala la mapenzi na Ngono.
Mwanamke ni Mhanga huku mwanaume akiwa siô Mhanga.
Mwanamke Kabla ya kuingia kwenye mapenzi au Kabla hujafanya Ngono lazima ujue Nafasi yako ni Ipi kwèñye huo mchezo.
Wewe ni Mhanga Kwa sababu baàda ya kufanya Mapenzi au ngono Matokeo mengi hutokea kwèñye mwili wako Kuliko Mwanaume hivyo lazima wewe ndiye uhakikishe unajihami
Wanajihami ndio maana tunawapa hela ili lolote likitokea basi tushamalizana malipo
 
Mkuu hapa:

"Ikitokea unapambana na serikali elewa kuwa wewe ndiye utakuwa Mhanga na utaumia hata kama baadaye Watu waseme hiyo haitabadili ukweli kuwa utakuwa umeumizwa vilivyo."

Kwenye haki yetu, usitutishe!

Pàmoja na kupambania Haki yako lazima ujue Nafasi yako vinginevyo utapigwa na Haki yako hutapata.

Tumeshaona hayo.
 
mhanga maana yake umeathiriwa, iwe kidogo au sana,

kwahiyo inategemea,

hapo kwa wanawake, mimba zisizotarajiwa zinaathiri wote mwanamke na mwanaume, ndo maana wanaume wanakimbia wanaogopa kulea

hapo kwenye serikali pagumu, kama ukipambana na serikali ukaweza kusababisha muamko fulani kwa watu basi umeiathiri

Mimba inamuathiri Mwanaume kama aliyempa Mimba ni mwanafunzi nje ya Hapo Mwanaume Hana mazîngira ya kukimbia Mimba
 
Mimba inamuathiri Mwanaume kama aliyempa Mimba ni mwanafunzi nje ya Hapo Mwanaume Hana mazîngira ya kukimbia Mimba
Robert na ubishi wako😅 ngoja nikupe kisa;

Baba mzazi wa Jeff Bezos, aliachana na mzazi mwenzake, Jeff akiwa mdogo sana. Hakujihusisha na maisha ya Jeff tena.

Jeff alilelewa na baba wa kambo, akaja kuwa moja kati ya watu matajiri duniani.

Mwandishi mmoja wa habari akiwa anaandika kitabu kuhusu historia ya Jeff, akamfuatilia na akaweza kukutana na yule baba mzazi.

Yule baba mzazi baada ya kupashwa habari alisema, 'Sitaki pesa zake, nataka nipate kumuona ili niombe msamaha kwa kosa kubwa nililofanya maishani mwangu'
 
Robert heriel unashindwa kutofautisha kati ya nature na nurture. Nurture inaweza kuwa ideal iliyobebeshwa structure na kuleta maana sawa na nature. Nature ni something else, beyond your opinion na inaweza kutofautishwa na nurture kwa kufanya comparative study
 
Nimezungumzia nature siô nurture Mkuu.
 
Robert na ubishi wako😅 ngoja nikupe kisa;

Baba mzazi wa Jeff Bezos, aliachana na mzazi mwenzake, Jeff akiwa mdogo sana. Hakujihusisha na maisha ya Jeff tena.

Jeff alilelewa na baba wa kambo, akaja kuwa moja kati ya watu matajiri duniani.

Mwandishi mmoja wa habari akiwa anaandika kitabu kuhusu historia ya Jeff, akamfuatilia na akaweza kukutana na yule baba mzazi.

Yule baba mzazi baada ya kupashwa habari alisema, 'Sitaki pesa zake, nataka nipate kumuona ili niombe msamaha kwa kosa kubwa nililofanya maishani mwangu'

Hapo Mhanga siô Babaake Jeff Bali ni Jeff na Mamaake.
Hiyo ya Jeff kuwa tajiri ni neema tuu àmbayo tunaita exceptional.

Huyo Mzee siô Mhanga Kwa sababu yeye ndiye chanzo cha matatizo. Anachofanya ni kutubu Kwa kumfanya Mtoto wake Mhanga.

Wewe umemuibia MTU ukamkat na mapanga. Aliyeibiwa ni Mhanga. Wewe kwenda kumwomba Msamaha uliyemuibia haugeuki kuwa Mhanga.
 
Nimezungumzia nature siô nurture Mkuu.
Ndio mana nasema wewe unashindwa kutoa gepu lililopo katika hivyo viwili katika maelezo yako. Fanya comparative studies kwanza mana mifumo inayosababisha mwanamke kuwa muhanga sio nature ni mifumo yenye idea za man muscular, ukienda kwenye mifumo ya matriach unaweza kuta mambo tofauti. Na hapo tutaanza kuuliza maswali kwqmba nature ni nn na nurture ni nn
 
Kwèñye hii Dunia huo mfumo wa matriach upo Asilimia ngapi ukilinganisha na patriach?

Unàtaka kusema kwèñye ngono Mwanamke siô Mhanga ila amefanywa kuwa Mhanga??
 
Utumwa hautakuja kuisha Duniani.

Mbona Mpaka Sasa tupo utumwan au hauoni

Ndiyo maana bila kujali maguvu yao wenye akili zetu tutaendelea kukomaa nao.

Kuna waliionyesha njia kuliko wamasai wa Loliondo au manguli wa HAMAS, Palestina au Hezbollah?

"Ni heri kufa ukipigania uhuru kuliko kuishi utumwani."

Maneno hayo ni mageni kwako?
 
Back
Top Bottom