Kwanza kabisa tujifunze kutofautisha kati ya nature na social constructs ukweli ni kwamba mwanamke siyo mhanga ila amefanywa kuwa mhanga na kwa bahati nzuri au mbaya hiyo ilifanya kazi kwenye ancient na medieval eras, ila kwenye hii modern era matokeo yake ndio haya tunayaona wanaume wanalalamika kwamba wanakosa wake wema wa kuoa yani ndoa wanazihitaji ila wanawake wa kuoa ndioa shida, kwa sababu kwa mujibu wao kumejaa ma single mother na malaya hadi kufikia hatua wanaume wengi kujifariji na ile kauli yao ya "kataa ndoa ni utapeli" ilihali wengi tunajua hiyo ni "sizitaki mbichi hizi" tu
Na kuhusu hiyo hoja yako it doesn't always work that way kuna mambo unaweza ukajiona wewe siyo mhanga kwa wakati huo ila baada ya muda mrefu ndio uhanga wako unaanza kuonekana, kwa mfano binadamu anapoyachafua mazingira kwa wakati huo mazingira ndio yanaweza kuonekana mhanga ila in the long run wote tunajua madhara ya mazingira machafu kwa binadamu kwahiyo mwisho wa siku huo uchafuzi alioufanya binadamu utaanza kumrudia mwenyewe, na katika muktadha huo hatuwezi kuyaambia eti mazingira yajitunze yenyewe bali binadamu ndio anasisitizwa ayatunze mazingira sababu mwisho wa siku yeye ndiye anahitaji mazingira yawe masafi ili aweze kuishi
Same applies kwenye muktadha wa mahusiano mwanzoni inaweza kuonekana kama mwanamke ndiye mhanga wa ngono kwa sababu ya hizo social constructs na gender stereotype, ila in the long run wanaokuja kupata shida ni wanaume pale watakapofikia wakati wa kuoa na kukosa wanawake wenye sifa wanazozitaka sababu wengi walishawachezea huko nyuma, kwa kisingizio kwamba wanaopata madhara ni wanawake na siyo wao na matokeo yake wanajikuta na options mbili tu either waoe wanawake hao hao waliopo au wasioe kabisa jambo ambalo ni gumu kwao
Japo najua kwenye maandishi huwa mnajifariji kwamba mnaweza ku hit and run kisha mkitaka kuoa mnaoa vibinti vibichi ila tukija kwenye uhalisia wote tunaona ndoa zinazofungwa kila siku wengi wanaoolewa ni hao hao so called masingle mother na malaya, na wenyewe huwa mnajifariji na kauli kwamba "masingle mother huwa wako matured na wanajua nini maana ya maisha" mara sijui "wanawake watu wazima ndio wanajua nini wanaume wanataka hivi vibinti ni visumbufu tu" na kauli nyingine kama hizo, na ukizingatia mabinti wa siku hizi nao hawataki kuolewa at their prime age wanasubiri wawe broke au rejects ndio waanze kutafuta ndoa so hapo unadhani hasara ni kwa mwanamke tu
Ndio maana mara nyingi huwa nawaambia wanaume kwa dunia ya sasa ili kurudisha maadili kwenye jamii ni either wote wanaume na wanawake wakubali kujitunza ili wanaume waje kupata wake wema wa kuoa, au wote muendelee na uzinzi na uasherati halafu mwisho wa siku mje muoe hao hao wanawake ambao mnadai ni wahanga chaguo ni lenu sababu mwisho wa siku wanaume ndio wanaoangalia tabia njema kwenye ndoa na siyo wanawake, kwahiyo ifike mahali tuache kujifariji kwa kauli mufilisi za mfumo dume ambazo hazifanyi kazi tena kwenye dunia ya leo bali zinalazimishwa tu na ifike mahali tuachane na hizi social constructs na kusingizia kwamba ni nature