Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Hii sijui ni shule gani mwalimu ameamua kutoa elimu kwa watoto juu ya ukatili wanaoweza kufanyiwa ni jambo jema sana katika kupambana na ubakaji na ulawiti kwa watoto, ni jambo linalopaswa kuigwa na shule zote pamoja na wazazi wote, tuweke aibu pembeni tuwaelelze ukweli watoto ili kuwanusuru na janga la ubakaji na ulawiti kwao.
Elimu hii isiishie kwenye ubakaji na ulawiti tu bali hata ukatili wa aina nyingine kwao, lakini tuwafafanulie zaidi juu ya usalama wao wakitoa taarifa kwani wengine huwa wamepewa vitisho wasitoe tarifa tuwaambie hawawezi kudhurika wakitoa taarifa ila ndio watakuwa salama kuliko kukaa kimya na kuvumilia ukatili.