Watoto Walindwe: Mtoto apigwa kama mnyama, ugomvi wangu ni huyu aliyechukua hii video anaroho mbaya sana

Watoto Walindwe: Mtoto apigwa kama mnyama, ugomvi wangu ni huyu aliyechukua hii video anaroho mbaya sana

Hapana mzee,huyu akikua atakuwa mtu mwenye chuki sana na wamama design ya huyo aliyemlea,akina junior ni special case.tunaowaponda akina junior,tulipigwa sana ila sio kwa kukanyagwa kichwa na kubamizwa chini,tena tukiwa na umri kati ya 8-14 maana huo ndio umri wenye kila aina ya wenge.sio hako ka malaika.
huyo dada ndio akina junior wenyewe sasa.
Hawakupigwa ndio maana hawajui namna ya kuadhibu,wanadhani unajipigia tu.
Ni wazi kabisa mtu ambaye hajawahi kupigwa na wazazi wake hawezi kuja kumpiga mtoto wake hata iweje.
 
Kwakweli hii tabia ya kuchukua picha matukio pale inapotokea majanga naona imeanza kushamiri, juzi kitaa palitokea moto kwenye nyumba Fulani jirani, Mara paa motoooo motoooo wananzengo wakatinga, tukajua wanakuja kupambana na janga la moto, muda kidogo tunashanga wanashughulika kuzima na kuokoa ni watu km wanne tu kitaa kizima waliobaki wanachukua tukio zima na simu zao, tuakabaki kuwashangaa tena sie wazima moto,jamani vp ...tena....kwani tumefika episode ya ngapi...Mara zimamoto awo wakakutana na majivu nyumba ishaungua yote.
Kwaiyo iyo tabia ya kuchukua tukio badala ya akuokoa majanga ni tabia mbaya sana ni kinyume na tamaduni zetu sie wabongo....tunapaswa kuikemea haraka sana
 
Mbeya ipi hiyo mkuu? Siyo tabia ya wanyakyusa, Wandali, Wanyiha au Wanyamwanga hii,labda ni tabia yamtu binafsi

Una maarifa kidogo sana mkuu.

Bado upo kizazi kinachoamini kwamba stereotype ya kabila flani wakiwa x basi hutakuja kumkuta mwenye Tabia Y.

Narudia tena una maarifa kidogo mnooo, Panua maarifa
 
Halafu huu ugonjwa wa kuchukua video matukio ya ajabu umeingia watu sana, kiasi mtu anaweza kuwa anaungua moto mtu yuko busy anarekodi.

Kuna moja wadada wanapigana, mmoja akakabwa, kashikwa kisawa sawa mpaka anaanza kurusha miguu, ishara ya kukata roho jitu linarekodi tu mpaka akatulia, kimyaaaa.

Sasa hapa lengo lilikiwa jema tu, kwamba "oneni anachofanya huyu mama" lakini mtoto ndio anateketea sasa.
Kuchukua video siyo vibaya kwa tukio kama hilo anaweza akawa house girl sasa hapo asingeweza kushindana na bosi wake lakini kwa ushahidi huo itasaidia kujua ukweli na muhusika kuchukuliwa hatua.
 
Itashangaza sana kama hii case itaishia hapa jukwaan tu...ni mauaji kabisa hayo..dah yaani nngekuwa karibu sijui ningemfanya nn huyo kahaba
 
Una maarifa kidogo sana mkuu.

Bado upo kizazi kinachoamini kwamba stereotype ya kabila flani wakiwa x basi hutakuja kumkuta mwenye Tabia Y.

Narudia tena una maarifa kidogo mnooo, Panua maarifa
Mm nawewe nani mwenye maarifa mafupi? Maana umedandia gari mbele lazima ugongwe tu
 
Mm nawewe nani mwenye maarifa mafupi? Maana umedandia gari mbele lazima ugongwe tu
Wewe unachukulia kwamba stereo type ikiwa ya kabila flani basi ni kila moja.

Mfano ni mtu huyu akikuwa anaiba watoto haina maana kwamba kabila lote ni wezi wa watoto ,

 
Huyo hawezi kuwa Mama mzazi wa mtoto, atakuwa Mama wa kambo tu.

Au unaweza kuta ni mtoto wa jirani.

Sio kwa kumsulubu mtoto hivyo.

Cha ajabu huyo anaemsulubu huyo mtoto ni mjamzito
 
Bora usiitazame du!! nimeumia sana, mtoto anainuliwa anabamizwa chini anakanyagwa kichwani

Kama ni hapa nchini, wanaharakati lazima watoe tamko na hata bunge liseme neno juu ya jambo hili
Ongezea, na Fimbo anayoitumia kumchapia huyo mtoto ni Fimbo ya kuulia nyoka, ni ile Fimbo kavu iliokauka tunayoiita gongo
 
Wabongo bana. Sasa asingechukua video mngejuaje kuna huu ukatili?
 
Hapo yangekuwa ni maelezo tu,ungeona watu wanakwambia :

"Bila picha au video hiyo ni chai tu kama chai nyingine" au kama wanavyosema.

Video nimeiangalia yote. Najisemea moyoni tu. Naweza uwa mtu aisee.
 
Wakamatwe haraka ili hivi vitendo vikomesshwee
 
Back
Top Bottom