WATOTO WASIOZALIWA: Ujumbe wa Mawazo na Hisia

WATOTO WASIOZALIWA: Ujumbe wa Mawazo na Hisia

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
WATOTO WASIOZALIWA
1. LETTER TO MY UNBORN CHILD - 2 PAC
Pac anamwandikia barua mtoto wake ambaye bado yupo tumboni mwa mama yake na KUMWAMBIA UKWELI kuhusu dunia hii.
Mistari ambayo inanigusa zaidi humu ni hii ifuatayo;
"MY ONLY FRIEND IS MY MISERY." 00:48
(Rafiki yangu wa pekee ni mabalaa yangu)
" I GOT SHOT FIVE TIMES BUT I'M STILL BREATHING
THAT'S THE PROOF THERE IS GOD IF YOU NEED A REASON" 01:26-29
(Nilipigwa "shaba" mara tano lakini bado ninapumua. Huu ni uthibitisho wa kuwa MUNGU YUPO kama unahitaji sababu)
"IF THERE IS A GHETTO FOR TRUE THUGS, I'LL SEE YOU THERE." 02;30
(Kama kuna PEPO kwa ajili ya WAHUNI tutakutana huko. Pengine aliyevumisha neno la WAHUNI WOTE PEPONI alilitoa hapa wazo lake.

Mstari mwingine kwenye barua hii ya Pac kwa mwanaye, anasema; " I WONDER IF YOU'LL SUFFER FOR YOUR FATHER'S CRIME." (Bado ninajiuliza kama utapata shida kufidia uhalifu niliowahi kuutenda)

Bonge la concern ya mzazi kwa mtoto wake. Mstari huu unaongea na mimi binafsi kwa namna ya pekee sana.

Itafute ngoma hii kisha urudi tujadiliane.
Hii ni ngoma niliyoanza kuisikia.

2. MWANANGU - FID Q FT BANANA ZORRO
Hii ni ngoma ya pili kuisikia kwenye mfululizo wa ngoma zilizo kwenye andiko hili.

Wimbo huu unapatikana kwenye albamu ya kwanza ya Fid Q "Vina Mwanzo, Kati na Mwisho" na ilipikwa Bongo Records.

Fid anasema anajiwa ndotoni na mtoto wake ambaye bado yu tumboni mwa mama yake.

"MWANANGU ANASITA KUJA DUNIANI, DUNIA INAMTISHA" 01:59
"AKIENDA KWA NDUGU ZAKE HATOJISIKIA YUPO NYUMBANI
SABABU BABA YAKE NSHAFUKUZWA, KOSA NILISAHAU KUSUUZA SAHANI" 00:33

3. KIJUSI - NIKKI MBISHI
Kutoka kwenye albamu ya kwanza ya Nikki " Sauti ya Jogoo" wimbo huu unatupeleka moja kwa moja mpaka tumboni mwa mama na kumsikia kijusi anayewalalamikia wazazi wake kwa kutoa mimba yake na kufa kabla ya kuzaliwa.

"KUNA MUDA ULIFIKA, MAMA ULIKUWA MTORO
SHULENI ULIADIMIKA, NYUMBANI IKAWA MGOGORO
BABA ALIKUCHANGANYA KWA VITU ALIVYOKUPA
KILA ULIPOPATA MWANYA, GHETO KWAKE ULIIBUKA." 01:30-36
"MLINIUA MALAIKA KWA MASLAHI BINAFSI
KWA MUUMBA NIMESHAFIKA, NAISHI PASI NA WASI
MMENITOA BILA KUJUA NILIKUWA MTOTO WA PEKEE
MUNGU UZAZI KAUCHUKUA, KUZAA TENA MSITEGEMEE" 02:52-59

4. LOST ONES - J COLE
Baada ya ngoma hizo tatu za moto, nikaja kuisikia hii.
Humu Cole World KACHEZA nafasi mbili ya mwanaume na mwanamke kama alivyokuja kurudia kuucheza mchezo huu DIZASTA kwenye ngoma yake iitwayo MUSCULAR FEMINIST.

Cole kasimama kama "mvulana" asiye na mbele wala nyuma anayempa ujauzito mpenzi wake na kutaka wautoe sababu hana uwezo wa kuuhudumia wala wa kuja kumtunza mtoto.

Binti kamsikiliza na alipoona Cole kaweka kituo kaja kampaka sana. Kumbe Cole naye alitelekezwa na baba yake. Binti anahoji kama yeye alichukia kutelekezwa, yeye anachokifanya kina utofauti gani?
Cole anasema;

"THINK ABOUT IT BABY ME AND YOU WE STILL KIDS OURSELF
HOW WE GON RAISE A KID BY OURSELF?"
(Fikiria kuhusu hili, mpenzi wangu, wewe na mimi bado ni vijana wadogo
Tutamleaje mtoto peke yetu?)

"A NIGGA BARELY OVER 20, WHERE THE HELL WE GON LIVE?
WHERE AM I GON GET THAT MONEY?
( Kijana mdogo mwenye miaka yangu ishirini na... Tutaishi wapi? Hizo pesa za matumizi nitazipata wapi?

Huyo ni Cole, Sasa binti anamjibu kwa kusema;
"THIS MY BODY NIGGA SO DONT THINK
YOU FINNA FORCE SHIT"
(Huu ni mwili wangu, usidhani utanilazimisha kufanya kitu chochote)
"NOW I'M PREGNANT YOU DONT WANNA GET INVOLVED MOTHERF****
TRYNA TAKE AWAY A LIFE, IS YOU GOD MOTHERF***?"
(Sasa nina ujauzito na hutaki kujihusisha nao km*****
Unataka utoe uhai wa kiumbe, kwani we ni Mungu, km***? )
"I'LL DO THIS BY MY MOTHERF*** SELF
SEE MY MOTHER RAISED ME WITHOUT NO MOTHERF*** HELP FROM A MAN
(Nitakitunza kiumbe hiki peke yangu
Hata mama yangu alinilea pasipo msaada wowote kutoka kwa mwanaume - mzazi mwenzake)

Tafuta goma hili halafu usikilize taratibu, ukiipata na video yake inanoga zaidi.

5. UKIZALIWA - STAMINA FT BANANA ZORRO
This is the latest release among all in the list. Banana anajitokeza tena kwenye orodha hii na chorus yake ya pili.

Bwana Bonventure anakiri kuwa alipoambiwa na mwenza wake kuwa ana ujauzito, alimtaka amtoe lakini mwenza wake akakataa.

Stamina kaongea mengi yaliyosemwa na wengine kwenye ngoma zilizopita ila yeye kaongeza vitu vipya; Hana uhakika na jinsia ya mwanaye lakini anasema yeyote sawa, njiti sawa, mlemavu sawa, Kubwa Sana hii!! Expectations kill!!

Banana Sasa anavyopenda sifa! Truth be told! Naupenda wimbo huu kutokana na vocals na lyrics kali za Banana, Stamina kaongea mengi yaleyale yaliyotawala kwenye tungo zao za siku hizi.

Banana anasema:
" SIKU UKIZALIWA NITARUDIA
TENA KWA SAUTI NA UTASIKIA
SITAKI KUKUONYA KUHUSU DUNIA
SABABU DUNIA IPO NA UTASHUHUDIA
NAJUA HUSIKII NINAVYOKUAMBIA
ILA UKIZALIWA NITARUDIA
UKIZALIWAAAAAAAAAAAA
UKIZALIWAAAAAAAAAAAA
MWANANGUUUUUUUU."
Mwandishi wa aina yake,
LUAH.
1683802702331.jpeg

May be an image of 1 person

1683802760129.jpeg

May be a black-and-white image of 1 person
 
Back
Top Bottom