BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani na Damu kwa Watoto kutoka Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Dkt. Heronima Kashaigil amesema kuwa watoto 5 hadi 7 wanahudhuria Kliniki ya matibabu ya Saratani kila siku, sawa na watoto 250 kwa mwezi.
Utafiti uliofanywa na Shirika la ICCARE Tanzania ulibaini wagonjwa wengi waliokuwa wanafika Bugando kupata matibabu ya Saratani walikuwa wanaishia kwenye dozi ya kwanza kutokana na gharama za kusubiria matibabu kuwa juu ambapo wengi wao hukatisha matibabu na kufariki.
Kutokana na hali hiyo Hospitali ya Bugando imewataka wazazi na walezi kuwapeleka watoto Hospitalini kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya Saratani ili waanze matibabu mapema.