Mtoa Taarifa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2024
- 213
- 671
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
================
Watu 14 wamefariki Dunia na wengine 9 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha gari ya abiria aina ya Toyota Hiace yenye namba T562 DGG ambalo imeligonga Mistubishi Fuso T361 CSB kwa nyuma Wilayani Nzega, leo Novemba 7, 2024.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao amesema Dereva wa Toyota bado hajafahamika kwa kuwa alikimbia baada ya tukio hilo na chanzo cha ajali imebainika ni uzembe wa dereva wa Hiace alipokuwa akijaribu kulipita Lori na kuligonga kwa nyuma.
Waliofariki Wanaume ni 8, Wanawake 4 na Watoto wenye umri chini ya umri wa mwaka mmoja (wawili).