Watu 14 wafariki dunia kwenye ajali ya Lori na Hiace mkoani Tabora

Watu 14 wafariki dunia kwenye ajali ya Lori na Hiace mkoani Tabora

Na hapo wengi watakuwa wanaume.
Wanaume tunaisha wajameni.
RIP kwako...
Dereva mzembe sana anauwa watu kindezi sana.
Kwa Tanzania, chukulia kila dereva hasa wa magari ya abiria kuwa ni mvuta bangi na hajui sheria. Hivyo ukiwa abiria inatakiwa muwe wakali kweli kweli mnapoona anafanya ujinga hasa wa mwendo mkali.
 
Waziri wa Mambo ya Ndani yukwapi? Unapoteza rais wajenga uchumi kila siku.

Ajali limekuwa janga la taifa sasa hivi. Tume iundwe ichunguze vyanzo vikubwa vya ajali ni nini. Haiwezekani kila siku watu wafe kwa makumi na polisi wa usalama barabarani mpo.

RAIS na mawaziri husika fanyeni kazi yenu
 
Mwenyezi Mungu atusaidie kwa kweli
Zamani nlikuwa na tabia,wakati napiga masanga kwenye bar zile
Wanazoweka viti mpaka karibu na barabara ,nlikuwa nakaa
Kuna siku nlikuwa kwenye bar fulani barabara ya mwinjuma Road...ilikuwa saa tano usiku
Pona yangu nlienda toilet,
Kuna mlevi alikuwa anapita akaacha njia wee 😄 waliyokuwepo walipatapata

Ova
 
Hi ni breaking news nimeiona pale Mwananchi kwamba watu 14 wamepoteza maisha baada ya gari la abiria dogo la aina ya Toyota Hiace kugonga lori kwa nyuma wilayani Nzega, mkoani Tabora, hii leo, Alhamisi, Novemba 7, 2024.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Richard Abwao, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

So far updates zaidi zinasubiriwa.

Source: Mwananchi
Umaskini mbaya sana, hiace inabeba watu 14, ambao wamefariki, na bado hapo uawezakuta kuna majeruhi kadhaa,

Eee Mungu wape pumziko la amani Watanzania wenzetu, nao pia walitamani waione jioni ya Leo,
 
Kuna wajinga hapa watakupinga. Ukweli uko sahihi kabisa. Hapa inaonyesha hiyo hiace ilikuwa kwenye mwendo mkali sana na abiria wakawa wanafurahia tu.
Takwimu nyingi za ajali hasa Tanzania zinatokana na mwendokasi wa dereva na uzembe.

Haya yote yanatokana na watu kuchukulia sheria za barabarani simple simple tu.

Kwa nchi za wenzetu kutii sheria za barabarani ni lazima hata usiku. Mfano kusimama kwenye zebra ni amri hata kama hakuna mtu anataka kuvuka, unapaswa kusimama hadi taa ya kijani iwake.

Ila kwa Afrika hasa Tanzania watu wanajiendea tu Vululu-valala.
 
Zamani nlikuwa na tabia,wakati napiga masanga kwenye bar zile
Wanazoweka viti mpaka karibu na barabara ,nlikuwa nakaa
Kuna siku nlikuwa kwenye bar fulani barabara ya mwinjuma Road...ilikuwa saa tano usiku
Pona yangu nlienda toilet,
Kuna mlevi alikuwa anapita akaacha njia wee 😄 waliyokuwepo walipatapata

Ova
Umeona mkuu,yaan kifo kinakukuta popote...
Tupo nyakati mbaya sana aisee
 
Leo imetokea ajali ya Hiace na Lori nakuua watu 14 papo hapo wakiwemo watoto wawili, wilayani Nzega mkoa wa Tabora . Kamanda wa Polisi Tabora amethibitisha.

==========================

Snapinsta.app_465938949_2259959024376387_6933617933271610871_n_1080 (1).jpg
Watu 14 wamefariki dunia baada ya gari ya abiria dogo aina ya Toyota Hiace kuligonga lori kwa nyuma wilayani Nzega mkoani Tabora leo Alhamisi Novemba 7, 2024.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
 
Kama hamas, Israel,palestina,urusi, Congo...
Mi nadhani kufa ni kufa tu
Ni nyakati zenyewe hizi...hakuna wa kupona!
Kufa si kufa tu.

Life expectancy za nchi za wenzetu haziji kwa kauli za namna hii kwamba eti, kufa ni kufa tu.

Wenzetu wapo very strictly na very seriously kuhusu kulinda uhai wa Raia wao kwanzia kwenye usafiri na Afya.

Sheria ni kali kwenye sekta nzima ya usafiri na lazima zifuatwe.

Huku Afrika ni kuchekeana tu na kuhongana barabarani.

Halafu mijitu ikishakufa inaanza kusema ni mipango ya Mungu.

Na watazidi kufa sana.
 
Back
Top Bottom