Watu 14 wafariki dunia kwenye ajali ya Lori na Hiace mkoani Tabora

Watu 14 wafariki dunia kwenye ajali ya Lori na Hiace mkoani Tabora

Aisee pole kwa Wafiwa inaumiza kusikia watu wamekufa kwa ajali ya mwendokasi uliosababishwa na dereva mzembe...
Na pia Serikali punguzeni kodi za gari za abiria kupunguza ajali hivyo vi hiace ni vile mmevizoea hakuna brake humo kwa safari za masafa marefu..
Tanzania kuingiza Sprinter Benz ya 2018 kodi Tsh 45 million abiria 22 tu..na ninyi mnalalamika ajali wakati mazingira ya wasafiri yapo kimashaka sana..
Quantum luxury sijui itakua ngapi mna balaa sana...
 
Majeruhi wote Mungu awaponye, Marehemu wote wapumzike kwa Amani.
 
Waafrika wengi wanakufa kutokana na ujinga na upumbavu wao.
Nani mwerevu ambaye hata kufa?.Sababu za kufo ndio zakibinadamu ila kifo nijambo ambalo hakuna kiumbe mwenye uwezo wakulikimbia awe mjinga au mwerevu tajiri kwa maskini kifo kiko pale pale.Siku yako ikifika lazima kuwe na sababu yakukufanya uondoke ata kama nisababu ya kijinga.
 
Nani mwerevu ambaye hata kufa?.Sababu za kufo ndio zakibinadamu ila kifo nijambo ambalo hakuna kiumbe mwenye uwezo wakulikimbia awe mjinga au mwerevu tajiri kwa maskini kifo kiko pale pale.Siku yako ikifika lazima kuwe na sababu yakukufanya uondoke ata kama nisababu ya kijinga.
Life expectancy unaelewa ni nini?

Na ni kwanini nchi za Afrika zina life expectancy ndogo kulinganisha na nchi za wazungu?
 
Watu 14 wamefariki dunia baada ya gari ya abiria dogo aina ya Toyota Hiace kuligonga lori kwa nyuma wilayani Nzega mkoani Tabora leo Alhamisi Novemba 7, 2024.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.


================

Watu 14 wamefariki Dunia na wengine 9 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha gari ya abiria aina ya Toyota Hiace yenye namba T562 DGG ambalo imeligonga Mistubishi Fuso T361 CSB kwa nyuma Wilayani Nzega, leo Novemba 7, 2024.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao amesema Dereva wa Toyota bado hajafahamika kwa kuwa alikimbia baada ya tukio hilo na chanzo cha ajali imebainika ni uzembe wa dereva wa Hiace alipokuwa akijaribu kulipita Lori na kuligonga kwa nyuma.

Waliofariki Wanaume ni 8, Wanawake 4 na Watoto wenye umri chini ya umri wa mwaka mmoja (wawili).
Gari ya kubeba watu 16 inabeba watu 24 kama coaster huku police wakifumbia macho hiyo tabia
 
Back
Top Bottom