Watu 14 wafariki dunia kwenye ajali ya Lori na Hiace mkoani Tabora

Watu 14 wafariki dunia kwenye ajali ya Lori na Hiace mkoani Tabora

R.i.P Classmates.....😥
Wameondoka wakiwa ma umri mdogo sana aisee...
 
Fafanua.
Maana humo ndani wengine hawana hatia.
Kifo kikikupigia ni ONE CALL 🤙
R.I.P JPM
Kwa nini ukubali kuendeshwa mwendo wa kasi na uridhike tu?

Kwa nini ukubali kuendeshwa na dereva mpumbavu asiyejali uhai wako na wakwake?

Halafu upo comfortable tu, useme kwamba huna hatia?

Utakufa vibaya wewe!!

Ndipo uelewe hata wewe una hatia.
 
Kufa si kufa tu.

Life expectancy za nchi za wenzetu haziji kwa kauli za namna hii kwamba eti, kufa ni kufa tu.

Wenzetu wapo very strictly na very seriously kuhusu kulinda uhai wa Raia wao kwanzia kwenye usafiri na Afya.

Sheria ni kali kwenye sekta nzima ya usafiri na lazima zifuatwe.

Huku Afrika ni kuchekeana tu na kuhongana barabarani.

Halafu mijitu ikishakufa inaanza kusema ni mipango ya Mungu.

Na watazidi kufa sana.
Sahihi, Utamaduni wa Kiswahili wa kuishi kwa kutegemea "kudra" tu ni wa hovyo sana na unafifisha uwajibikaji.
 
Kwa nini ukubali kuendeshwa mwendo wa kasi na uridhike tu?

Kwa nini ukubali kuendeshwa na dereva mpumbavu asiyejali uhai wako na wakwake?

Halafu upo comfortable tu, useme kwamba huna hatia?

Utakufa vibaya wewe!!

Ndipo uelewe hata wewe una hatia.
Nimekuelewa mkuu Mimi huwa sinyamazi ikiwezekana nipewe/ rudishiwa nauli yangu nikapande gar lingine
 
Sahihi, Utamaduni wa Kiswahili wa kuishi kwa kutegemea "kudra" tu ni wa hovyo sana na unafifisha uwajibikaji.
Juzi juzi tu hapa, Kuna clip moja niliona na ilitrend sana kwenye social media,

Kuna Boti moja huko DRC Congo ilikuwa imebeba watu wengi sana, Yaani nyomi, Halafu hawaku vaa hata life jackets.

Boti ikaanza kuzama, wakawa wanasali na kupayuka, Oh Yesuuu! Yesuuuu eeeeeh! Tuokoe.

Walizama na kuishia wote kwenye maji wakafa.

Waafrika wengi wanakufa kwa ujinga na uzembe wao.
 
Watu wanafunga mwaka kwenye viringe vyao huko
 
Hiace inabeba abiria wangapi kwani?

Hii ni uroho wa fedha kuhatarisha maisha ya watu.
 
View attachment 3146171
Watu 14 wamefariki dunia baada ya gari ya abiria dogo aina ya Toyota Hiace kuligonga lori kwa nyuma wilayani Nzega mkoani Tabora leo Alhamisi Novemba 7, 2024.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

================

Watu 14 wamefariki Dunia na wengine 9 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha gari ya abiria aina ya Toyota Hiace yenye namba T562 DGG ambalo imeligonga Mistubishi Fuso T361 CSB kwa nyuma Wilayani Nzega, leo Novemba 7, 2024.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao amesema Dereva wa Toyota bado hajafahamika kwa kuwa alikimbia baada ya tukio hilo na chanzo cha ajali imebainika ni uzembe wa dereva wa Hiace alipokuwa akijaribu kulipita Lori na kuligonga kwa nyuma.

Waliofariki Wanaume ni 8, Wanawake 4 na Watoto wenye umri chini ya umri wa mwaka mmoja (wawili).
Duuh RIP
 
Wapumzike kwa aman 🙏🙏
 
Mbona kila ajali yenye vifo dereva huwa anakimbia? Kwani madereva wao huwa hawafi?
 
Back
Top Bottom