Watu 20 wahofiwa kufariki baada ya basi walilokuwa wakisafiria kugongana na lori mjini Nzega, leo Oktoba 21, 2023

Sema Polisi wa barabarani hawana msaada tofauti na kula rushwa.

Kila siku ajali zinaongezeka badala ya kupungua.

Ajili nyingi zinahusisha Bus na Lory mara nyingi, hii ni ishara kuwa tuna madereva wasiozingatia usalama barabarani wanaoendesha magari makubwa.
 
We jamaa taarifa zako ni ajali tu.
 
Dah poleni Sana wafiwa
 
Ajali ikishakuwa kwa magari kugongana uso kwa uso, mara nyingi chanzo huwa ni ama uzembe wa dereva wa gari moja au hitilafu ya chombo kimoja...

Haya yote tunaweza kuyaepuka kama tungekuwa tunajenga barabara zetu kwa kutenganisha njia za kwenda na kurudi walau basi hata kwa vipande ambavyo ni maarufu kwa ajali...

Mfano wa highways za US kama hii I-35, ambapo unaona magari ya kila uelekeo yapo upande wake...

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…