GE2025 Watu 29 wafikishwa Mahakamani kwa kesi ya uhaini Mara, Jumla yafikia 320 nchi nzima

GE2025 Watu 29 wafikishwa Mahakamani kwa kesi ya uhaini Mara, Jumla yafikia 320 nchi nzima

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
557
Reaction score
1,039
Maumivu yanazidi kuendelee! Hivi hii serikali itawakamata wangapi?

Kudai haki Tanzania sasa imegeuka kosa la Uhaini. Ipo siku ya ukombozi inakuja tu
=============
Watu 29 wakiwemo wanachama wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamefikishwa Mahakama ya wilaya ya Bunda mkoa wa Mara wakikabiliwa na mashitaka mawili ambayo ni kula njama ya kutenda jinai, na uhaini.

Hati ya mashitaka inaeleza kuwa kati ya Machi na Oktoba 30, 2025, watuhumiwa walidaiwa kupanga njama za kuzuia uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, kutishia uongozi wa nchi, na kusababisha uharibifu wa mali za serikali wilayani Bunda.

Watuhumiwa hawakuruhusiwa kujibu chochote baada ya mashitaka kusomwa, kwa sababu Mahakama haikuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi ya aina hiyo. Upande wa utetezi chini ya Wakili Alex Massaba, uliwasilisha maombi ya kuhakikisha watuhumiwa walioumia wanapatiwa matibabu stahiki na kulinda haki za watuhumiwa wawili walio chini ya miaka 18. Mahakama ilikubali maombi hayo.

Akizungumza na Jambo TV, Wakili Massaba amesema kuwa kuandamana au kukusanyika kwa amani hakuwezi kuainishwa kama uhaini. Ameongeza kuwa mashitaka yanayodaiwa tarehe 30 Oktoba hayana msingi kwa kuwa siku hiyo hakukuwa na uchaguzi.

Soma Pia: Jamhuri yaongeza wengine 47 kwenye kesi ya Uhaini baada ya Maandamano Oktoba 29, idadi yafikia watu 145

Amesisitiza kuwa ni muhimu Mahakama ziwe huru katika kubaini aina na uzito wa makosa ili haki itendeke kwa mujibu wa sheria.

Kesi imeahirishwa hadi tarehe 24 Novemba 2025 kwa ajili ya kutajwa tena.
 
"...mlikuwa na Simba wa Yuda hapa.."😁
 
Dhambi ya mauaji ya kikatili ya namna ile itawatafuna sana makatili wote.Kuanzia viongozi,watekelezaji hata wakaa kimya waliokiwa na uwezo wa kuzuia unyama ule.

Eee Mungu shusha mapigo makali kwao.
 
If the court will get rid of the image that portrays it as a "Kangaroo Court" then surely the accused persons will be definitely acquitted.
 
Kuna time inafika unashindwa u comment nini!

Anyway 9dec tukutane.
 
Back
Top Bottom