Watu 4 wanaotuhumiwa ‘kutumwa na afande’ kumlawiti na kumbaka binti mkazi wa Yombo Dovya Mkoani Dar, Wafikishwa Mahakamani

Walipaswa kuonyeshwa sura zao zionekane live jamii iwaone hao binadamu wajinga na wapumbavu.

Siku zote wanazopelekwa mahakamani sura zao zionyeshwe kwenye vyombo vya habari.

Serikali iwakamate haraka watuhumiwa wengine akiwepo mmoja ambaye hayupo hapo na bosi wao aliyewatuma
 

Asante sana japo sehemu nyingine imekuwa tafsiri sisisi.
 
kuna madai kuwa mwanamke huyo alikuwa anajiuza, yaani kazi yake ni ukahaba.
kama ni hivyo basi hapo hamna kesi.
labda washitakiwe kwa kosa la kusambaza picha za ngono.
 
Tunamtaka aliewatuma hao vibaka
 


Kesi hazifanani. Kila kesi huamuliwa kulingana na muktadha wake.

Kesi ya RC na ya Binti wa Yombo zina utofauti, na hivyo maamuzi yake hayawezi kufanana na wala huwezi kuchukua uamuzi wa kesi hizi mbili kama kitu kimoja.

Kwanza kesi moja ni ulawiti pekee wakati nyingine ni ubakaji wa kundi (gang rape na ulawiti).

Halafu kuwa na ushahidi ni jambo moja, na kuuthibitisha* ushahidi ni jambo lingine.
 

Nazungumzia video kama ndiyo hoja ya kuwatia hatiani ,hizo kesi ni tofauti kabisa...video ni supporting evidence tu ,kesi nyingi za waliofungwa miaka thalatha za ubakaji hazina video so hoja ya kuthibitisha kwenye video siyo ya msingi sana maana kuna watu wamefungwa kwa kesi za ubakaji na wala kulikuwa hakuna video clip.
 

Hoja ya uthibitisho wa video ni ya msingi kwa sababu maelezo ya historia ya kesi, ushahidi muhimu ni wa video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…