Watu 4 wanaotuhumiwa ‘kutumwa na afande’ kumlawiti na kumbaka binti mkazi wa Yombo Dovya Mkoani Dar, Wafikishwa Mahakamani

Watu 4 wanaotuhumiwa ‘kutumwa na afande’ kumlawiti na kumbaka binti mkazi wa Yombo Dovya Mkoani Dar, Wafikishwa Mahakamani

Watu wanajua kuzusha sana bongo, walikuwa wanasema ni wanajeshi Sasa hao ni.wanajeshi wa wapi? Au huyo mmoja kuvaa likitambaa lenye rangi zinazofanana na Jeshi?Wahalifu huita mara nyingi KIONGOZI wao Kamanda, afande, hivyo kutaka neno afande haimaanishi ni afande kweli. Wapate adhabu Kali ili iwe fundisho kwa wengine maana kwa ujinga walioufanya tayari umeleta madhara kwa wasiohusika na kwa Taifa kwa ujumla
Siku nyingine uwe unasoma Uzi mpaka mwisho au ujifunze kuuliza usikimbilie ku comment tu ona sasa unavyojitia aibu.
 
Wakatoliki hutumia neno hilo wakimaanisha MTAKATIFU. Hivyo mwalifu anaweza kujificha kwa kujiita mtakatifu kumbe ni firauni. Ingekuwa inamaana yoyote ya jeshi lolote wangetaja na cheo chao
Samahani mkuu hii comment umeandika ukiwa bar Gani? Kama ya mataputapu ondoka upesi maana unapoelekea utaanza kusaula viwalo vyote uwape watu faida
 
Ili ithibitike kwamba kulikuwa na ubakaji na ulawiti, ni lazima ithibitishwe kwamba watuhumiwa walimuingilia bila ridhaa yake Binti.

Ili kuthibitisha kwamba watuhumiwa ndiyo walimuingilia ni lazima ripoti ya daktari iseme kwamba kwenye sehemu za Siri za Binti kulikuwa na majimaji ya watuhumiwa.

Sasa changamoto hapa ni ukosefu wa hayo majimaji. Sidhani kama alipimwa kabla hajaoga. Hapa kimsingi hakuna uthibitisho wa kuingiliwa.

Tuje kwenye ushahidi wa video.

Kanuni za ushahidi wa video zinamtaka Shahid athibitishe kwanza kwamba vifaa vilivyorekodi vilikuwa vinafanya kazi Kwa ufasaha kabla ya kurekodi, na uthibitisho unatakiwa uwe wa mtaalamu aliyebobea kisimi katika fani ya electronic. Lengo la kanuni hii ni kuepuka uwezekano kwamba video imeyengenezwa na siyo halisi.

Pia kama video zimehamishwa kutoka kwenye simu, CCTV na kuwekwa kwenye flash, ni lazima ithibitishwe kwamba kuhamisha huko hakukuathiri ushahidi. Hili linaenda sambamba na kuthibitisha kwamba hiyo flash ilikuwa salama yaani haina virus au mechanical damage iliyopunguza ubora wa ushahidi.

Basi nenda ukawe wakili wao. Naona utashinda kesi hii kirahisi sana learned brother
 
Mkuu Mtaalamu aliyebobea kisimi katika fani ya electronics. Una maana gani?
 
Watu wanajua kuzusha sana bongo, walikuwa wanasema ni wanajeshi Sasa hao ni.wanajeshi wa wapi? Au huyo mmoja kuvaa likitambaa lenye rangi zinazofanana na Jeshi?Wahalifu huita mara nyingi KIONGOZI wao Kamanda, afande, hivyo kutaka neno afande haimaanishi ni afande kweli. Wapate adhabu Kali ili iwe fundisho kwa wengine maana kwa ujinga walioufanya tayari umeleta madhara kwa wasiohusika na kwa Taifa kwa ujumla

1. MT. 140105 Clinton Honest Damas maarufu Nyundo - JWTZ
2.C.1693 Praygod Edwin Mushi - Jeshi la Magereza
3. Amin Lord Lema - Anon
4.Nickson Idala Jackson - Anon
5.ASP - Afande
 
Watu wanne wanaotuhumiwa ‘kutumwa na afande’ kumlawiti na kumbaka binti mkazi wa Yombo Dovya, jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Agosti 19, 2024 wamefiksihwa mahakamani na kusomewa mashktaka mawili.

Watuhumiwa hao wamefikishwa katika Mahakama ya Kanda Dodoma na kusomewa mashtaka ya kubaka kwa kikundi (gang rape) na kumwingilia kinyume na maumbile binti ambaye hakutajwa jina lake mahakamani.

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania mkoani Dodoma, Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Mashtaka Makao Makuu, Renatus Mkude amesema vijana hao wamekana mashtaka hayo na kutokana na unyeti wa shauri hilo wataendelea kuwa mahabusu.

Watuhumiwa hao waliofikishwa mahakamani ni MT. 140105 Clinton Honest Damas maarufu Nyundo, Amin Lord Lema, Nickson Idala Jackson na C.1693 Playgod Edwin Mushi

Kwa mujibu wa taarifa ya Renatus Mkude, Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Taifa ya Mashtaka amesema kesi hiyo itasikilizwa kwa siku tano kuanzia leo Agosti 19 hadi Agosti 23 siku ya Ijumaa.

Pia soma:

1. Polisi yaanza kufuatilia tukio la Binti aliyebakwa na wanaume watatu

2. Watuhumiwa wa mande ya Ubakaji na ulawiti waliotumwa na afande wakamatwa
Aisee! Wote ni wagalatia/makafiri?
 
1. MT. 140105 Clinton Honest Damas maarufu Nyundo - JWTZ
2.C.1693 Praygod Edwin Mushi - Jeshi la Magereza
3. Amin Lord Lema - Anon
4.Nickson Idala Jackson - Anon
5.ASP - Afande
Daah jamaa anaitwa Praygod wakati mwingine kumpa mtoto jina zuri hakusadiki matendo yake kabisa Bora hata angemwita Mende tu.
 
Hii ndo maana halisi ya nguvu ya umma. Kesi tayari imekula kichwa ya RPC. Wahusika lazima wapigwe mvua ili jeshi la polisi lijisafishe.
 
Wahusika wa hili sakata hata kama wakichomoka na hukumu watakuwa wamenyooka na kuwa na staha katika maisha yao.
Dunia imewafunza vya kutosha.
 
Back
Top Bottom