Watu 8,476 kusaka nafasi 42 za ajira zilizotangazwa na Bunge

Watu 8,476 kusaka nafasi 42 za ajira zilizotangazwa na Bunge

Tatizo la Tanzania haijulikani unemployment rate ni kiasi gani.

Ilitakiwa Waziri wa Fedha awe anatoa takwimu kila baada ya miezi 3 ili ijulikane wangapi wameajiriwa, wangapi wameachishwa kazi
Wangapi hawajaajiriwa japo wana vigezo
Biashara ngapi mpya zimefunguliwa
Biashara ngapi zimefungwa
 
Dodoma. Tume ya Utumishi ya Bunge imetangaza ajira za kada mbalimbali ambapo walioitwa kwenye usaili wako zaidi ya 8,000 kati ya nafasi za kazi 42 zilizotangazwa, huku kada zinazoongoza kwa idadi kubwa ni uchumi, udereva, sheria na uhasibu.

Kwa mujibu wa tangazo la kuitwa kwenye usaili lililotolewa Mei 19, mwaka huu na Katibu wa Bunge jijini Dodoma, liliorodhesha jumla ya majina 8,476 ya waliovuka hatua va kwanza ya mchujo na kuitwa kwenye usaili kwa kada 21 za ajira kwenye Bunge la Muungano wa Tanzania.

April 21, mwaka huu Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilitangaza nafasi za kazi 42 katika kada 21 mbalimbali ili kuim arisha utendaji wake.

Juzi, Bunge lilitoa tangazo lililosomeka: "Katibu wa Bunge, kwa niaba ya Sekretarieti ya Bunge anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia Mei 27, 2023 hadi Juni 03, 2023 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo."

Kwa mujibu wa tangazo hilo, kada zinazoongoza kwa waombaji wengi ni uchumi, sheria, udereva na uhasibu, huku kada zenye waombaji walio chini ya 100 ni afya na maktaba.

Tangazo hilo liliainisha kada hizo na idadi ya walioteuliwa kwenye usaili ikiwa kwenye mabano, ofisa hesabu daraja la II (538), msaidizi wa kumbukumbu daraja la II (279), udereva daraja la I (984), mhandi-si umeme daraja la II (234), ofisa usimamizi wa fedha daraja la II (492), mwandishi wa taarifa rasmi za Bunge darala la II (413), mchumi daraja la II (904), ofisa sheria dara-ja la I (302).

Nyingine ni ofisa Tehama daraja la II (310), msaidizi wa maktaba daraja la II (98), katibu msaidizi wa Bunge daraja la II Sheria (831), katibu msaidizi wa Bunge daraja la II uchumi (1,208), katibu msaidizi wa Bunge daraja la II (afya ya jamii/menejimenti ya huduma za afya) 47
 
Hizi ajira za kuingia asubui kutoka 12 kwa mshahara wa 250K wengi ndio wanazo hizo[emoji34][emoji34]
HALAFU HAZINA MKATABA NSSF WALA KINGA YOYOTE, SIKU BOSI AKICHAFUKWA TU UNARUDI NYUMBANI NA HAKUNA MAFAO NA NDIO MAANA WATU WENGI WANAKIMBILIA KUOMBA AJIRA ZA SEREKALI KILA ZINAPOTANGAZWA.
 
INGEKUA INAFAA KILA BAADA YA MUDA FLANI KUFANYWE MZUNGUKO WA BAADHI YA WAAJIRIWA WA SEREKALI WAPUNZISHWE KISHA WAAJIRIWE WENGINE NAO WALE MEMA YA NCHI KISHA BAADA YA MUDA TENA WAPUNZISHWE WAWEKWE WENGINE.
HII INGESAIDIA KUHESHIMIANA KIDOGO MAANA KUNA WAAJIRIWA WA SEREKALI WANAJISAHAU SANA NA WANAJUA HAKUNA WA KUWAGUSA NA WATAIFAIDI NCHI HII MPAKA MWISHO WAO NA BAADA YA WAO WATARITHI WATOTO WAO.
 
JamiiForums790734876.jpg
 
Back
Top Bottom