Watu 8,476 kusaka nafasi 42 za ajira zilizotangazwa na Bunge

Watu 8,476 kusaka nafasi 42 za ajira zilizotangazwa na Bunge

Ila serikali nayo ni kama haina akili! Sasa kwa nini uite wote hao wakati nafasi ni chache? Kwa nini usiweke vigezo vya kuwachuja kabla ya kuwatia kwenye interview? Kwa mfano unaanza na walio na ajira unawatema kwanza, then unaangalia sasa sifa ili mradi kwa nafasi 42 uite angalau 420, kwa maana kila nafasi ishindaniwe na watu 10!
 
kuna jamaa yangu ameitwa kwenye kada ya udereva…nikamwambia ya Mungu mengi ila usichome nauli..
Bora atengeneze connection bandarini awe anasukuma IT au awe wa daladala
 
Dodoma. Tume ya Utumishi ya Bunge imetangaza ajira za kada mbalimbali ambapo walioitwa kwenye usaili wako zaidi ya 8,000 kati ya nafasi za kazi 42 zilizotangazwa, huku kada zinazoongoza kwa idadi kubwa ni uchumi, udereva, sheria na uhasibu.

Kwa mujibu wa tangazo la kuitwa kwenye usaili lililotolewa Mei 19, mwaka huu na Katibu wa Bunge jijini Dodoma, liliorodhesha jumla ya majina 8,476 ya waliovuka hatua ya kwanza ya mchujo na kuitwa kwenye usaili kwa kada 21 za ajira kwenye Bunge la Muungano wa Tanzania.

Aprili 21, mwaka huu Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilitangaza nafasi za kazi 42 katika kada 21 mbalimbali ili kuimarisha utendaji wake.


Juzi, Bunge lilitoa tangazo lililosomeka: “Katibu wa Bunge, kwa niaba ya Sekretarieti ya Bunge anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia Mei 27, 2023 hadi Juni 03, 2023 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.”

Kwa mujibu wa tangazo hilo, kada zinazoongoza kwa waombaji wengi ni uchumi, sheria, udereva na uhasibu, huku kada zenye waombaji walio chini ya 100 ni afya na maktaba.

Tangazo hilo liliainisha kada hizo na idadi ya walioteuliwa kwenye usaili ikiwa kwenye mabano, ofisa hesabu daraja la II (538), msaidizi wa kumbukumbu daraja la II (279), udereva daraja la II (984), mhandisi umeme daraja la II (234), ofisa usimamizi wa fedha daraja la II (492), mwandishi wa taarifa rasmi za Bunge darala la II (413), mchumi daraja la II (904), ofisa sheria daraja la II (302).

Nyingine ni ofisa Tehama daraja la II (310), msaidizi wa maktaba daraja la II (98), katibu msaidizi wa Bunge daraja la II Sheria (831), katibu msaidizi wa Bunge daraja la II uchumi (1,208), katibu msaidizi wa Bunge daraja la II (afya ya jamii/menejimenti ya huduma za afya) 47.
 
Back
Top Bottom