Watu maarufu duniani waliofariki kabla ya kufikisha miaka 50

ni kweli mkuu royal family kwa kiasi kikubwa inahusika ktk kifo cha diana

Alikuwa ni people's princes hata umauti ulipomfika nilikuwa huko na jeneza lake nililishuhudia nilishtuka sana kwani alikuwa hana majivuno alikuwa anakuja na watoto wake bado wakiwa wadogo Mac Donald ya Kensington karibu na kwao, tatizo ni Prince nae akaamua kutembea na watu kadhaa kama major Hewitt aliekuwa anamfundisha kupanda farasi na Dr mmoja mpakistan na tajiri moja la mafuta mmarekani baada ya hapo ndipo akawa na Dodi mtoto wa bosi wa Fulham na aliekuwa mmiliki wa duka kubwa duniani (Harrod's) ambapo sasa limeuzwa. Kabla alisema atatangaza karibuni kitu ambacho dunia itashangaa,ndipo wakammaliza na Dodi pia
 
Ayrton Senna (racing driver) jamaa aliwatesa sana madereva alikufa kwa ajali akiwa bado kijana. Steve McQueen (actor) mzuri sana, na muimbaji Peter Tosh - bado nawakumbuka sana hawa
 
Reactions: itv

daah inasikitisha sana
 




Thomas Sankara, Rais wa Burkinafaso, huyu aliuwawa mwaka 1987 akiwa na umri wa miaka 38. Mauji ya Thomas Sankara ambaye anatajwa kama Che Guivara wa Afrika yalipangwa na kutekelezwa na Colonel Blaise Compaure, Rais wa Burkinafaso aliye ondolewa madarakani miezi kadhaa iliyopita kwa mapinduzi ya kiraia.

Oda ya kumuua Sankara ilitoka kwa Serikali ya Ufaransa wakishirikiana na puppet wao mkubwa Afrika Magharbi, Felix Houphouet-Boigny, ambaye alikuwa Rais wa Ivory Coast wakati huo.

Charles Taylor ambaye alikuja kuwa Rais wa Liberia, anatajwa kama miongoni mwa watu waliotumiwa na Blaise Compaure kwenda kuwashambulia kwa Risasi , Sankara pamoja na wanajeshi kumi na mbili waliokuwa wanamlinda Ikulu.
 
Steve Biko muzee wa black consciousness movement. Rest in peace illustrious son of Africa.
 
Princess Diana alianza mahusiano na mtoto wa Bilionea Al-fayed aliitwa DODI. huyu Al-fayed ni Billionia wa London na ni mwarabu, Kilichowaudhi familia ya kifalme wa Uingereza ni pamoja na tetesi kwamba Diana tayari alikuwa na ujauzito wa huyo mwarabu, na ikumbukwe kama mtoto angezaliwa bado angekuwa na uhusiano na familiya ya kifalme, hivyo yakamkuta yaliyomkuta, Dereva wao aliekuwa anawaendesha siku hiyo bwana Henry alikuwa mahututi alitegemewa kuelezea masaibuya ajali ile lakini nae mauti ilimfika.Al-Fayed anamiliki timu ya soka huko Uingereza.
 
Mkuu sule ulimpima Manet kabla hajafaa???yy safari yake alishaimaliza kilichobaki ni ww kujiuliza safari yako utaimaliza namna gani,mwache marehem apumzike huko aliko sio vyema kumsema sema marehemu.
Nilisikia enzi hizo kuwa huyu mwanamuziki alikufa kwa kwa AIDS. Na nadhani wanamuziki wengi kipindi kile walicharangwa na AIDS. Mwana kufa ni kufa tu.
Kama kumbukumbu zangu ziko sawa, kulikua na mfululizo wa makala flani ktk gazeti moja la kiswahili ambalo mwanamama mmoja mjane wa Maneti alikua akitoa simulizi za mapambno yake na virusi vya HIV ambavyo amekua navyo tangu miaka 80, watz tuache unafiki na kufichaficha mambo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…