GT,
Mbona unapenda kupotosha ukweli, kama kusema kambona alipata post siku ya uhuru, wakati yeye alikuwa katibu wa tanu kabla ya uhuru.
Pili historia gani ya nchi hii inayoandikwa kwenye msikiti wa manyema huoni hiyo histori inaweza kuwa biased.
Tatu mbona Rashid Mfaume Kawawa aliachiwa uwaziri mkuu? Je, sio kutambua mchango wake au waislamu katika mchango wao wa kuleta uhuru wa nchi hii? Je, kupewa jina uwanja wa Sheikh Amri Abeid huko Arusha sio kutambua huo mchango wake?
Je, Sykes kuwa balozi mpaka alipostaafu sio kutambua mchango wake? Huyo Kitwana Kondo from 'taxi driver' mpaka kupata kile alicho nacho sio kutambua mchango wake, au ulitaka mpaka apewe uraisi wa nchi ndio utambue hilo? Au ulitaka baraza lote la mawaziri liwe la hapo msikiti wa Manyema ndio uone kwamba huo mchango wao umetambulika?
Na huyo Nyerere alijichagua mwenyewe? Si walimchagua wao wenyewe kwa kuuona busara au akili zake au kipaji au uwezo wake wa kuongoza?
Vugu vugu la ukombozi Tanzania lililetwa na watu wengi kwa njia tofauti, na si kwa dhana unayotaka kuileta, kuna Abdul Mtemvu alikuwa na TLP, na kuna wengine wengi, kutegemeana na huyo mtu yupo wapi, kama ni Kilimanjaro, Mwanza, Tabora, Dar es Salaam, Arusha, Kigoma, na kwa mtu mwenye akili ratio ya watu fulani inategemea upo wapi e.g Dsm - kwa wakati huo wakazi wake wengi walikuwa wanaishi hapo Livingstone, Shule ya Uhuru mpaka hiyo Magomeni Mikumi, na kwa sababu vugu vugu kubwa ilikuwa makao makuu ya serikali i.e Dsm, basi yanaweza kuonyesha, hiyo picha unayotaka wewe.
Lakini ukiwa unataka ukweli uchambuzi wako au mchango wako usijikite hapo Manyema, maana vyama vilivyokuwa na nguvu wakati huo vilikuwa vingi na ni watu wengi ndio waliotoa mchango wa nchii hii kupata uhuru. Ilikuwepo Nyanza Co-op Union na akina Bomani, KNCU na akina Marealle, na kuna watu wengine ambao hawakuwa upande wa Nyerere, ambao bahati mbaya historia haijawaandika au walielezwa tofauti kama ilivyokuwa kwa Abel Muzorewa Zimbabwe au kwa kuwa muda umepita saana vitu vingine hatuvikumbuki.
Au ulitaka nchi igawanyike kwenye kila kanda ili ujuwe michango ya watu wengine?
Kuna watu kama Chifu Lukumbuzia (kama jina nima andika vizuri), kuna Jaji Ruhumbika etc je hao wote walikuwa hawajui kuvaa Suruali mpaka wakaja kufundishwa kuvaa hizo suruali hapo Manyema? Au ndio akutukanae hakuchagulii tusi?