Marehemu Tewa Said alipata kueleza kwamba siku ile kabla ya uchaguzi pale Arnatouglo Hall, kwamba Abdulwahid alikwenda nyumbani kwake jioni. Wakati huo Tewa akikaa mtaa wa Pemba si mbali sana toka nyumbani kwa Abdulwahid. Abdulwahid alimwambia Tewa kuhusu mabadiliko ya uongozi ambayo waliamua yafanyike kwenye chama cha TAA...Bwana Tewa, kesho tunakwenda kumpa huyu mtu, Nyerere, mamlaka ya kuendesha nchi hii. Kuanzia hapo, mara tu tutakapomchagua kutuongoza hakuna namna ya kumnyang'anya mamlaka hayo. Hatumfahamu vizuri sana lakini natumaini kila kitu kitakwenda vizuri....
the rest is history....
Na mzee Tewa alikuwa anasema kuwa kitu pekee alichokuwa nacho Nyerere zaidi ya Abdulwahid kilikuwa ile digrii ya chuo kikuu....Ninaamini kama Abdulwahid angekwenda Makerere wazee wangeunda chama cha TANU mapema zaidi, labda kabla ya mwaka 1954 na Abdulwahid angekuwa rais, hata kama angeshindana na Nyerere....lakini historia ilichukua mrengo tofauti