Watu saba wamefariki dunia na wengine 75 wamejeruhiwa katika ajali mbili tofauti zilizotokea wilayani Same

Watu saba wamefariki dunia na wengine 75 wamejeruhiwa katika ajali mbili tofauti zilizotokea wilayani Same

Watu saba wamefariki dunia na wengine 75 wamejeruhiwa katika ajali mbili tofauti zilizotokea wilayani Same. Ajali ya kwanza ilitokea majira ya saa saba usiku wa kuamkia leo katika maeneo ya Njoro na kuhusisha basi la Kampuni ya Osaka lililokuwa likielekea Dar es Salaam, ambapo ilisababisha kifo cha mtu mmoja na wengine 52 walijeruhiwa.
IMG-20250330-WA0087-1536x1024.jpg

IMG-20250330-WA0078-1536x1024.jpg

IMG-20250330-WA0086-1536x1024.jpg
Ajali ya pili ilihusisha basi aina ya Costa la Kampuni ya Mkokota majira ya saa2 asubuhiya leo, ambalo lilipinduka katika kona za milima ya Ilamba, na kusababisha vifo vya watu sita na majeruhi 23. Waliofariki dunia katika ajali hiyo ni wanakwaya waliokuwa wakisafiri kutoka Chome kuelekea Ndolwa.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Same, Dkt. Alex Alexander, amesema kuwa majeruhi wa ajali ya kwanza walipokelewa hospitalini majira ya saa nane usiku, huku majeruhi wengine 23 pamoja na miili ya marehemu sita ikifikishwa hospitalini mchana wa leo Machi 30, 2025.

Baadhi ya majeruhi wa ajali iliyotokea usiku wameeleza kuwa ajali hiyo ilisababishwa na mwendokasi, hali iliyomfanya dereva kushindwa kulimudu gari. Chanzo cha ajali ya pili chanzo chake kikielezwa kuwa ni kukatika kwa stering road.

Chanzo: Full Shangwe
 
Maeneo Yale Kuna upepo kweli, usipokuwa makini unapotea...Sema Kuna gari za kupanda aisee, mambo ya Mungu atatuokoa wakati gari yenyewe mbovu hakuna hiyo.
 
Pole Kwa majeruhi na waliofariki Mungu azilaze roho zao mahali pema peponi, ingekuwa ni mkutano wa Lissu wangefika Kwa wakati
 
RIP na poleni sana mliofiwa na mliojeruhiwa tunawaombea mpone haraka.
 
Pole sana wafiwa wote, Nawaombea majeruhi wapone haraka. Huyo DC wa Same alikuwa reporter wa RFA na STAR TV miaka ya nyuma, nimeimiss sana sauti yake akiripoti matukio mbalimbali tokea Turiani Morogoro
 
Poleni sana wote mliopoteza wapendwa wenu. Na majeruhi tunawaombea wapone haraka.
 
Watu saba wamefariki dunia na wengine 75 wamejeruhiwa katika ajali mbili tofauti zilizotokea wilayani Same. Ajali ya kwanza ilitokea majira ya saa saba usiku wa kuamkia leo katika maeneo ya Njoro na kuhusisha basi la Kampuni ya Osaka lililokuwa likielekea Dar es Salaam, ambapo ilisababisha kifo cha mtu mmoja na wengine 52 walijeruhiwa.

Ajali ya pili ilihusisha basi aina ya Costa la Kampuni ya Mkokota majira ya saa2 asubuhiya leo, ambalo lilipinduka katika kona za milima ya Ilamba, na kusababisha vifo vya watu sita na majeruhi 23. Waliofariki dunia katika ajali hiyo ni wanakwaya waliokuwa wakisafiri kutoka Chome kuelekea Ndolwa.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Same, Dkt. Alex Alexander, amesema kuwa majeruhi wa ajali ya kwanza walipokelewa hospitalini majira ya saa nane usiku, huku majeruhi wengine 23 pamoja na miili ya marehemu sita ikifikishwa hospitalini mchana wa leo.

View attachment 3288047


View: https://youtu.be/D_2maGWZn4Y?si=_QUdY4lhQHgOjcfN

CCM wahini dili Mungu amewaletea neema ya wapiga kura, pesa isilazwe itembee, CAG atalalamika mpaka basi.
 
Back
Top Bottom