Watu tunasherekea utajiri wa Elon Musk kushuka

Watu tunasherekea utajiri wa Elon Musk kushuka

Yaani huyu Elon simpendi.Ana nyodo yaani na ile idea yake ya kupandikiza kipichi kwenye ubongo.Stupid kabisa aanze yeye kwanza kupandikizwa.Anajiona yeye ndo yeye na sometimes anaongea ujinga tu.Silipendi hili li baba .Tena ninaomba lishuke na lishuke tena.
Kipichi ndo nn
 
Hivi huwa unaamini jarida la forbes eti ndo linajua nani ni tajiri kuliko mwingine. Bila kuwapeleka wao taarifa hawawezi jua utajiri wako. Kuna watu ni matajiri zaidi kuliko hata hao lakini sio watu wa media
Unamaanisha kina vunja bei na Diamond?
 
Ngebe, nyodo, madharau, majigambo, kiburi, kujiona na kujiinua vimefika ukingoni.

Ni chereko na vifijo.

Elon Musk (Mwafrika Uchwara) mmiliki wa Tesla, Space X na Twitter utajiri wake umeshuka kutoka dollar billion 230 hadi dollars billion 168 na kujikuta kupoteza nafas ya kwanza utajiri duniani. Sasa hivi namba moja ni mfaransa billionaire mstaarab Bernard Arnault akiwa na utajiri wa dollars 172.

Wadau wengi tumepokea hii habari kwa furaha na shangwe. Watu tumefurahi hadi tumepata faraja kwenye umaskini wetu.

Musk alijionaga mungu mtu akidhani dunia ipo mabegani mwake. Na tunaomba utajiri wake uzidi kushuka asiwe hata kumi bora.

Kazaliwa Africa na kukulia Africa lakini hana msaada kwenye bara ilipomfikisha alipo. Watu tunakula mara moja baada ya siku tatu lakini hatukumbuki na hana fadhila.

Bora wote tu tuwe sawa kuwe na uihano.

Furaha ya maskini ni masahibu ya tajiri hasa kufulia.

Maskini Jeuri!
Unahisi atakuwa masikini kama ukoo wenu?
 
Yaani huyu Elon simpendi.Ana nyodo yaani na ile idea yake ya kupandikiza kipichi kwenye ubongo.Stupid kabisa aanze yeye kwanza kupandikizwa.Anajiona yeye ndo yeye na sometimes anaongea ujinga tu.Silipendi hili li baba .Tena ninaomba lishuke na lishuke tena.
Jambo, hadi wewe kweli 😀
 
Mi nampenda Elon,Kanye napenda watu vichaa vichaa hivi na mabilionea
Daah nimekuelewa sana.
Ndio wale mnapenda hata mapatna wako rafu rafu kila idara😄
 
Back
Top Bottom