Kura ya maoni ya hivi karibuni ya Kituo cha Utafiti cha Pew inaonyesha kwamba taswira ya Marekani imeharibika vibaya barani Afrika wakati wa miaka miwili ya kwanza ya muhula wa pili wa rais Donald Trump. Watu waliohojiwa katika nchi za Ghana, Kenya, Nigeria, na Afrika Kusini, tatu kati ya hizi sasa wanaipendelea China kwa kiwango cha juu kuliko Marekani, ikidhihirisha mabadiliko makubwa kutoka utawala wa Biden wa mwaka 2024.
Kwa ujumla, upendeleo wa Marekani umepungua katika nchi zote nne, huku tathmini chanya kuhusu China zikiendelea kuongezeka. Kenya na Afrika Kusini zimeonesha mabadiliko makubwa katika maoni ya umma, huku upendeleo wa China ukizidi ule wa Marekani; kiwango cha Wanaigeria wanaoipendelea China kimeongezeka kutoka asilimia 3 hadi asilimia 15 (78% wanaikubali China, 63% wanaikubali Marekani). Ni Ghana pekee ambayo bado inaipendelea Marekani kwa kiwango cha juu kidogo (68% wanaikubali Marekani, 64% wanaikubali China), lakini kiwango cha kukubali uwezo wa rais wa China kushughulikia masuala ya kimataifa (56%) kimezidi kile cha wale wanaomwamini Trump (54%).
Hitimisho hili linathibitishwa na utafiti uliofanywa mwaka jana na shirika la Afrika "African Barometer," unaohusisha nchi 30: 60% ya Waafrika wanaamini kwamba China ina ushawishi mzuri katika uchumi na siasa za nchi zao (60%), juu kuliko Marekani (53%) na EU (49%).
Kupoteza upendeleo kwa Marekani kunatokana na sera zake. Mtaalamu wa Baraza la Mahusiano ya Kigeni la Marekani Ebenezer Obadare anasema kwamba vikwazo vya viza, ushuru wa adhabu, kupunguzwa kwa misaada ya kigeni, na maneno ya uadui vinazidisha kuiharibu taswira ya Marekani. Kinachoikasirisha Afrika zaidi ni utekelezaji mbaya wa sheria dhidi ya wahamiaji wa Kiafrika nchini Marekani.
Kwa upande mwingine, China kwa muda mrefu imekuwa ikikuza uhusiano wa kina na Afrika, na faida zake za sera zinaendelea kuonekana. Sera ya ushuru sifuri kwa bidhaa za Afrika zinazosafirishwa kwenda China, iliyoanzishwa mwaka jana na kutekelezwa mwaka huu, imewanufaisha wauzaji nje na kupata pongezi nyingi. Zaidi ya hayo, Shirika la Ushirikiano wa Akili Bandia Duniani lililoanzishwa hivi karibuni, likiwa na wanachama 29 waanzilishi wake (ikiwa ni pamoja na nchi 10 za Afrika), linaiinua Afrika kutoka mpokeaji wa teknolojia hadi mjenzi mwenza wa utawala wa kimataifa—wakati vijana wa Afrika wanapokuwa waanzilishi wa vigezo na wakufunzi wa mifano, nia yao njema kwa China itakuwa kubwa zaidi.
Kama methali ya kiswahili inavyosema, " Ukitaka kwenda haraka, nenda peke yako, Ukitaka kwenda mbali, nenda na wenzako." Kuanzia makubaliano ya kibiashara hadi utawala shirikishi wa kiteknolojia, China inaonyesha usawa na kunufaishana kupitia vitendo vyake. Mabadiliko haya ya maoni ya umma si tu chaguo la sasa bali pia ni mwenendo usioepukika katika zama za leo.