KWANINI WAMERU WANACHUKIWA?
Kabila la WAMERU wanaopatikana mkoa wa Arusha upande wa ardhi yenye rutuba ya mlima Meru lugha yao wameikopa kutoka kwa wachagga(wamachame) na baadhi ya tamaduni zao, majina yao na hata vyakula kutoka kwa wamasai na wachagga na kutokana na udogo wa kabila hili mara nyingi ni kaskazini ndio linaumaarufu lakin sehemu zingine za nchi hutambulika tu kama wamasai au wachagga
Kabila la WAMERU ni kundi la mwisho kuhama la jamii ya wa cushitic ambayo asili yao ni kutoka Ethiopia ambapo Karne ya 18 walivofika Kenya waligawanyika katika makundi mbalimbali wengine waliishia Uganda ankole, wengine wakaenda Hadi Rwanda Leo hii wanaitwa watusi
Kabila hili dogo walivofika Kaskazini mwa Tanzania na kuweka makazi waliishia katikati ya wachagga na wamasai kuanzia katikati ya jiji la Arusha kama inavotambulika Leo hii Hadi kuzunguka mlima Meru hvyo kuleta taharuki kubwa ya mgogoro wa ardhi na kupelekea vita za mara kwa mara na jamii ya wamasai na wachagga hivyo kuchukiwa na makabila hayo na kuenezewa propaganda Kuwa Hawa watu ni wabaya na ndio maana Kila mchangiaji anakuambia Hawa watu ni wabaya lakini ukimuuliza mmeru alikufanyia nini Hana jibu la moja kwa moja hizi ni propaganda zilizoenezwa kwa vizazi dhidi ya WAMERU kwa vile ni wavamizi kama watusi walivovamia Rwanda na kuonekana tishio kwa wahutu Hadi kupelekea vita kwa uthibitisho Angalia mfanano wa pua au sura za WAMERU, Ankole au Watusi wa Rwanda utagundua watu Hawa ni ndugu, chuki hizi ni matokeo ya propaganda kama Urusi na marekani Leo hii mtoto mdogo wa kimarekani anaona Urusi kama ni adui hata kama haujawah kukutana ana kwa ana na mrusi au muulize mkenya yoyote atakuambia watanzania wanatuchukia wakati sisi hatuna hata stori nao, tabia ya kuwajumuisha watu wote kwenye kundi la tabia mmoja hizi ndio zinaitwa propaganda kama shabiki wa simba anavoweza kusema yanga wote hawana akili and vice versa au kama mikoa mingine wanavodhani mikoa mingine watu wote wa Arusha ni wadudu au kwamba wachagga wanaua waume zao au hawana mashepu😂
Huwezi kujiuliza kama kwa WAMERU Kuna viongozi wa dini au ndoa zilizodumu na zenye amani au watu mashuhuri na waliofanikiwa mfano Mkuu wa kwanza wa majeshi Sarakikya, Waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa, Mwandishi wa habari mashuhuri Millard Ayo, Miss Tanzania pekee aliyeshinda taji la Africa Nancy Sumari, Askofu Isangya na wengine wengi lakini ukichunguza 90% ya wanaowasema vibaya WAMERU ni wachagga na wamasai kutokana na sababu za kihistoria zilizotajwa hapo juu manake Kila kabila Lina watu wabaya na wazuri iweje mabaya tu ndio yasemwe na makabila mengine yote yana uchawi, umalaya, wizi na kuuwana
Kutokana na kuwa na maadui wengi WAMERU wakawa ni watu wenye hofu ya kuvamiwa hata historia mji wa Arusha ulianza baada ya WAMERU kuwaua wajerumani wawili hivyo kupelekea wajerumani kuweka kambi Arusha ambapo sasa hivi panaitwa viavia na WAMERU kukimbilia mlimani zaidi kujificha ikapelekea Kuwa watu wenye kujihami na wenye mshikamano sana hata mtu wa kwanza kwenda UNO kuomba uhuru alikua japhet kirilo na alienda kuomba uhuru wa WAMERU pengine ndio maana hakupata kutokana na kuisemea Meru badala ya Tanganyika kutokana na wao kutengwa na jamii zingine wakakaa peke yao jamii zingine wakaanza kuwaita tena wabaguzi😂
Lakini kiuhalisia WAMERU ni watu wenye roho nzuri na wachapakazi sana nashuhudia kwa vile Mimi ni mtoto wa baba mnyakyusa na mama mmeru hivi wamefikisha miaka 50 ya ndoa na nlichojifunza ni heshima aliyonayo mama kwa mume wake Hadi na sisi watoto tumekuwa watu wazima
Pia WAMERU na watu wachacharikaji sana nimeshuhudia mitaa kadhaa kariakoo ambayo mtaa mzima ni maduka ya WAMERU tu licha ya udogo wa kabila hili ambalo ni kama tu wa old Moshi au wasiha ambayo ni vikabila vidogo tu ndani ya kabila kubwa la wachagga lakini nadiriki kusema idadi ya WAMERU kariakoo wenye maduka makubwa unazidi hata idadi ya kabila kubwa kama wasukuma au wanyakyusa "I stand to be corrected" ni vile watu wengi wanawajumuisha kama wachagga hapo ndio utaelewa jinsi Gani Hawa watu ni wachapakazi licha ya uchache wao
Kwahiyo wasikukatishe tamaa hao watu mkuu kwa mmeru umepata jembe, wanaheshima sana, ni warembo na sio wepesi kukukimbia hata uwe na maisha magumu vipi mtapambana pamoja shida yao tu hawapendi kuonewa 😂 na hii nadhan ni kwasababu za kihistoria imeingia kwenye DNA yao
NB: Nlitamani kuandika kwa kifupi lakini makala ndefu ndio ingeleta uwelewa zaidi kwa mgeni 👏