Watu wa Dar acheni kuwatelekeza ndugu zenu stendi

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
1,831
Reaction score
5,489
Watu wengi wanaoishi Dar es salaam wakipigiwa simu na ndugu zao wa mikoani, hawataki kusema ugumu wa maisha ulioko Dar es salaam badala yake wanasifu uzuri wa jiji na raha zilizoko kwenye jiji hilo namba moja nchini Tanzania. Kupelekea kuwafanya na ndugu walioko mikoani kutaka kufunga safari wakihisi Dar es salaam kuna maisha raha mstarehe.

Ndugu hao wakishafunga safari na kufika stand ya mabasi Magufuli basi wanatelekezwa, na hao ndugu zao wa Dar uwazimia simu. Jambo ambalo limesababisha watu wengi wa mitaani kuongezeka jijini, ambapo kwa siku stand ya Magufuli upokea makumi ya watu waiokuwa na pa kwenda miongoni mwao ni hao waliotelekezwa na ndugu zao.

Kama uwezi kuwa mwenyeji wa mtu, si bora umwambie tu, atafute alternative kuliko kumtia moyo ya kuja kuishi Dar es salaam na kisha kumtelekeza. Kama maisha yamekuchapa, mwambie tu ukweli kwamba maisha yangu hayako sawa. Hili abaki mkoani, kuliko kujichanga nauli alafu unamtupa stand.

===

Pia soma: Afisa Ustawi wa Jamii Ubungo: Watu kutoka kanda ya ziwa wanaongoza kutelekezwa na ndugu zao Stendi ya Magufuli
 
Kuna mmoja kaniambia anakuja jumatano. Me nikakubali tu. Anzia kesho sipatikaniii.

Mnavopanga safari zenu huwa mnamshirikisha nani? Unaamua tu kwa vile flani yuko sehemu ngoja niende.unajua anapitia hali gani? Unajiamulia tu mwenyewe. Maisha yenyewe yashaharibika tukiwalaza na watoto wetu mnawaharibu.dawa yenu ndo hyo mtaishia magufuli stend hadi mkome.
 
Mimi nafanyakazi stend ya Magufuli na hizo kesi za watu kutelekezwa na ndugu zao mbona sizioni? Wanaweza kupoteana siku moja kutokana na matatizo ya mawasiliano kesho yake anapata mwenyeji wake! Ebu tupe ushaidi mkuu
 
Tutolee unafiki na ujinga wako hapa, .Ulitakiwa umwambie safari njema ila sina nafasi ya kufikia kwangu.
 
Mimi nafanyakazi stend ya magufuli na hizo kesi za watu kutelekezwa na ndugu zao mbona sizioni? Wanaweza kupoteana siku moja kutokana na matatizo ya mawasiliano kesho yake anapata mwenyeji wake! Ebu tupe ushaidi mkuu
Wakiwa njiani wanapiga simu kila saa .anafika kati huko simu inaisha charge. Hawatulii
Mtu anatoka mwanza hajafika hata shinyanga amepiga mara kumi kila mahali anatoa update
Hadi afike dodoma na simu ishaharibika kabisa. Anaingia dar hajui aanzie wapi.
 
😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 nimechekaa balaa
 
Fikiria unamwambia hivyo dada yako aliyekulea
 
Mimi nafanyakazi stend ya magufuli na hizo kesi za watu kutelekezwa na ndugu zao mbona sizioni? Wanaweza kupoteana siku moja kutokana na matatizo ya mawasiliano kesho yake anapata mwenyeji wake! Ebu tupe ushaidi mkuu
Wanaopotea ni wale wanaodhani Dar es salaam ni kijiji anapanda basi tu anashuka stendi analeta ujuaji wa kijijini akidhani akiulizia mtu yeyote jina la huyo ndugu yake kila mtu atakuwa anamjua

Akifika Dar ujuaji unaisha simu ya huyo nduguye hana kaja kichwa kichwa jiji anashangaa
 
Hiv mtu anafika dar ndo anakupgia? Hayupo serious, toa taarifa siku mbili tatu kabla mtu ajue anakupa jibu la ndio au la!!
 
Wanakuja tu kutembea eti anytime wanajiskia
Na hapo nauli ya kurudi na hela zingine anataka umpe na vitu kibao
Wanakosea mpigie mtu uje labda ndo unakuja chuo... Utakaa wiki then uhamie hosteli au kwako,

Au anakuja kweny sherehe.... Ila aje kutembea na sio kwa wanae apo pazito wallah...

Watu wapo bize na laifu
 
Asee Daslam na watanzania💔😅
Ni vyema kutoa taarifa mapema kama unakuja kwa jambo la msingi ili anaekupokea ajipange au akupange unipange.
Na kama unakuja kuzurura tu basi fika Daslam fanya mishe zako tenga muda kidogo wa kumsalimia umjuae ila sio kumvika majukum.
Watu wana ndugu chungu nzima na wote hufika Daslam kwa sababu zao huwezi wamaliza.
 
Hata watz waliopo USA hawatuambii ukweli wa hali halisi ya maisha ya huko, kimbembe tukifika tunakuta mchizi analala kwenye kichumba hata kugeuka hageuki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…