Watu wa Dar acheni kuwatelekeza ndugu zenu stendi

Watu wa Dar acheni kuwatelekeza ndugu zenu stendi

Watu wamejawa na roho mbaya sana.

Katika harakati za maisha nilipata kibarua Morogoro tatizo likawa wapi pakufikia ukizingatia kile kibarua kilikuwa hakitoi pesa za kujikimu nikamueleza inchaji wa Moro akanitumia namba za mfanyakazi mwenzangu aliyetangulia huko brother sitakusahau una roho nzuri sana na ulinipa ushirikiano katika kila jambo licha ya kuwa tulikuwa hatufahamiani kabla nipende kukuomba msamaha tena kwa kufumaniwa na mke wa mtu kwenye geto lako.
 
Hata watz waliopo USA hawatuambii ukweli wa hali halisi ya maisha ya huko, kimbembe tukifika tunakuta mchizi analala kwenye kichumba hata kugeuka hageuki
[emoji28][emoji28][emoji28]
 
Ndugu yako huwezi muacha stand na ukiona unashindwa kumwambia ukweli wa maisha yako ujue hapo kuna utata kwenye undugu wenu
Me nilishawah waza kumzimia sim ndugu yangu ila niliwaza sana nafsi ikanisuta nikaenda mpokea ubungo ila nikamwambia amezingua

Saiz ndugu yangu katoboa kwenye mambo ya kilimo yani hazipiti week mbili sijatumiwa vifurushi vya mazaga yani ndani mchele kibao hadi natamani kuuza

Amebaki kusema tu nilimsaidia kipindi ana shida hana kitu hawezi kunisahau, nikicheki msaada niliompa ni kufikia gheto kwangu tu akakaa wiki2 ila anayorudisha kwangu mpaka nimeanza kumuogopa sasa [emoji38][emoji28]
Wewe umekomaa kiakili na matokeo yake unayavuna.

Wengine wanaoingia mitini hawakumbuki kuwa maisha yanaweza kugeuka muda wowote ukasaidiwa na hao uliowakimbia.
 
Kiukwel hii hali sio dar pekee hata tulio nje ya tz hali hii inatupata sana ,, fikiria mtu mlikua jiran tu mmekua wote anatafuta namba yako anakupigia anasema yupo sehemu kaja kutafuta maisha ,,anaomba afikie kwako hapo hapo anakwambia yupo na rafiki yake ,,unafikiria ukiangalia unafamilia maisha yenyewe ya dollars yalivyokua high ,,,kinachofuata hapo unamblock kabisaa.
Duuuh kumbe hizi mishe zipo adi huko mitaa ya mbelez?! Mi nikajua ni Downtown swekeni huku bongo tu?![emoji28][emoji28][emoji28]
 
[emoji1787][emoji1787] hivi haya mambo ni kweli au mnafurahisha watu humu
Nilichokipenda kwenye hii mada leo watu wa Dar wameamua kutoa ya moyoni na kufunguka ukweli .. safiii sana [emoji28][emoji28][emoji28]
 
Sidhani kama unaweza kumuacha ndugu yako stend,,itakuwa labda majirani zao wa huko Mbwinde
Ni kweli, damu nzito sana kuliko maji labda tu uwe umevamiwa na shetani
 
Wenyeji wanafurahia zawadi Kama hizi vile.
a0e33a36dca344dd89d96718f27df4c9.jpg
 
Usiende Kwa ndugu, jamaa au rafiki bila kumtaarifu iwe Kijijini au mjini, maisha yanabadilika sana. Pia mtu akihitaji hifadhi maskani kwako Kwa muda mueleze uhalisia wako maamuzi yabaki mikononi mwake.
 
Usiende Kwa ndugu, jamaa au rafiki bila kumtaarifu iwe Kijijini au mjini, maisha yanabadilika sana. Pia mtu akihitaji hifadhi maskani kwako Kwa muda mueleze uhalisia wako maamuzi yabaki mikononi mwake.
Mkuu hawatoi taarifa .wanakuja ghafla
 
Mkuu hawatoi taarifa .wanakuja ghafla
Mtu akija bila kutoa taarifa haijalishi ni nani... Akubali lolote litakalo mkuta asilaumu...maisha yamebadilika sana. Niko kijijini ila mgeni usije kwangu bila kunitaarifu labda kama unakuja tu kukaa masaa kidogo na kuondoka lakini kama ni kulala hata kama ni siku moja Nitaarifu kwanza, itakuwaje maisha ya mjini? Miss Natafuta pole sana kwa changamoto hiyo.
 
Back
Top Bottom