Watu wa Dar acheni kuwatelekeza ndugu zenu stendi

Hao ndugu ni WA kuanzia Miaka mingapi?18 -,20 hao unawapa nauli warudi nyumbani hao wengine achana nao watachagua wenyewe wabaki mtaani au warudi nyumbani unaendaje Kwa watu eti kusalimia tu
 
Hata kama kuna uzuri wa maisha (uzuri huo una gharama) sasa swali ni kwamba hao ndugu wa huko mikoani wanaweza hizo gharama ?

Kutokana na Maelezo yako jibu ni kwamba hawawezi....; Anyway karne hii mtu anaweza kujitosheleza yeye haimaanishi mkiongezeka wawili bado atajitosheleza (unless unakuja kutoka anapotoka na Nusu Bajaji ya Mahindi, Maharage na Pesa ya Mtungi wa Gesi)
 
Kuna jamaa yangu mmojaa yupo Dar Miaka mingi sana Sasa tatizo linakuja ana ji proud sana......

Kuna siku nikmweleza nipo dar nmkuja tok majuzi kuna mishe nafatilia fanya tukutane...kiukweli sikua Dar... Jamaa
Mara safari za gafra mara visingizio kibao..

Sasa Kuna siku nikaenda Kwa mishe zangu
Nikakutana nae ubungo USO Kwa USO....
Sababu nyingiiiingi

Kimsingi ukiwa Dar be Real...ishi maisha ya uhalisia wako kua mkweli.......
 
Umemaliza.
 
Watu mna roho mbaya kwahiyo umeamua kunisema JF, basi ntakuja na jogoo na mchele 100kgs.
 
Miss Natafuta umenena vyema pasi na kutafuna maneno. Jina lako linaonesha umekuja mjini kutafuta. Hao wanaokuja mjini kukutafuta wewe watajiju.
 
Miss Natafuta umenena vyema pasi na kutafuna maneno. Jina lako linaonesha umekuja mjini kutafuta. Hao wanaokuja mjini kukutafuta wewe watajiju.
Mkuu mgeni akija kwako ni budget ingine ujue.akija anataka aishi kama mfalme hata nauli ya kurudia umpe wewe bado hawezi kuondoka mikono mitupu.hawako fair kabisa
 
Hata mimi niliwahi kumuacha mtu sababu ya ujinga wake. Alipofika ndio ananiambia niende nikamchukue,wakati anatoka mkoani hakuniambia.
Nikamwambia alale hapo, nitaenda kesho asubuhi kwa kuwa huku niliko kwa majira haya kuna Panya road.
Aligongwa na mbu usiku mzima nikaenda kesho saa 4 asubuhi.
Hilo lilikuwa fundisho, kwa sasa kila akitaka kuja lazima anipigie.
 
Kwani ukimwambia una maisha magumu itakuwaje.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…