Watu wa Dar es Salaam noma. Mama ana mtoto hamtaki kumpisha kiti!

Utakuta mpo mwisho wa gari/kituo, Gari kibao zinapakia, Kaacha zote kaifuata inayoondoka iliyojaa seat afu anataka apishwe.
Umenikumbusha. Nilipanda basi moja mwanzo wa kituo. Basi nililopanda lilikuwa limejaa na linaondoka lakini kulikuwa na mabasi mengine yanapakia kwa ruti ile ile. Mara akaja mama mmoja mbio na mtoto akadandia, na kuja kwenye siti yangu na kuniambia.... ''Kaka naomba unisadie kubebe mtoto'' (ili yeye asimame). Wala sikupepesa macho bali nilimwambia sitaki!
 

Ulimkomesha hatari hahahah
 
Mjini kila mtu na stress zake hatuna utumwa wa kupishana kwenye seat,wewe nunua hiace zako ziwe zinawabeba hao wajawazto wa wazee wanaopenda seat vitonga
 

Hii tabia ya kuwekeana siti iko sana Makumbusho inashangaza sana.
 
Nimepanda daladala,live sade, ubungo nimeshuudia mama wa watu,akiwa na mtoto, bado amesimama tena mimi nimemkuta,kwachini ya siti kuna vijana, wamekaa tu, tena pamoja na wadada wanachezea sm zao, da, jamani tuwe na uruma bs,mpaka nikakumbuka uzi mmjo, ulitupiwa juzi umu,tuwe na uruma bs,
 
Aisee !! Hii ngumu kumeza we jamaa nahic umekomaa na maisha na huu ndio ukakamavu ninaoutaka maana kuna baadh ya wazee wanajionaga mungu watu na kuna mda wazee hutumika ata kwenye dili xa utapel
 
Upo sahihi sana mkuu,hilo lipo sana.......pia binafsi hata nikimkuta mwanafunzi amekaa staki anipishe maana magari yanajaa sana hata sehemu ya kuweka mguu hakuna,pia watoto asubuhi wanawahi hivyo wanachoka ndiyo maana wengi huwa wanalala wkt wamesimama na nature ya usafiri ndiyo inafanya ionekana watu hawana adabu,baadhi ya route foleni na joto......wakati wa mvua mwingine anapanda amelowa....sasa ule mbanano joto inakuwa harufu kali
 
Wanajifanyaga wazungu.
Sisi huku kanda maalum wazee, walemavu na wamama wenye watoto ni raha kunako usafiri.
 
Wana loho mbaya sana watu wa dar yaani unaweza hata ukawa unaibiwa wala hawajali wanaendelea na mambo yao
 
Wana loho mbaya sana watu wa dar yaani unaweza hata ukawa unaibiwa wala hawajali wanaendelea na mambo yao
Hii kwel !! Mm niliwah kuibiwa kariakoo karibu kabisa na maduk ya simu tapel alieniibia mpaka anakimbia hakuna alie nisaidia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…