Watu wa Dar es Salaam noma. Mama ana mtoto hamtaki kumpisha kiti!

Watu wa Dar es Salaam noma. Mama ana mtoto hamtaki kumpisha kiti!

Kati ya tabia zinazokera ni kumpisha "mtu mzima" kiti ndani ya usafiri wa umma then unakuta anashuka kituo cha jirani tu; wakati huo anashuka wewe umesimama jirani yake wala asante hakuna wakati kiustaarabu alitakiwa sio tu kusema asante bali kukurudishia siti yako ila ndio hivyo saa hizo wala hana habari na wewe uliyempisha kama aliiokota vile! So, unapoona watu wanakausha kuna mambo mengi; shukrani ya punda ...
Swali la kuudhi nitakalomuuliza hiyo mimba ni ugonjwa?
 
Wengine ni viherehere..unakuta magari yapo mengi yamepanga foleni hlf anakuja kupanda lililojaa. Simpishi kwa kweli..
Exactly, unakuta limtu linapandia makumbusho stendi kabisa na linataka watu walihurumie kuliachia siti wakati lingesubiri lingekaa...nashangaaga sana watu wanaofanyaga hivi afu wanaona watu wabaya
 
Habarini wana JamiiForums

Leo ndio nimejua mjini shule. Asubuh majira ya saa 5 hivi nilikuwa nimepanda basi la G/MBOTO-KIVUKONI nikitokea G/MBOTO. Nilibahatika kupata siti kipindi safari inaendelea, ghafla akapanda mama mmoja hivi kabeba mtoto.

Mara ya kwanza nilitake easy nikijua kuna mtu atampisha, eeh maajabu watu wamekausha utasema hawajamuona vile. Na katika viti idadi kubwa ilikuwa ni akina mama na wadada baadhi, wanaume walikuwa wachache lakini wapi, wale wanawake wakaupiga kimya basi linaenda kasi huku linatikisika mama mkono mmoja kamshika mtoto mkono wa pili kashika bomba. Watu wamekausha, uzalendo ukanishinda ikabidi niinuke nimpishe, ikabidi nisimame safari nzima.

Sasa basi halijafika mbali kaingia mmama tena kabeba mtoto, watu wamekausha. Huyu hakupata kiti ata cha huruma mpaka tulipofika M/MMOJA kuna mtu akashuka ndio akapata nafasi.

Sasa kimbembe kikaja tena jioni kipindi narudi, kuna mmama kapanda basi na mtoto watu wamekausha mpaka nikaanza kusikitika sasa kipindi navuta gia kusimama nimpishe ndio ghafla yeye akamuomba mdada mmoja amshikie mtoto. Kwa bahati nzuri yule dada akaamua kumpisha kabisa.

WATU WA DAR MNAKWAMA WAPI?
Aisee jioni kila mtu amechoka anaitaji kukaa kwenye siti angalau apunguze kero ya foleni then umpishe mtu usimame na basi limejaa aisee mbona mtihani hapo kila mtu anakuwa busy na simu yake
 
Hii hoja haipo sawa watoto ambao tayar washapata uwezo wa kujisimamia hawa wasimame tu ila wale vichanga ambao muda wote wanahitaji uangaliz wa mama ndio wasaidiwe
Sio sahihi maana na wao wanachoka sana, wengine wanaumwa au njaa. Wewe ukipanda daladala na mtoto wako huwa anasimama wewe unakaa?
 
Hapana sio sawa !!! Ila ww kwa stor ulizotoa apo juu mmh nahic kuna tanur ndan ya moyo wako
Sina tanuru lolote. Why uone kuwa mwanamke ampishe mwanamke mwenzie na sio mwanaume. Wewe ndo una tatizo ..ukarimu hauna jinsia
 
Exactly, unakuta limtu linapandia makumbusho stendi kabisa na linataka watu walihurumie kuliachia siti wakati lingesubiri lingekaa...nashangaaga sana watu wanaofanyaga hivi afu wanaona watu wabaya
[emoji2][emoji2]
 
mimi nipambane kupata siti halafu yeye aje nimpishe my friend hapana na kuna wengine wanatabia wanagombania gari halafu anamuwekea mwenzie siti eti ina mtu yeye aje akae nakubeba nakaa halafu wewe ndio mpishe wewe na foleni hizi za dar saa 2 upo tu umesima mpaka miguu inataka kuungia ndani
 
Nilikuwa nipo mbal nae yaan aliposimama yy na mm kuna umbali na apo karibu kulikuwa kuna vijana na mabint akimama wengine ambao hawana watoto wamekaa
Nafikiri wa kulaumiwa hapa ni serikal kwa kutokuwa na sera nzuri za usafiri wa abiria.
 
Kwanza karibu jijini kwetu,hayo ndio maisha yetu ya Kila siku,hao kina mama unaowaona wamekaa wote hao ni wazazi si wagumba,hayo waliyopitia hao kina mama uliiwaona Wewe ndio ambayo wamnapitia hao waliokaa leo pindi wakitoka na watoto wao!so hapo ni ngoma droo,Kama hauna usafiri binafsi DAR kutembea na mtoto lazima uwe na nauli ya ziada Kama kuzunguka na gari au kupanda Bajaj,ila kutegea huruma za waja wakupishe hiyo sahau!maana Wana walishatendwa ...Binafsi sipishi mama kijacho Wala mama mtoto napisha mgonjwa tu ninaeona kabisaaa huyu anaumwa.
 
Joto la dar msongamano wa watu ndani ya daladala foleni , yani mnaweza kusimama kwenye foleni hata masaa 3 alafu nimpishe mtu siti. Hapana kwa kweli
Hujaongelea ulivyopigana pale mlangoni nusura uibiwe kisimu chako😂
 
We endelea kuwapisha ila itafika kipindi umetingwa utakausha tu,yaan mikikimikiki sababu zinazochangia watu kutowapisha
1.kutokan na pilika za jiji unakuta mwingine kachoka hana hali yaan yeye nwenyewe kajichoka haya anampisha vipi mama mtoto au mzee
2.baadhi ya wamama kujitia wanaweza wakiona gari wao wanafyatuka washazoea maisha ya kusimama ko hata usipompisha anaona poa,m kawaida huwa nawapisha ila kuna sku magar yalikuwa mengi maza anaona limejaa akapanda nikamkaushia
3.roho mbaya za baadhi ya watu au kuona unatoa msaada kwa mtu hata hakujui utakuwa unafanya hvo daily,hunijui sikujui pambana na hali yako
N.B nakumbuka mwaka jana nilkuwa nmepanda gar mbagala to G/mboto gar siti zikajaa wakasimama kizuian akapanda mzee hko nyuma anawalazimisha vijana wampishe jamaa wakakausha dah mzee aliwaka akidai hawajalelewa kimaadili m nikkuwa nimekaa zangu mbele kdogo nkaona isiwe kesi mzee njoo ukae ila sikuona kama alikuwa na haki ya kuwatukana vile moyoni nkawaza mzee kama ulitaka starehe mpaka unazeeka ungekuwa na usafir wako nkaamua kukausha
Sasa ulimpisha wa nini mzee mshenzy mshenzy huyo?ulitaka kuwaprove wrong wenzio waliokataa au?
Suala la kupisha wazee ndio sitaki kabisaaa kulisikia imagine natoka na mama yangu mtu mzima sijaona mtu akimpisha Sasa Mimi napisha mama wa mtu ili iweje?
 
Kuna maza mmoja niliwahi kumuonea huruma nikambebea mtoto alaf mtt mwenyewe sijui kamlisha vitu gani inaonekana alimchanganyia vyakula huko alipotoka na kweny gar akampa tena mahindi ya kuchoma na juice, dogo nimembeba saa ngapi asitapike bahat nzur matapishi hayakunipata Mimi yakampata dada niliekua nimekaa nae jirani.
Sikuiz na mm najikausha kiaina kuliko nibebe mtt wa mtu bora nimpishe siti akae na mtt wake, na mkitaka msaada hakikishen watt wenu mnawaweka kwenye Hali ya usafi
 
Hii ya akimama kutowapisha akimama wenzao wajawazito au wenye watoto ndio inaniua nguvu kabisa
Wewe na wewe hamnazo kwanini ulaumu wanawake tu, na ujue dar watu huzunguka na gari hulipa Mara mbili, pia kuwa na mimba au mtoto inahusu Nini watu wengine, gari imejaa unaingia ili upishwe then ulaumu wengine. Huwa nashangaa wanaume wanaolaumu wanawake, pia hujui watu wengine Wana matatizo makubwa
 
Sasa ulimpisha wa nini mzee mshenzy mshenzy huyo?ulitaka kuwaprove wrong wenzio waliokataa au?
Suala la kupisha wazee ndio sitaki kabisaaa kulisikia imagine natoka na mama yangu mtu mzima sijaona mtu akimpisha Sasa Mimi napisha mama wa mtu ili iweje?
Hapana niliona kelele zimekuwa nyingi
 
Kipindi naishi Goms tena ile fly over bado niliapa hata kikongwe,mjamzito sitowapisha siti


Unakaa kwenye basi masaa 2 au 1:30 foleni kama lote,umbali wa safari nk

Usichukulie poa Goms Kunachokesha ushikilie bomba tena foleni na umbali wa safari plus joto aah ndio kawaida kwa bus za goms

Pia abiria wa goms walikuwa wanaongoza kwa kulala karibia nusu ya abiria hulala ..umbali,foleni foleni

Wasamehe bure watu wa goms
 
Back
Top Bottom