Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,984
Baada ya akina Gambo, Sabaya, Mneti, Muro, na viongozi wengine kutowesha amani na furaha ya Xmas Kaskazini kwa kisingizio cha kulinda amani na kuepusha vurugu hatimaye mwaka huu tunaona Ndugu zetu kwa mara nyingine wakirejea makwao Kwa furaha huku biashara zikipamba moto.
Ni kama wamepata Uhuru ulioibwa na baadhi ya watu walioaminishwa kwamba ukanda flani ni watu wasiopaswa kufurahi huku hata biashara zikitakiwa zimilikiwe na watu wa mrengo flani tu na ukitaka kufungua biashara ukiwa na mrengo tofauti basi utafilisiwa au kufanywa vyoVyote uondoke sokoni.
Nimpongeze Mama kwa kufuta ukiritimba wa akina Sabaya na akina Jeryy Muro na vikosi vyao, nimwombe atuwekee utaratibu mzuri wa kikatiba utakaozuia yaliyopita yasijirudie tena.
Akina Manka kuleni maisha msiwasikilize wasiojua kutafuta, msiwasikilize wasiopenda kwao, msiwasikilize akina ishomire tunaokimbia makwetu na kuja kuwekwa lockdown huko Kwa watu. Vibe la Moshi lafaa kusindikizwa na bia tamu