Mchaga mwenye akili zake timamu ndio wewe baada ya marehemu Mengi, mwana FA ameshauri kwenye nyimbo tafuta pesa ila usipige nazo picha…. Wachaga wengi ni wapiga picha na hela ukitizama matukio yao hasa wakati huu wa sikukuu za kufunga mwaka.
Ni vigumu sana kuwaona wahindi ambao ndio jamii tajiri zaidi hapa Tz lakini kama ulivyosema wako very humble, kina Mo utawaona zaidi wakipost yatima, wahitaji kama ilivyokuwa enzi za mzee Mengi. Ile mjengo alijengewa mama mapacha wa Mengi ingekuwa ni mchaga ordinary tungeanza kuonyeshwa kuanzia kiwanja, msingi, beam zikifungwa lkini ajabu tumekuja jua baada ya mchaga special kuenda zake.
Unajua hata jamii ya wapemba na wazanzibar huwa lazima kipindi Cha sikukuu especially za kidini nao henda makwao na boat huwa shida kupata nafasi kama hujakata ticket mapema .
Jamii za wahindi nao wakati wa sherehe za Diwali wengi huondoka nchini kwenda kujumuika na ndugu zao.
Kiuhalisia Moshi jamii kubwa ni wakristo hivyo imekuwa utaratibu wa kukutana wakati huu wa sikukuu especially mwisho wa mwaka ili kuweza kusherehekea pamoja na kujadili masuala mbalimbali ya kifamilia ikiwemo changamoto tunazopata na kuangalia namna ya kusaidiana.
Sasa huu utaratibu ni ngumu kwa baadhi ya jamii sababu kuu ni mchamganyiko wa dini pia, unakuta familia ni moja Ila dini tofauti hivyo wakati wengine wanashangilia Xmas wengine wanasubiri Eid hivyo huwa ngumu kidogo tofauti na huku kaskazini ambako jamii kubwa ukristo umetawala hivyo huwa rahisi.
Ni sawa na Pemba na Unguja Nako wakati wa sikukuu ya Eid huwa hivyo hivyo, Mara nyingi hizi siku za holiday watu huzitumia kukutana ndugu na marafiki Ila mostly zile jamii zenye kuabudu dini moja.
Sasa hii ya watu kuwasema wengine kwamba hawaendi kwao sio sahihi pia ukiona umepata bahati ya kuwa dini moja kama wapemba na watu wa kaskazini ni jambo la kushukuru Mungu kwakuwa mnajikuta kipindi cha sikukuu mnakuwa mnasherehekea pamoja hivyo huweza kuwakutanisha pamoja.
Kuhusu pesa aisee kila jamii Wana pesa labda watu hawajakutana na wasukuma au wakinga au watu wa kigoma, Wana pesa na wapo kimya tu .
Mwisho wa siku ndio nachosema, ukiketa mbwembwe sana kumbuka wateja wako wanatoka kwa haohao unaowaletea mbwembwe sema wao wanaamua kunyamaza tu Ila nao wakiamua wasinunue kwako hutoki hapa mjini salama.
Tunategemea a kama jamii. Utamaduni fulani usionekane ni wa maana kushinda mwingine, hii ndio ukifanya wazungu wachukiwe na jamii nyingine sababu ya kujiona wao ni Bora kushinda wengine, kila tamaduni ziheshimiwe.
Karibuni Shanty town .