Kurutu wa Mungu
JF-Expert Member
- Oct 23, 2017
- 366
- 578
Nakumbuka enzi hizo kwenda Disco Toto Tembo Beach kila sikukuu za Mwisho wa mwaka, Wasanii wakija Karume Stadium tunasubiria mda wa fungulia mbwa ndipo tuingie wakati kiingilio ni 1000 tu watoto.
Watu maarufu kama Tajiri mwenye mbwembwe Nyakiteri, Dereva wa mbio za magari Mama's, Hussein Sokoni, Redio yetu pendwa Victoria FM hapo utawakuta wakina Boke Wambura, Maregesi Girishon, Emmanuel Chibasa, Issa Nundu, mzee wa Mafua Robson Wangaso na wengineo, mitaa ya Nyasho hapo ndilo chimbo la kujipatia mavazi.
Fujo za Musoma Tech na Songe hadi kupelekea Songe kuwa ya wadada, Mitaa maarufu kama Mukendo, Iringo, Mwigobelo, Majita Road bila kusahau vibaka wa Magamaga, na kila likizo tunakutana tuition Mwembeni hapo utakutana na watoto wa Isenye, Ikizu na sisi wa Bweri Makatani.