Watu wa Tanga nawaita hapa

Watu wa Tanga nawaita hapa


Jamani ndugu zangu wa Tanga kwani alietuloga nani? fursa tunazisikia ila hata hatushtuki wanakuja walowezi wanajizolea fursa na sisi tupo hapa hapa kweli, zinatangazwa zabuni mpo kimya mnakuja kukurupuka dakika za majeruhi watu wameshasafirikutoka mikoani mbali huko kukimbilia fursa.

Na hata mkipewa nafasi hamchangamkii mpk mnawapa watu nafasi ya kujipandikiza na kuwahia nafasi kupitia wachahce wenye nazo ambao ni waroho na wenye tamaa ya pesa. Halafu mnalalamika mji unazidi kufa wakati pesa zimekuja na zinaondoka kurudi mikoa mingin. Mradi wa ujenzi wa Jetty ungekuwa umetangazwa vizuri na vyombo vya habari vya hapa tanga na serikali kwa ujumla.

Huu mradi ungerudisha hadhi ya mkoa wetu kwa jinsi ulivyo na tija ila cha kusikitka hata wale waliofidiwa baada yakupisha eneo la ujenzi badala ya kuzungusha mrdini pesa wengi wamekwenda kuoa kuongeza wake wengine eeeehh Mungu baba. Nini shida?

Kunahaja kupaza sauti kurudisha mkoa kwenye chati yake, fikiria mkoa umeshakuwa jiji lkn ni kheri hata kipindi ulipokuwa mji. Wana Tanga tuamke jamani hali tete inaumiza. Viwanda vimebaki kama magofu, wagosi wa kaya wamechoka kupiga kelel wameamua kujiajiri nchi imewekwa bond.
Achaneni na CCM!
 
Alietuloga na alaaniwe kutoka tanga ya viwanda mpk tanga ya magofu inaumiza sana
Hakuna kulogwa ni Umwinyinyi umekithiri.
Ingekuwa rahisi ningeeabeba wooote waende jkt au mambo wakapate ujakamavu kidooogo.
 
Ongezea na Kupenda Ngono

Ni Mkoa pekee umebarikiwa kuwa na Mawaziri Karibia 4.Lakini sinahakika kama wanaumia kwa kudorora kwa uchumi wa Mkoa(sipendi kuita Jiji)

1.January
2.Ummy
3.Juma
4.Khamisi
Huyo January Ondoa kwenye list,
Waziri/Mbunge Gani Jimbo lake halina hata Nukta ya Lami? Karavati tuu limemshinda, Asaivi maji yanapita Juu ya barabara... Watanganyika mkimpa huyu mtu Uraia namba 1 mmekwisha...
 
Hakuna kitu kama hicho hakunamahali pana uchawi kama dar es salaama maana kuna mvurugiko wa makabila kila mtu anajihami
DAR ES SALAAM haina kabila lakini DSM ina masikini wengi hata hivyo masikini wengi DSM ni wakazi wa mikoa ya pwani
 
...Inahuzunisha Sana ! [emoji45] Ukikumbuka Tangold iliyotoa Juisi ya Embe iliyokuwa Nzito na Tamu Sana!
Kiwanda Cha Sabuni kilichotoa Mbuni na Gardenia.
Kiwanda Cha Chuma.
Kiwanda Cha Mbolea
Kiwanda Cha Plastiki Amboni zilikotoka ndoo na mabeseni Bora vya Plastiki.

...vyote vimebaki Historian TU.

Tanga kunani palee ?
Sasa hivi Tanga imebaki na kiwanda cha warembo
 
Hakuna kulogwa ni Umwinyinyi umekithiri.
Ingekuwa rahisi ningeeabeba wooote waende jkt au mambo wakapate ujakamavu kidooogo.
Umenena kweli, ila kuna wanawake wazuri na wanajua kupika vyakula vya kunukia vizuri.
 
Ongezea na kupenda ngono

Ni Mkoa pekee umebarikiwa kuwa na Mawaziri Karibia 4. Lakini sinahakika kama wanaumia kwa kudorora kwa uchumi wa Mkoa (sipendi kuita Jiji)

1. January
2. Ummy
3. Juma
4. Khamisi
wote wa ccm
 
Hivi na sisi wakulima tunaoishi huku Lushoto milimani, tunaruhusiwa kuchangia chochote kwenye huu uzi?
 
Vijana Tanga wote wamekimbilia Dar,wamebakia wazee,ila twende mbele turudi nyuma Tanga pazuri sana.Ukitaka kuifaidi Tanga uwe na Baiskeli au Usafiri wako binafsi,halafu uanze kutembelea mitaa unayotaka wewe ,isiwe ni boda au Taxi,ni mji mzuri kiasi chake.....
 
Back
Top Bottom