"Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza

"Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza

Pascal nakufuatilia sana siku nyingi unamsifia sana mama Samia.Sisi wote tunamwona jinsi mama Samia alivyo 'humble' ,mwenye lugha tamu,mwenye subra na haiba kubwa lakini tumekaa kimya .Wewe sasa umezidi.
Mkuu senzighe , was is a problem?.
p
 
hivyo kusema mama samia hivyo ndio kuonesha Muungano hauna matatizo?
hakuna anayesema muungano hauna matatizo, lakini yanatatulika na yanatatuliwa!.
Muungano kuwa unamkorogeko sio siri

TUME YA KISANGA
TUME YA NYALALI
TUME YA WARIOBA
Zote hizo zilichukua maoni ya wananchi na wakaelekeza hatua za kufuatwa
Muungano utabakia kizungumkuti kama wazanzibar hawatopew nafas ya kuongelea Muungano wautakao
Hicho ndicho alichokisema Mama hapa!.
Suluhisho pekee la Muungano ni Watanzania na khasa wazanzibar waulizwe tena kwa uhuru na uwaz aina ya Muungano wautakao
Rukhsa
Hoja ZANZIBAR inafaidika ZANZIBAR ktk Muungano hpja ya Kipuuzi sana
Pascal huwezi ukatusemea ss pia tunavinywa!
Ni mimi ndio nimesema ama mimi nimeripoti tuu kilichosemwa?. Jee huyu aliyesema haya sii Mzanzibari?.
p
 
Viongozi wengi wa Tanzania huwa wanazungumza vizuri tu kwa hiyo sijaona maana ya wewe kusema mama yetu Samia anazungumza vizuri labda kama ulitaka kutwambia anazungumza vizuri kuliko hata b...…..wake
ndo maana yake!.
p
 
Unataka kutuaminisha kuwa uchaguzi wa rais mwaka huu umeshafanyika na mshindi kujulikana?
Uchaguzi Mkuu wa rais anafanyikia mioyoni mwa watu siku nyingi kabla, mfano sasa japo tuko 2023, lakini uchaguzi wa rais wa JMT wa 2025 ameisha chaguliwa mioyoni mwa watu, uchaguzi ni kukamilisha tuu taratibu!.
P
 
Huyo Mwandishi angemuuliza makamu wa rais je Revolution council ya Zanzibar kipindi hicho iliratify articles of union? Maana kuna upotoshaji mkubwa sana juu ya hili suala. Na sababu ofisi yake inahusika na Muungano nafikiri majibu anayo.
Hii ni hoja very valid na haijawahigi kupatiwa majibu!. hata mimi niliwahi izungumza!
p
 
Mwanamke ambaye naweza kumpigia kura kwa Tz ni kati ya hawa wawili: 1 Fatuma Karume na Maria Sarungi, hawa ni watoto wa viongozi wakubwa sn hapa TZ lakini wamekataa kuwa sehemu ya mfumo ambao keki ya Taifa wanakula wachache, hawa wadada kaka zao wameshindwa lakini wenyewe wameweza wanapigania maslahi ya nchi na siyo maslahi yao binafsi, Fatuma Karume na Maria Sarungi kama siyo kupigia maslahi mapana ya Wtz sasahivi wangekuwa mawaziri.
Washauri wagombee 2025 uwape kura yako.
p
 
Anazungumza vizuri kwa unyenyekevu mpaka raha.[emoji15][emoji15][emoji15]

Kwahiyo unaibiwa kirahsi vile kwa maneno matamu hata kama ni ya kilaghai.?

Sijasoma bandiko lote, nimeishia hapo tu... acha niimagine hiyo mpaka raha.[emoji39]
malizia kusoma bandiko!.
p
 
Back
Top Bottom