"Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza

"Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza

Kaka Pascal Tabia ya mtu huwezi kuipima kwa mazungumzo pekee yake. Suala la kuwa vizuri katka kupangilia hoja ya mambo ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania sio credit za kujiridhisha Kama mtu huyo atauweza urais ipasavyo.
Naunga mkono hoja, kipimo kisiwe mazungumzo pekee.
Kwa mitazamo yako kwa kigezo Cha logic katka kufanya analysis ya mambo ndio sifa kuu ya kuwa kiongozi mkuu wa nchi Basi Leo hii tusingekuwa na Rais Kama Dr John P. Magufuli pamoja na sifa kedekede ambazo umempa Mara nyingi kuhusu utendaji wake katika Taifa Hili.
Mbona nilisema kila kitu kumhusu JPM tangu 2014, nilisema Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli na baada ya uchaguzi nikasema Elections 2015 - If you can't beat them, join them! He is the worst dictator. Let's pray for him! but he kept changing for the better, hivyo nikaanza kusifu, hadi anatwaliwa ni straight peponi!.
Pascal utakubaliana na Mimi kwamba Rais Magufuli hayupo vizuri Sana katka kupangilia hoja lkn yupo vizuri katka kusimamia kile anachokiamini na baadae kuleta mawazo chanya kwa wananchi.
Nakubaliana na wewe 100% kwa 100% na hiki ndicho wananchi wanachotaka!, changing people's mindset, Tanzania sio nchi masikini, Watanzania sio masikini!, ukichange mindset kutoka umasikini na kuwa tajiri, unakuwa tajiri!. Positive outlook and positivity na positivism attitude!.
Usipokubaliana na Mimi Basi wewe Ni msifiaji tu bila kujua unachosifia kina nantiki gani ukirejerea post zako nyingi zipo humu za kusifia utendaji mzuri wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania .
Mimi sio msifiaji tuu kama machawa!, kila nikisifu kitu naweka na reasons, na hata huyo ninayemsifu akikosea namkosoa!.
Na ukikubaliana na Mimi kuwa uongeaji sio utendaji Basi post yako hapa juu haina mantiki yoyote zaidi ya kusifia facial expression ya Mama Samia
Japo nakubaliana na wewe kuwa uongeaji sio utendaji, lakini naamini by now na wewe utakuwa umeona how much I was damm right!.
Kwahyo mi bado nakupinga kwamba upangaji wa hoja sio kigezo Cha kuwa Rais. Tanzania Sasa hatuhitaji viongozi wa kusimama majukwaani wakipanga hoja kwa umahiri ya mikakati lakn utendaji mbovu. Tunahitaji kiongozi Mwenye Kutenda zaidi kwa wananchi sio porojo
Naunga mkono hoja na naamini hili utakuwa umeliona na kulishuhudia.
Need I say more?.
P
 
Pascal Mayalla,
Visiwani wanasiasa hawafanyi "doublespeak" Tell It Like It Isn't: A Campaign Guide to Political Doubletalk . Kweli labda yupo CCM ila moyo upo upinzani. Na historia ya kisiasa Zanzibar lolote linaweza kutokea maana tunaona huko Zanzibar jaji mkuu Ali Haji Pandu kujiuzulu, Maalim Seif waziri kiongozi kujiuzulu, makamu wa kwanza serikali ya maridhiano SMZ kujiuzulu Seif Sharrif Hamad, mwanasheria mkuu wa SMZ kujiuzulu .....listi ni ndefu vigogo waZanzibari halafu wanajitoa au kufukuzwa CCM na kujiunga kambi ya pili yaani almaaruf upinzani.

February 17, 2020

FULL HISTORIA YA MAMA SAMIA

Mama Samia anakubali hoja nzito za wapinzani, nilikataa pendekezo la kuwa Makamu wa Rais

Makamu wa Rais wa serikali ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Hassan Suluhu asema kilichomsukuma kuingia katika siasa ni maoni na hoja za mashiko za wapinzani Bungeni / Baraza la Wawakilishi ambazo hazijibiwi vyema kwa hoja na mawaziri wa serikali.

Hilo la kukerwa na majibu ya serikali yasiyokidhi hoja za wapinzani, Mama Samia akajiona ni kama Activist / Mwanaharakati ingawa ni CCM anayehusudu maswali magumu yajibiwe kwa hoja thabiti.

Mama Samia anaongeza kabla ya kuingia siasa alikuwa anaona nondo za wapinzani huku upande wa serikali ambayo ni ya CCM bara na Visiwani pia, mawaziri huja na majibu hafifu yasiyo ridhisha kwake na wanaofuatilia shughuli za Bunge.



Pamoja na kukunwa na hoja zilizoenda shule za wapinzani, Mama Samia aliwaeleza wasikilizaji ametokea ktk familia ya kawaida ambapo baba yake alikuwa mwalimu wa shule na mama yake mama wa nyumbani aliyetumia nafasi kuwafundisha na kuwasaidia kazi za masomo wakitoka shule.

Hiyo ilimsukuma kujiendeleza kimasomo kila wakati na kufanya kazi katika serikali ya SMZ na muda mrefu katika NGO's mbalimbali za kimataifa kabla ya kujiunga na siasa kupitia viti maalum CCM.

Mama Samia alipofanikiwa kuteuliwa Mwakilishi wa Viti Maalum alipata faraja kubwa akitegemea kutasaidia kukijenga chama cha CCM kuwa na watendaji wajibu-hoja-wazuri, kutokana na kuona mawaziri wa serikali na wabunge wa CCM kukosa hoja motomoto au majibu yakuridhisha kwa maswali na hoja nzuri za wapinzani na kuzidiwa wakiwa bungeni au baraza la wakilishi wakionekana / kusikika 'live' .

Ghafla bin vu, Mama Samia alipoingia Baraza la Wakilishi akateuliwa kuwa Waziri wa Sera Ajira Maendeleo ya akina Mama na Vijana ktk Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Na miaka 5 baadaye akawa waziri wa Biashara na Utalii katika SMZ. Baadaye akagombea kiti Makunduchi Zanzibar na kufanikiwa kuwa mbunge wa Zanzibar katika Bunge la Jamhuri ya Muungano na kuteuliwa kuwa Waziri wa Mazingira na hatimaye mgombea Mwenza wa Urais na kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania.

Hakutegemea kupewa nafasi hizo ghafla hivyo na pia akikumbuka nondo za wapinzani bungeni kupitia maswali, akaona amewekwa mstari wa mbele kukabiliana na hoja zinazowagusa wananchi ambazo hazipatiwi majibu ya kuwaridhisha wananchi.

Source: Millard Ayo

Toka katika maktaba :

Mwananchi
Advertisement

Karume, Maalim Seif wakutana faragha Z’bar
Saturday May 3 2014
Rais Mstaafu wa Zanzibar awamu ya sita, Dk Amani Abeid Karume amekutana na viongozi wa Kamati ya Maridhiano Zanzibar na kujadiliana hali ya kisiasa iliyojitokeza katika mjadala wa Katiba Mpya, pamoja na kujitoa kwa wabunge wa Ukawa kwenye vikao vya Bunge Maalumu la Katiba.

Rais Mstaafu wa Zanzibar Amani Abeid Karume na Makamu wa Kwanza wa Rais wa SMZ, Maalim Seif Sharif Hamad wakifurahia jambo wakati wa mazungumzo yao nyumbani kwa Karume, Mbweni mjini Zanzibar. Na Mpigapicha Wetu

Kumbe ndio maana...!, then 2025 tunakwenda kupata SUK ya JMT!.
P
 
Mama Samia yuko vizuri sana. Tafuta clip alipomtembelea Tundu Lissu pale Hospitalini Nairobi. Utamfaidi Samia orijino yaani bila zile mbwembwe za kisiasa. Mama mmoja mtamu saaana.
Duh...!, Mkuu Mindi hizi lugha hizi...!,
P
 
Kwa hali ya covid 19 ilivyo katika taifa letu ni vigumu kutabiri nani atakuwa rais wa nchi mwishoni mwa mwaka huu wakuu wanamchezea mgeni sebuleni na hajali idadi ya walinzi wanaomzunguka mzee you never know Pasco imagine wale wazee wa kucheza na kura wakati wako busy kuiba mara paap anaanguka mmojawapo kwa kushindwa kupumua
Mkuu Hassan J. Mosoka , leo ndio nakusoma hapa in between the lines!, umesema jambo fulani kubwa sana, ambapo zile Idara za wale 'jamaa' za wenzetu ndio huwa wanachukulia serious!. Kwa vile walifanya siri, usikute ni kweli hiki ndicho kilichotokea!.
You are very powerful fellow!, sharpen those powers!.
P
 
Uchaguzi Mkuu wa rais anafanyikia mioyoni mwa watu siku nyingi kabla, mfano sasa japo tuko 2023, lakini uchaguzi wa rais wa JMT wa 2025 ameisha chaguliwa mioyoni mwa watu, uchaguzi ni kukamilisha tuu taratibu!.
P
Ni kwa sababu unajua kuwa hapa huwa haufanyiki uchaguzi bali uchafuzi kama uliofanywa na yula juha wa kisukuma
 
Ni kwa sababu unajua kuwa hapa huwa haufanyiki uchaguzi bali uchafuzi kama uliofanywa na yula juha wa kisukuma
Kiafrika tuna mila na utamaduni wa kuwaheshimu marehemu wetu, mtu very bright upstairs with calculus photographic memory, huwezi kumuita juha!.
P
 
appreciate = thamini

Ila kwa vile umeijaza kimombo kuonesha msisitizo, acha ikae hivyo!
Nikiacha hivyo na kuonekekana kama mimi natamani... haitakuwa poa, japo mimi pia ni binadamu, na wanadamu wote ni viumbe dhaifu!.
P
 
Tuko sawa kabisa!.
p

Upotashaji wa nini huu Pascal Mayalla ?

Kulikoni kujaribu kumnukuu mtu out of context?

Mada yako na comment yangu za 28 Apr 2020 zilikuwa kwenye sekeseke haswa la ugonjwa wa corona. Kumbuka mgonjwa wa kwanza Tanzania ilikuwa 17 March 2020:

Dereva taxi aliyemchukua ambaye sasa ni mgonjwa wa Corona, hana corona

Screenshot_20230426-073914.jpg


Tafadhali zingatia nukuu nzima, vinginevyo upotoshaji huu wa nini ndugu?
 
Duhh, hizi kauli kweli huumba. Haikuchua muda.


“Kwa hoja kama hizi za huyu mama Samia, kama age sio issue sana, si huyu mama atatufaa sana 2025 au tuwashauri kwa vile Magufuli analamika sana kuhusu urais, mara ni mateso, mara ni kazi ngumu, mara ni mzigo mzito, tumshauri rais Magufuli, kwa vile Samia anatosha sana, hivyo tumpunguzie mateso, hana haja ya kuendelea na mateso, mzigo mzito na kazi ngumu ya urais, na hata kama ni wale tausi au wanyama wa Magogoni, au yale majabali ya Chamwino, tutamjengea Chato na kumuomba bora apumzike tuu mapema, na kumpisha Mama Samia ndio amalizie ngwe yake iliyobakia?. Hili mnalionaje?.”
 
Pascal Bango lako hili limekuwa kama Dua njema kwa Mama Samia
Leo ndie Mku wa Nchi
Sasa Ni wakat muafaka kuondoa Kero zote za Muungano
ikiwemo ya Mamlaka ya Zanzibar kurejeshwa.
 
Wanabodi,

Amesema Zanzibar ni visiwa hivyo viko wazi pande zote, hivyo faida kubwa kabisa ya muungano ni ulinzi usalamax amani na na utulivu wa Zanzibar, bila muungano, ilikuwa ni rahisi sana kuivamia Zanzibar na Zanzibar ikivamiwa ni rahisi sana kuivamia bara, hivyo muungano umeimarisha sana ulinzi na usalama, amani na utulivu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kuna kitu Mama Samia amekisema sikuwahi kukijua!. Kumbe Wizara ya Mambo ya Nje ilipokiwa ikiitwa Wizara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa ndio ilikuwa ya Muungano iki handle issues zote za Zanzibar kimataifa, lakini , ilipobadilishwa jina na kuitwa Wizara ya Mambo, ya Nje na Ushirikiano wa Africa Mashariki, sasa ina handle mambo ya Zanzibar ndani ya Africa Mashariki tuu, lakini kimataifa, kwa yale mambo ambayo sio ya muungano, SMZ ya Zanzibar imepewa uhuru wa kunegotiate ufadhili, misaada, na mikopo na mikataba ya kimataifa kwaniaba ya Zanzibar, ila kwenye kutiliana saini, anayetia saini ni serikali ya JMT, kwasababu Zanzibar haina sovereignty, sovereignty ni moja tuu ambayo iko kwenye JMT pekee!.

Hili sikuwahi kulijua, hivyo kumbe sasa Zanzibar inaweza kupata misaada na mikopo ya kimataifa, sasa kwavile uwiano wa kugawana misaada ya kutoka nchi wafadhili na wahisani, Zanzibar inastahili kupata asilimia 4.5% ya misaada yote kwa Tanzania, sasa kwa vile Zanzibar nayo inaweza kuomba ufadhili wa kimataifa, jee hii misaada ya kimataifa ya Zanzibar inayoomba, Tanzania bara pia tunapewa ule mgao wa asilimia 95.5% ya misaada ya Zanzibar, au misaada ya Tanzania tuu, ndio Zanzibar inapaswa kugaiwa asilimia 4.5%, lakini kwa misaada ya Zanzibar, then misaada hiyo ni ya Zanzibar pekee?.

Mama Samia amezungumzia kero za muungano na kusema kero nyingi zimeisha tatuliwa ila utekelezaji ndio unasua sua, na kutolea mfano deni lililokuwa la umeme la Tanesco, deni hilo lilisababishwa na double taxation, kwa Tanesco kuwachaji SMZ VAT huku shirika la umeme la Zanzibar, Zesco nalo likiwachaji kodi ya ongezeko la thamani Vat, wateja watumiaji wa umeme zao nao wakilipishwa Vat, kero hiyo imetatuliwa kwa Tenesco hawaichaji tena Vat kwa SMZ, hivyo Zanzibar haidaiwi tena deni lolote la umeme na Tanesco.

Ninachokumbuka kwenye deni la umeme la Zanzibar, lilitokana na Tenesco kuuza umeme kwa bei ya juu kwa Zesco, halafu Zesco wanauza umeme huo kwa bei ya chini Zanzibar, kumbe ilikuwa ni issue ya VAT!.

Pia amezungumzia kero za muungano kadri zinavyotatuliwa, kero nyingine zinaibuka, hivyo issue za kero za muungano ni issue endelevu.
Taja faida zake Ili uweze kutuambia utaulinda kwa Gharama zote!
Karibu hapa usome faida za muungano.
P
 
Back
Top Bottom