Nilicho-conclude ni kwamba wenye akili na big brains wako mtaani wanakufa kwa stress tu hasa anapoona mtu aliyesoma naye kilaza wa kutupwa ndio kashikilia kitengo kinachohitaji mtu mwenye akili kama yeye lakini yeye anakufa kwa kutopata connection tu
Kwa maelezo yako hata na wewe ukipata kazi serikalini utakuwa kilaza kama hao wengine.
Maelezo yako yana ukweli uliopinda kwa kiwango cha juu. Kuna kipindi nilikuwa nashiriki sana kuhoji watumishi watarajiwa (interviews) kwa sekta niliyokuwa nafanyia kazi na kwa kiwango kikubwa tulkuwa tunapata waajiriwa wenye uwezo mzuri kitaaluma.
Mimi nimefanya kazi serikalini kwa muda wa miaka zaidi ya 40 na kwa maoni yangu yanayotokea serikalini ni kama yafuatayo:
1. Zamani (enzi unaajiriwa bila ya degree) unakwenda kujiunga kazini unamkuta bosi wako anakufunza kazi kwa uhakika kabisa na wewe bila ya dharau unasota kujifunza. Na unajifunza kweli hatua kwa hatua bila ya short cut.
Leo hii kijana ameajiriwa ana degree inakuwa balaa akifika kazini yeye ndiye anajiona anajua vitu kumbe hajui na hana uzoefu wo wote. Dharau zinakuwa nyingi sana hata ukimuelekeza anakudharau eti 'mimi nina degree ya kitu fulani wewe utaniambia nini?'. Matokeo yake wanaachwa kama walivyo na wanaishia kuharibu kazi.
2. Kupewa cheo bila ya kuwa na uzoefu kunamfanya kijana kujiona kama yeye ndiyo kila kitu, communication skills hakuna kabisa. Anaandika barua ya kiswahili tu basi haieleweki kabisa, sisemi hiyo kiingereza tena. Zamani mtumishi wa serikali ulikuwa unafanya mtihani wa kiswahili na kiswahili kigumu (hii aliniambia mfanyakazi mwenzangu).
3. Nadhani ule mpangilio wa kwenda kujifunza a b c za utumishi serikalini pale Magogoni zingerudishwa kwa ajili ya kuweka nidhamu serikalini.
Mukubali kujifunza mukipata ajira musijione muna degree ndiyo munajua kila kitu.