Watu waliokataa Magufuli asiongezewe Miaka ndio haohao wanashadadia Mbowe aendelee kuongoza. Ndio haohao wanakapinga CCM isiendelee! Unafiki mtupu!

Watu waliokataa Magufuli asiongezewe Miaka ndio haohao wanashadadia Mbowe aendelee kuongoza. Ndio haohao wanakapinga CCM isiendelee! Unafiki mtupu!

Maoni yako ni yapi?
Kwamba nisijadili Jambo ambalo kila mwezi wanapewa ruzuku ambayo ni Kodi yangu?

Kwamba Kodi zinazochukuliwa na kutolewa kama ruzuku zinataka kwa wajumbe na wanachama tuu?
Hakuna utaratibu wa serikali kugawa kodi kwa SACCOS nchi hii, inakubidi uamue kwanza kama CHADEMA ni chama cha siasa au SACCOS ili ueleweke unapokijadili unataka nini.

Kama CHADEMA ni SACCOS ya Mbowe kama mnavyodai tatizo kubwa kwa kodi yenu haiwezi kuwa Mbowe, inabidi iwe ni serikali inayogawa kodi yenu kwa SACCOS ya mtu kwa hiyo inakuwa ujua kukata matawi badala ya kuchimbua mizizi kabisa kwa kuitaka serikali isitishe kodi yenu kwenda SACCOS binafsi.
Huelewi nini hapo??
 
Kwa hiyo Umekiri sio Saccos,
Mbona hutaki watu wajadili kisa wao sio wanachama au wajumbe?
 
😃😃

Kwamba mtu haruhusiwi kubadili nafasi ya uongozi anayotaka kugombea?
inaleta mashaka na wasiwasi mno, kwamba umeona au kusense nini hata ubadili nafasi ya kugombea?

unaelewa gentleman,
hata wagombea uongozi wa vyama vya upinzani kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa walikua na mawenge hivi hivi kama huyo muungwana wa mara autake umakamu baada ya muda anautaka uenyekiti.

wawo walikua wanaadika mathalani sehemu ya mwaka wa kuzaliwa, anaandika 1975, anafuta anaandika tena 1989, anafuta tena anaandika 19767 anafuta mpaka anakosa kabisaa sehemu ya kuandika tena 🤣

sasa akirejesha fomu kwa mkurugenzi wa uchaguzi inakutikana na makosa mengi sana , lakini pia baadhi ya taarifa hakuna au hazionekani vizuri kwasababu ya kufutafuta taarifa sehemu mbalimbali za fomu ya uongozi.

Naona yale mawenge ni kama yamehamia ngazi ya Taifa 🐒
 
Mtoa hoja huna akili hata kidogo ila usiseme nakutukana. Hujui kuwa kwa Magufuli Katiba ilikuwa haimruhusu kuongeza hata siku moja baada ya mihula yake miwili wakati Mbowe yeye katiba ya chama chake haina ukomo, inamruhusu kugombea hata milele akitaka. Suala ni KATIBA
 
inaleta mashaka na wasiwasi mno, kwamba umeona au kusense nini hata ubadili nafasi ya kugombea?

unaelewa gentleman,
hata wagombea uongozi wa vyama vya upinzani kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa walikua na mawenge hivi hivi kama huyo muungwana wa mara autake umakamu baada ya muda anautaka uenyekiti.

wawo walikua wanaadika mathalani sehemu ya mwaka wa kuzaliwa, anaandika 1975, anafuta anaandika tena 1989, anafuta tena anaandika 19767 anafuta mpaka anakosa kabisaa sehemu ya kuandika tena 🤣

sasa akirejesha fomu inakutikana na makosa mengi lakini pia baadhi ya taarifa hakuna au hazionekani vizuri kwasababu ya kufutafuta taarifa sehemu mbalimbali za fomu ya uongozi.

Naona yale mawenge ni kama yamehamia ngazi ya Taifa 🐒

Gentleman!
Unamatusi ya Rejereja kwa CHADEMA. Wewe ni mtani wao?

Unaelewa nini kuhusu kubadili gear angani?
Nani waasisi wa kubadili gear angani?

Kuwaita Wanachadema wanamawenge sio Sawa gentleman
 
Mtoa hoja huna akili hata kidogo ila usiseme nakutukana. Hujui kuwa kwa Magufuli Katiba ilikuwa haimruhusu kuongeza hata siku moja baada ya mihula yake miwili wakati Mbowe yeye katiba ya chama chake haina ukomo, inamruhusu kugombea hata milele akitaka. Suala ni KATIBA

Katiba inaweza kufanyiwa amendment ndani ya wiki na Rais akaongezewa Muda wake.

Katiba ni kitabu tuu ambacho kinaweza Leo kikawepo Kesho kisiwepo.
 
Mpo salama!

Watu wenye ndimi mbili. Watu wenye mawe mawili ya kupimia ni watu Hatari Sana popote walipo. Ni watu wanafiki na muda wowote wanaweza kukuuza.

Alipokuwepo Magufuli, Chawa wake walitoa maoni Yao kuwa Magufuli aongezewe Muda, Magufuli atawale milele, na kama Magufuli angekataa wapo walioapa wangemshikia kiboko kumlazimisha aendelee kutawala. Yalikuwa ni maoni Yao.

Sisi wengine maoni yetu tulikataa tukasema Hapana. Miaka yake ikiisha inatosha. Wengine tukasema Katiba hairuhusu lakini Katiba ni kitabu tuu tunaweza kukibadilisha sehemu ndogo (Constitution amendment) ili kuweka kipengele cha kuongeza Muda.

Haya walewale ambao waliwaka, walimkalia kooni JPM ambaye yeye mwenyewe hata hakuwahi kusema ataongeza Miaka zaidi ya yeye kutamka hataongeza Miaka. Leo hii kile walichokuwa hawakitaki kwa JPM wanakifanya kwenye chama Chao.

Mbowe hata angekuwa kiongozi mzuri kama Malaika, kumuongezea Miaka mingine juu ya ishirini sio Sawa.

Alafu Mbowe angetakiwa aonyeshe uzuri wake katika kuandaa viongozi wengine wazuri zaidi yake wa kumrithi.

Siongei kumtetea Lisu awe kiongozi nope! Anaweza kugombea mtu mwingine Nje ya Lisu na akawa kiongozi wa CHADEMA hii itaonyesha kuwa CHADEMA inaakiba ya kutosha ya viongozi.

Kama kuna watu wanaona Mbowe aendelee Basi wasishangae wale wanaoona CCM iendelee.

Wanasema Mbowe kaitoa CHADEMA Mbali.
Watu wanasema CCM imeitoa nchi Mbali.

Uongozi mzuri ni pamoja na kuweza kuachia nafasi wengine waongoze.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Mtaikon wa fasihi, huwezi tofautisha uongozi wa kiserikali na chama Cha siasa? Kama katiba ya chama Cha siasa haisemi ukomo wa madaraka Kwa nini unalazimisha? Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania imeweka ukomo wa rais, Hivyo tusubiri uchaguzi wa kidemokrasia wa Chadema siku ikifika.
 
Katiba inaweza kufanyiwa amendment ndani ya wiki na Rais akaongezewa Muda wake.

Katiba ni kitabu tuu ambacho kinaweza Leo kikawepo Kesho kisiwepo.
Huwezi kufanya mabadiliko makubwa ya katiba ya nchi bila kura ya wananchi, ili ubadili jambo kubwa kama ukomo wa Urais unahitaji kufanya referendum, huwezi kufanya hivyo kwa wiki moja tu.
 
Huwezi kufanya mabadiliko makubwa ya katiba ya nchi bila kura ya wananchi, ili ubadili jambo kubwa kama ukomo wa Urais unahitaji kufanya referendum, huwezi kufanya hivyo kwa wiki moja tu.

Amendment hahitaji wananchi .wananchi wapo bungeni pale
 
Mtaikon wa fasihi, huwezi tofautisha uongozi wa kiserikali na chama Cha siasa? Kama katiba ya chama Cha siasa haisemi ukomo wa madaraka Kwa nini unalazimisha? Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania imeweka ukomo wa rais, Hivyo tusubiri uchaguzi wa kidemokrasia wa Chadema siku ikifika.

Chama ndio serikali.
Kwa tawala za nchi Zetu. Ukikitaja chama unazungumzia serikali na ukitaja serikali unazungumzia chama.

Mpaka hapo utaona ugumu wa kukitoa chama kilichopo madarakani kwa sababu hapo unazungumzia kuitoa serikali madarakani.

Kwa upande wa chama, yaani level ya chama.
Hujawahi kujiuliza kwa nini mbunge wa chama Fulani yeye kila mwaka ndiye anagombea Jimbo Fulani kana kwamba hakuna watu wengine?

Au upande wa viti maalumu.
 
Magufuli alikuwa Rais wa nchi, Mbowe ni mwenyekiti wa CHADEMA.
Nchi ni ya watu wote, wenye vyama na wasio na vyama, wenye dini, wasio na dini wapagani n.k
CHADEMA ni ya wanachadema
Kwa mfano mbowe akachukua urais wa Tz, unafikiri ataishia miaka kumi? Lazima atabadilisha Katiba.
 
Binafsi namshukuru sana Lissu kutangaza nia ya kugombea uenyekiti wa CDM taifa, imenisaidia kuwafahamu baadhi ya viongozi waandamizi wa CDM kuwa wapo ki maslahi tu na ni wachumia tumbo tu na wajasilia siasa. Namkubali sana mwamba, lakini kama kweli atagombea tena nitamtoa maana kabisa na nitabadili mtazamo wangu juu ya CDM.
Who are you by the way
 
Chama sio mali ya umma, chama ni mali ya wanachama. CHADEMA hakiwajibiki kukidhi matamanio na haja zenu wanaCCM, ACT n.k Kwa mfano CCM wao huwa hawana utaratibu wa kushindanisha nafasi ya mwenyekiti taifa kupitia uchaguzi au kama ambavyo waliamua kutoa fomu moja mwaka 2020 na wameamua kufanya hivyo tena 2025, huo ni uamuzi wa wana CCM, itakuwa kituko CHADEMA kulalamikia huo utaratibu wa CCM au kulazimisha utaratibu wao wanaoona unafaa.
Chama ni Mali ya Umma na kikipata kura nyingi za Wananchi kinapata Ruzuku ambayo ni Kodi za Wananchi

Hapa unasemaje Chama sio Mali ya Umma?
 
Magufuli alikuwa Rais wa nchi, Mbowe ni mwenyekiti wa CHADEMA.
Nchi ni ya watu wote, wenye vyama na wasio na vyama, wenye dini, wasio na dini wapagani n.k
CHADEMA ni ya wanachadema
CHADEMA ni mali ya Mbowe na mkwewe Edwin Mtei
 
Magufuli alikuwa Rais wa nchi, Mbowe ni mwenyekiti wa CHADEMA.
Nchi ni ya watu wote, wenye vyama na wasio na vyama, wenye dini, wasio na dini wapagani n.k
CHADEMA ni ya wanachadema
Chadema haiwezi kuwa ya wanachedema huku wanaendesha chama kupitia ruzuku ambazo nipamoja na Kodi zetu sisi tusio na vyama.
 
Kwa mfano mbowe akachukua urais wa Tz, unafikiri ataishia miaka kumi? Lazima atabadilisha Katiba.
Amesema anagombea Urais wa Tanzania?
Aligombea huo urais 2015 au 2020?
 
Hata yanga ikicheza mechi inaangaliwa na watu wote ikiwemo wa Simba, Azam, Tabora n.k ila Yanga ni ya wanayanga.
Kama unafikiri CHADEMA ni mali ya umma nenda wewe mwanaCCM kapige kura za kumchagua mwenyekiti wa CHADEMA.
Yanga/Simba haiendeshwi kwa Kodi zetu, lkn CDM inaendeshwa kwa Kodi za wananchi ndio maana CAG anawakagua matumizi yao.
 
Chama ndio serikali.
Kwa tawala za nchi Zetu. Ukikitaja chama unazungumzia serikali na ukitaja serikali unazungumzia chama.

Mpaka hapo utaona ugumu wa kukitoa chama kilichopo madarakani kwa sababu hapo unazungumzia kuitoa serikali madarakani.

Kwa upande wa chama, yaani level ya chama.
Hujawahi kujiuliza kwa nini mbunge wa chama Fulani yeye kila mwaka ndiye anagombea Jimbo Fulani kana kwamba hakuna watu wengine?

Au upande wa viti maalumu.
Badala ya kupiga porojo zako ungepigania mambo ya serikali yatenganishwe na chama.
Na sio nchi zetu hizi, sema Tanzania. Kenya, Zambia, Malawi, Ghana, Senegal na nchi nyingine nying tu za Afrika wamefanikiwa kutenganisha chama na serikali.
 
Back
Top Bottom