Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hakuna utaratibu wa serikali kugawa kodi kwa SACCOS nchi hii, inakubidi uamue kwanza kama CHADEMA ni chama cha siasa au SACCOS ili ueleweke unapokijadili unataka nini.Maoni yako ni yapi?
Kwamba nisijadili Jambo ambalo kila mwezi wanapewa ruzuku ambayo ni Kodi yangu?
Kwamba Kodi zinazochukuliwa na kutolewa kama ruzuku zinataka kwa wajumbe na wanachama tuu?
Bila unafiki, maisha hayanogi, hata wewe mada yako imejaa unafiki mtupu
Hakuna utaratibu wa serikali kugawa kodi kwa SACCOS nchi hii, inakubidi uamue kwanza kama CHADEMA ni chama cha siasa au SACCOS ili ueleweke unapokijadili unataka nini.
Kama CHADEMA ni SACCOS ya Mbowe kama mnavyodai tatizo kubwa kwa kodi yenu haiwezi kuwa Mbowe, inabidi iwe ni serikali inayogawa kodi yenu kwa SACCOS ya mtu kwa hiyo inakuwa ujua kukata matawi badala ya kuchimbua mizizi kabisa kwa kuitaka serikali isitishe kodi yenu kwenda SACCOS binafsi.
Huelewi nini hapo??
inaleta mashaka na wasiwasi mno, kwamba umeona au kusense nini hata ubadili nafasi ya kugombea?😃😃
Kwamba mtu haruhusiwi kubadili nafasi ya uongozi anayotaka kugombea?
inaleta mashaka na wasiwasi mno, kwamba umeona au kusense nini hata ubadili nafasi ya kugombea?
unaelewa gentleman,
hata wagombea uongozi wa vyama vya upinzani kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa walikua na mawenge hivi hivi kama huyo muungwana wa mara autake umakamu baada ya muda anautaka uenyekiti.
wawo walikua wanaadika mathalani sehemu ya mwaka wa kuzaliwa, anaandika 1975, anafuta anaandika tena 1989, anafuta tena anaandika 19767 anafuta mpaka anakosa kabisaa sehemu ya kuandika tena 🤣
sasa akirejesha fomu inakutikana na makosa mengi lakini pia baadhi ya taarifa hakuna au hazionekani vizuri kwasababu ya kufutafuta taarifa sehemu mbalimbali za fomu ya uongozi.
Naona yale mawenge ni kama yamehamia ngazi ya Taifa 🐒
Mtoa hoja huna akili hata kidogo ila usiseme nakutukana. Hujui kuwa kwa Magufuli Katiba ilikuwa haimruhusu kuongeza hata siku moja baada ya mihula yake miwili wakati Mbowe yeye katiba ya chama chake haina ukomo, inamruhusu kugombea hata milele akitaka. Suala ni KATIBA
Mtaikon wa fasihi, huwezi tofautisha uongozi wa kiserikali na chama Cha siasa? Kama katiba ya chama Cha siasa haisemi ukomo wa madaraka Kwa nini unalazimisha? Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania imeweka ukomo wa rais, Hivyo tusubiri uchaguzi wa kidemokrasia wa Chadema siku ikifika.Mpo salama!
Watu wenye ndimi mbili. Watu wenye mawe mawili ya kupimia ni watu Hatari Sana popote walipo. Ni watu wanafiki na muda wowote wanaweza kukuuza.
Alipokuwepo Magufuli, Chawa wake walitoa maoni Yao kuwa Magufuli aongezewe Muda, Magufuli atawale milele, na kama Magufuli angekataa wapo walioapa wangemshikia kiboko kumlazimisha aendelee kutawala. Yalikuwa ni maoni Yao.
Sisi wengine maoni yetu tulikataa tukasema Hapana. Miaka yake ikiisha inatosha. Wengine tukasema Katiba hairuhusu lakini Katiba ni kitabu tuu tunaweza kukibadilisha sehemu ndogo (Constitution amendment) ili kuweka kipengele cha kuongeza Muda.
Haya walewale ambao waliwaka, walimkalia kooni JPM ambaye yeye mwenyewe hata hakuwahi kusema ataongeza Miaka zaidi ya yeye kutamka hataongeza Miaka. Leo hii kile walichokuwa hawakitaki kwa JPM wanakifanya kwenye chama Chao.
Mbowe hata angekuwa kiongozi mzuri kama Malaika, kumuongezea Miaka mingine juu ya ishirini sio Sawa.
Alafu Mbowe angetakiwa aonyeshe uzuri wake katika kuandaa viongozi wengine wazuri zaidi yake wa kumrithi.
Siongei kumtetea Lisu awe kiongozi nope! Anaweza kugombea mtu mwingine Nje ya Lisu na akawa kiongozi wa CHADEMA hii itaonyesha kuwa CHADEMA inaakiba ya kutosha ya viongozi.
Kama kuna watu wanaona Mbowe aendelee Basi wasishangae wale wanaoona CCM iendelee.
Wanasema Mbowe kaitoa CHADEMA Mbali.
Watu wanasema CCM imeitoa nchi Mbali.
Uongozi mzuri ni pamoja na kuweza kuachia nafasi wengine waongoze.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Huwezi kufanya mabadiliko makubwa ya katiba ya nchi bila kura ya wananchi, ili ubadili jambo kubwa kama ukomo wa Urais unahitaji kufanya referendum, huwezi kufanya hivyo kwa wiki moja tu.Katiba inaweza kufanyiwa amendment ndani ya wiki na Rais akaongezewa Muda wake.
Katiba ni kitabu tuu ambacho kinaweza Leo kikawepo Kesho kisiwepo.
Huwezi kufanya mabadiliko makubwa ya katiba ya nchi bila kura ya wananchi, ili ubadili jambo kubwa kama ukomo wa Urais unahitaji kufanya referendum, huwezi kufanya hivyo kwa wiki moja tu.
Mtaikon wa fasihi, huwezi tofautisha uongozi wa kiserikali na chama Cha siasa? Kama katiba ya chama Cha siasa haisemi ukomo wa madaraka Kwa nini unalazimisha? Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania imeweka ukomo wa rais, Hivyo tusubiri uchaguzi wa kidemokrasia wa Chadema siku ikifika.
Kwa mfano mbowe akachukua urais wa Tz, unafikiri ataishia miaka kumi? Lazima atabadilisha Katiba.Magufuli alikuwa Rais wa nchi, Mbowe ni mwenyekiti wa CHADEMA.
Nchi ni ya watu wote, wenye vyama na wasio na vyama, wenye dini, wasio na dini wapagani n.k
CHADEMA ni ya wanachadema
Who are you by the wayBinafsi namshukuru sana Lissu kutangaza nia ya kugombea uenyekiti wa CDM taifa, imenisaidia kuwafahamu baadhi ya viongozi waandamizi wa CDM kuwa wapo ki maslahi tu na ni wachumia tumbo tu na wajasilia siasa. Namkubali sana mwamba, lakini kama kweli atagombea tena nitamtoa maana kabisa na nitabadili mtazamo wangu juu ya CDM.
Chama ni Mali ya Umma na kikipata kura nyingi za Wananchi kinapata Ruzuku ambayo ni Kodi za WananchiChama sio mali ya umma, chama ni mali ya wanachama. CHADEMA hakiwajibiki kukidhi matamanio na haja zenu wanaCCM, ACT n.k Kwa mfano CCM wao huwa hawana utaratibu wa kushindanisha nafasi ya mwenyekiti taifa kupitia uchaguzi au kama ambavyo waliamua kutoa fomu moja mwaka 2020 na wameamua kufanya hivyo tena 2025, huo ni uamuzi wa wana CCM, itakuwa kituko CHADEMA kulalamikia huo utaratibu wa CCM au kulazimisha utaratibu wao wanaoona unafaa.
CHADEMA ni mali ya Mbowe na mkwewe Edwin MteiMagufuli alikuwa Rais wa nchi, Mbowe ni mwenyekiti wa CHADEMA.
Nchi ni ya watu wote, wenye vyama na wasio na vyama, wenye dini, wasio na dini wapagani n.k
CHADEMA ni ya wanachadema
Chadema haiwezi kuwa ya wanachedema huku wanaendesha chama kupitia ruzuku ambazo nipamoja na Kodi zetu sisi tusio na vyama.Magufuli alikuwa Rais wa nchi, Mbowe ni mwenyekiti wa CHADEMA.
Nchi ni ya watu wote, wenye vyama na wasio na vyama, wenye dini, wasio na dini wapagani n.k
CHADEMA ni ya wanachadema
Amesema anagombea Urais wa Tanzania?Kwa mfano mbowe akachukua urais wa Tz, unafikiri ataishia miaka kumi? Lazima atabadilisha Katiba.
Yanga/Simba haiendeshwi kwa Kodi zetu, lkn CDM inaendeshwa kwa Kodi za wananchi ndio maana CAG anawakagua matumizi yao.Hata yanga ikicheza mechi inaangaliwa na watu wote ikiwemo wa Simba, Azam, Tabora n.k ila Yanga ni ya wanayanga.
Kama unafikiri CHADEMA ni mali ya umma nenda wewe mwanaCCM kapige kura za kumchagua mwenyekiti wa CHADEMA.
Badala ya kupiga porojo zako ungepigania mambo ya serikali yatenganishwe na chama.Chama ndio serikali.
Kwa tawala za nchi Zetu. Ukikitaja chama unazungumzia serikali na ukitaja serikali unazungumzia chama.
Mpaka hapo utaona ugumu wa kukitoa chama kilichopo madarakani kwa sababu hapo unazungumzia kuitoa serikali madarakani.
Kwa upande wa chama, yaani level ya chama.
Hujawahi kujiuliza kwa nini mbunge wa chama Fulani yeye kila mwaka ndiye anagombea Jimbo Fulani kana kwamba hakuna watu wengine?
Au upande wa viti maalumu.