Watu waliomkufuru Mungu wakafariki dunia

Watu wanasema Shetani ni Adui yetu na kumchukia kwelikweli lakini mbona Mungu ktk kitabu chake anaonekana akiongea na shetani Freandly kabisa? ss inakua vp tumchukie ? I think tumfanye rafiki na nadhani hata2dhuru
 
Mungu ni Yeye yule aliyekuwepo , aliyepo na atakayekuwepo.
Mungu ni Mwanzo na Mwisho, ni Alpha na Omega.
Yeye vile vile ni Neno linaloumba.

Mungu hataniwi, hadhihakiwi, aona na asikia yote.

Hivyo basi wanaomdhihaki na kumtukana Mungu, wanajiondolea pumzi ya bure waliyowekewa , tena pumzi waliyowekewa hata bila ridhaa yao wenyewe.
 
hakuna mungu wa isaka wala yakobo,kuna mungu wa wanadamu wote.
 


Kabisa mkuu!!
 
kuna watu wanataka tuamini kuwa mungu alianza kuwepo wakati wa yakobo na isaka,eti wanajibinafishia hadi mungu anakua wa fulani kama kwamba isaka na yakobo ndo walimuumba huyo mungu.
 
Mungu hadhihakiwi!
Hata hivyo,post hii ni uzushi,na imethibitika wote hapo juu walikufa vifo vya kawaida!
Baadhi walikuwa na HIV,wengine[kwa mfano huyo binti wa Brazil] hakuna ushahidi popote kuwa kumewahi tokea ajali ya aina hiyo.

CLICK LINK hii:

Beware: Men Who Mocked God - Religion - Nairaland

Halafu msome Lagerwhenindoubt,
kaweka links za sababu za kifo cha kila mmoja hapo.
 
kuna watu wanataka tuamini kuwa mungu alianza kuwepo wakati wa yakobo na isaka,eti wanajibinafishia hadi mungu anakua wa fulani kama kwamba isaka na yakobo ndo walimuumba huyo mungu.

Kweli nakubali Mungu Ni Wa wanadamu wote!

Mkuu kwa mfano mtu akisema Mungu Wa Eliya na mungu baali anamaanisha nini?
 
kwani huwajui hawa jamaa wanavyopenda kumtangaza mungu wao kwa vitisho ili tu ukubali sera zao.kama ni kufa kila mtu atakufa it is just a matter of time,kila mtu atakufa kwa wakati wake,hamna haja ya kutishana.
 
Kweli nakubali Mungu Ni Wa wanadamu wote!

Mkuu kwa mfano mtu akisema Mungu Wa Eliya na mungu baali anamaanisha nini?
mkuu katika bibilia kuna miungu wa kila dizaini.
 
???????????????????????????
 
Zaburi 82:1-2.
MUNGU akasimama katika kusanyiko la Mungu.
KATIKATI YA MIUNGU ANAHUKUMU.
Hata lini mtahukumu kwa dhuluma.
6-mimi nimesema,NDINYI MIUNGU ,na wana wa aliye juu,mtakufa kama wanadamu.

Ndo kusema katika biblia walikuwepo miungu kibao akiwemo wa isaka,yakobo,eliya,daudi etc.
 
Mleta mada na wanaokuunga mkono mnachofanya ni kutaka kumrahisisha Mwenyenzi Mungu kwa mitizamo ya kibinadamu; kama vile Mungu anaendesha mambo yake kishabiki kama timu za mpira. Waliosema "Mungu si Athumani" walikuwa na hekima ya kipekee. Mwenyenzi Mungu hampimi binadamu kirahisirahisi hivyo wala haendeshi mambo yake kwa jazba za kibinadamu. Wako waliomtukana na wakaishi hadi umri mkubwa sana. Kwa hiyo mifano uliyotoa, wako watakaokupa mingine hai ya wanaomkana na kumkashifu kila siku lakini wanaendelea kula nchi na "kufanikiwa" kila siku. Halafu utakosa hoja ya kuonyesha UKUU wa kweli wa Mwenyenzi Mungu ambao haupimiki kirahisi hivyo. Ukumbuke kuna waliomkashifu lakini akaamua kuwabadili kama akina Paulo/Sauli.
 
mkuu katika bibilia kuna miungu wa kila dizaini.


Bado hujanijibu ndugu yng! Kwa mfano ukisema atukuzwe Mungu Wa Eliya! Au atukuzwe Mungu Wa Shadrack, Meshack na Abednego! Hapo kuna Maana gani?
 

Ndugu yangu..tatizo la dunia kua flat liko wazi..pata ufafanuzi wa aya zifuatazo utaelewa..
Quran 20;53.. since he is the one who has laid out the earth as a carpet for you...
Ouran pia inasema..is not he (better than your gods) who has made the earth as a fixed abode.. mistari hii inakinzani na sayansi..

swali kwako mwenye kitabu.. kwanini mitume wanajichanganya kuhusu mavazi yesu..wakati wa mwisho wa uhai wake pili kwanini waandishi wanatofautiana kuhusu muda wa mateso ya yesu? mungu anasaau?
 

Mkuu ktk Biblia kuna Mungu mmoja tu! Mungu aliumba kila kitu na vyote vilivyomo! Na ndio Mungu Wa Isaka, Yakobo, Eliya, Daudi etc!

Labda ukiulizwa mtu akisema atukuzwe Mungu Wa Eliya anakua na Maana gani hapo, kwamba Eliya alikua na Mungu wake au?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…