Watu waliomkufuru Mungu wakafariki dunia

Watu waliomkufuru Mungu wakafariki dunia

Kighoma Ally Malima alimkufuru Alah hata Mungu abishe atakuwa rais wa Tz kwa kupitia NRA,Mungu alimpiga bao la kisigino kwa dharau zake,RIP Malima.
Ebanaee, hiyo sikupata kuisikia. Nilichosikia kisababishi cha umauti wake ni tahayari ya muflisi aliyoibaini kwenye akaunti yake.
 
Kighoma Ally Malima alimkufuru Alah hata Mungu abishe atakuwa rais wa Tz kwa kupitia NRA,Mungu alimpiga bao la kisigino kwa dharau zake,RIP Malima.
Nonsense!! waliokufa wote wamemdhihaki mungu? Na wasiomdhihaki hawatakufa kabisa kwani kifo ni adhadu?
 
Nonsense!! waliokufa wote wamemdhihaki mungu? Na wasiomdhihaki hawatakufa kabisa kwani kifo ni adhadu?
VERY TRUE..KUNA WATU WENGI TU WANATAMKA MANENO MACHAFU NA WANAPETA TU. MUNGU SIO BINADAMU..ANGEKUWA ANAADHIBU KWA STYLE HIYO HAKUNA AMBAYE ANGEKUWA HAI
 
Hapo kwa John Lennon umechemka. Yesu si Mungu ndugu yangu bali ni mtume wa Mungu.
 
HAWA NI WATU WALIOMDHIHAKI MUNGU NA KUPATWA NA MAJANGA.

1. JOHN LENNON (MUIMBAJI)

Wakati alipokuwa akihojiwa na Mwandishi wa habari wa gazeti la [HASHTAG]#American[/HASHTAG] alinukuliwa akisema hivi "Ukristo utakufa na kutoweka duniani, siwezi kuwa na wasiwasi na hilo kwa kuwa nina uhakika nalo. Mafundisho ya [HASHTAG]#Yesu[/HASHTAG] yalikuwa sahihi na wala sipingi hilo ila mafundisho yale yalikuwa mepesi sana ambayo mtu yeyote anaweza kuyafundisha. Hebu angalia leo, tumekuwa maarufu hata zaidi yake (Hapo alilitaja kundi lake la The Bettle). Ilikuwa mwaka 1966.
Wiki moja baada ya kutamba kwamba yeye na kundi lake lilikuwa maarufu hata zaidi ya Yesu, akapigwa risasi sita na kufariki.

2. TANCREDO NEVES (RAIS WA BRAZIL)

Alisema kwamba endapo angepata kura laki tano kutoka katika uchaguzi mkuu wa Brazil na kuwa rais, hata [HASHTAG]#MUNGU[/HASHTAG] asingeweza kumtoa katika urais huo. Akafanikiwa, akapata kura zaidi ya hizo, akashinda uchaguzi, siku moja kabla ya kuapishwa, akafariki dunia.

3. CAZUZA (MWANAMUZIKI WA BRAZIL)

Alipokuwa katika shoo yake ndani ya jiji la [HASHTAG]#Rio[/HASHTAG] #De [HASHTAG]#Janeiro[/HASHTAG], alichukua sigara, akaanza kuivuta, akachukua nyingine na kisha kuirusha juu na kusema [HASHTAG]#Mungu[/HASHTAG], hiyo yako, chukua nawe uvute"
Alifariki akiwa na miaka 32 kwa ugonjwa wa kansa ya mapafu ambayo iliyaharibu sana mapafu yake kuliko mgonjwa yeyote yule.

4. MTENGENEZAJI WA MELI YA TITANIC.

Baada ya kutengeneza meli ya Titanic, Mwanahabari akamuuliza ni kwa kiasi gani ilikuwa salama nae akajibu "Ni salama sana, haiwezi kuzama na hata [HASHTAG]#Mungu[/HASHTAG] hawezi kuizamisha"
Nafikiri unajua kilichotokea kuhusu Titanic.

5. BON SCOTT (MUIMBAJI)

Mwimbaji huyu ambaye alitamba miaka ya 70 alitoa wimbo wake mmoja mwaka 1979 wenye maneno haya
"Don't stop me; I'm going down all the way, down the highway to hell'.
Tarehe 19 February mwaka 1980, alikutwa amekufa baada ya kupaliwa na matapishi yake.

6. Mwanamke mmoja alikuwa akihofia sana kuhusu ulevi wa marafiki wa Mtoto wake. Wakati wanataka kuondoka na gari, akamshika mtoto wake mkono garini na kumwambia "Binti yangu, Mungu awatangulie katika safari yenu" Yule binti akajibu "Gari imejaa Mama, huyo [HASHTAG]#Mungu[/HASHTAG] labda akae kwenye boneti la gari".
Baada ya masafa fulani ya safari yao, gari lile lilipata ajali kiasi ambacho hata polisi hawakujua ni aina gani ya gari lilikuwa. Lilikuwa limebondeka sana na watu wote walikutwa wamekufa. Kilichowashangaza polisi, trey la mayai wala halikuonekana kuguswa na hakuna hata yai moja lililokuwa limevunjika na wakati gari lilibondeka mpaka kutokutambulika.

7. CHRISTINA HEWITT (MWANDISHI WA HABARI)

Huyu alikaririwa akisema hivi "Nimesoma vitabu vyote duniani, ila hakuna kitabu kibaya...kibaya na kibaya kama [HASHTAG]#Biblia[/HASHTAG]"
Siku chache baada ya kusema maneno hayo, mwili wake ulikutwa umeunguzwa na moto ambao haikujulikana mpaka leo ule moto ulisababishwa na nini.

8. MARILYN MONROE (MUIGIZAJI)

Huyu alifuatwa na [HASHTAG]#Bill[/HASHTAG] [HASHTAG]#Graham[/HASHTAG] na kumwambia kwamba alitumwa na Roho wa Mungu kwa ajili ya kumhubiria. Alimkaribisha ndani, akamsikiliza kwa makini, alipomaliza akasema "Simhitaji [HASHTAG]#Yesu[/HASHTAG] wako, unaweza kuondoka nae". Wiki moja baadae, alikutwa amekufa katika makazi yake. Polisi walijaribu kuchunguza kipi kilimuua, mpaka leo hawajapata jibu.

[HASHTAG]#share[/HASHTAG] Ujumbe huu Kwa Ndugu na jamaa,ujumbe huu utawasidia kumuheshimu Mungu na kumtii.


Mungu ni pendo
 
Mmeanza vitisho vyenu kama wakati wa kuzika.. logic hamna kabisa.. mmeulizwa kila siku..kama huyu Mungu yupo..na ana akili sana..mbona hakutengeneza dunia nzuri sana isiyo na dhambi..wala makosa..nini kusudi lake..je alituumba akitegemea tutatenda dhambi ili atucheke na kutuchoma kama mnavyo dai.. hamuoni kwamba ni maigizo alifanya..yaani anatengeneza dhambi alafu anatukataza kufanya dhambi.. mtu/kiumbe yule yule mmoja..

pili mbona vitabu vyake vitakatifu..vina makosa sana tena primitive/vya kikale..na mambo yasiyo ya kibinadamu kama utumwa vimetamalaki.. tena mbaya zaidi vitabu havijui hata mambo ya wazi kabisa kama umbo la dunia..na kusema eti dunia ni ya flat.. huu ni ukale..
muandishi wake si mtu makini kama inavyo semwa bali ni mtu primitive..asiyekua na maarifa yakutosha
Duh
 
Back
Top Bottom