Watu waliomkufuru Mungu wakafariki dunia

Watu waliomkufuru Mungu wakafariki dunia

Mungu hadhihakiwi
Kama Mkuu Jose, umekomenti hivi basi ni kweli.
Mungu hadhihakiwi,

Kuna watu wanasema Mungu hayupo kwa sababu hawamjui na wala hawajawahi kupata taarifa zake.
Kuna wengine ambao ni wengi wanasumbuliwa tu na Kibri,
Kiburi cha Uzima, wakisha shiba Pilau na kulinywea maji baridi basi mabega juu, hata hawaulizi nani alitengeneza huo mpunga wa Pilau na Maji wanayo kula na kufulahi, na wala hawana wa kumshukuru kwa kuleta Pilau zaidi ya kumsifia aliye pika.
Wanaamini wao wapo duniani kwa miujiza tu, hakuna aliyewaumba.
Na mazingira yanayowalea kama, chakula, maji, Jua, hewa, nk, vipo kimiujizaijiza tu, hakuna aliyeviandaa kwa ajiri yao.
Pia wapo ambao wanapinga uwepo wa Mungu, lakini wanaujua ukweli kuwa Mungu yupo.

Usisumbuke mkuu dunia ina watu wa kila aina.

Wengine sifa yao ni Upinzani, yaani Wanapinga kila kitu, kiwe cha Ukweli au Uongo.

Ndivyo Walivyo.
 
1. JOHN LENNON (MUIMBAJI)

Wakati alipokuwa akihojiwa na Mwandishi wa habari wa gazeti la [HASHTAG]#American[/HASHTAG] alinukuliwa akisema hivi "Ukristo utakufa na kutoweka duniani, siwezi kuwa na wasiwasi na hilo kwa kuwa nina uhakika nalo. Mafundisho ya [HASHTAG]#Yesu[/HASHTAG] yalikuwa sahihi na wala sipingi hilo ila mafundisho yale yalikuwa mepesi sana ambayo mtu yeyote anaweza kuyafundisha. Hebu angalia leo, tumekuwa maarufu hata zaidi yake (Hapo alilitaja kundi lake la The Bettle). Ilikuwa mwaka 1966.
Wiki moja baada ya kutamba kwamba yeye na kundi lake lilikuwa maarufu hata zaidi ya Yesu, akapigwa risasi sita na kufariki.

2. TANCREDO NEVES (RAIS WA BRAZIL)

Alisema kwamba endapo angepata kura laki tano kutoka katika uchaguzi mkuu wa Brazil na kuwa rais, hata [HASHTAG]#MUNGU[/HASHTAG] asingeweza kumtoa katika urais huo. Akafanikiwa, akapata kura zaidi ya hizo, akashinda uchaguzi, siku moja kabla ya kuapishwa, akafariki dunia.

3. CAZUZA (MWANAMUZIKI WA BRAZIL)

Alipokuwa katika shoo yake ndani ya jiji la [HASHTAG]#Rio[/HASHTAG] #De [HASHTAG]#Janeiro[/HASHTAG], alichukua sigara, akaanza kuivuta, akachukua nyingine na kisha kuirusha juu na kusema [HASHTAG]#Mungu[/HASHTAG], hiyo yako, chukua nawe uvute"
Alifariki akiwa na miaka 32 kwa ugonjwa wa kansa ya mapafu ambayo iliyaharibu sana mapafu yake kuliko mgonjwa yeyote yule.

4. MTENGENEZAJI WA MELI YA TITANIC.

Baada ya kutengeneza meli ya Titanic, Mwanahabari akamuuliza ni kwa kiasi gani ilikuwa salama nae akajibu "Ni salama sana, haiwezi kuzama na hata [HASHTAG]#Mungu[/HASHTAG] hawezi kuizamisha"
Nafikiri unajua kilichotokea kuhusu Titanic.

5. BON SCOTT (MUIMBAJI)

Mwimbaji huyu ambaye alitamba miaka ya 70 alitoa wimbo wake mmoja mwaka 1979 wenye maneno haya
"Don't stop me; I'm going down all the way, down the highway to hell'.
Tarehe 19 February mwaka 1980, alikutwa amekufa baada ya kupaliwa na matapishi yake.

6. Mwanamke mmoja alikuwa akihofia sana kuhusu ulevi wa marafiki wa Mtoto wake. Wakati wanataka kuondoka na gari, akamshika mtoto wake mkono garini na kumwambia "Binti yangu, Mungu awatangulie katika safari yenu" Yule binti akajibu "Gari imejaa Mama, huyo [HASHTAG]#Mungu[/HASHTAG] labda akae kwenye boneti la gari".
Baada ya masafa fulani ya safari yao, gari lile lilipata ajali kiasi ambacho hata polisi hawakujua ni aina gani ya gari lilikuwa. Lilikuwa limebondeka sana na watu wote walikutwa wamekufa. Kilichowashangaza polisi, trey la mayai wala halikuonekana kuguswa na hakuna hata yai moja lililokuwa limevunjika na wakati gari lilibondeka mpaka kutokutambulika.

7. CHRISTINA HEWITT (MWANDISHI WA HABARI)

Huyu alikaririwa akisema hivi "Nimesoma vitabu vyote duniani, ila hakuna kitabu kibaya...kibaya na kibaya kama [HASHTAG]#Biblia[/HASHTAG]"
Siku chache baada ya kusema maneno hayo, mwili wake ulikutwa umeunguzwa na moto ambao haikujulikana mpaka leo ule moto ulisababishwa na nini.

8. MARILYN MONROE (MUIGIZAJI)

Huyu alifuatwa na [HASHTAG]#Bill[/HASHTAG] [HASHTAG]#Graham[/HASHTAG] na kumwambia kwamba alitumwa na Roho wa Mungu kwa ajili ya kumhubiria. Alimkaribisha ndani, akamsikiliza kwa makini, alipomaliza akasema "Simhitaji [HASHTAG]#Yesu[/HASHTAG] wako, unaweza kuondoka nae". Wiki moja baadae, alikutwa amekufa katika makazi yake. Polisi walijaribu kuchunguza kipi kilimuua, mpaka leo hawajapata jibu.
Mkuu hii kitu ilishaletwa humu jf 2014 ikajadiliwa sana

Watu waliomkufuru Mungu wakafariki dunia
 
Kama Mkuu Jose, umekomenti hivi basi ni kweli.
Mungu hadhihakiwi,

Kuna watu wanasema Mungu hayupo kwa sababu hawamjui na wala hawajawahi kupata taarifa zake.
Kuna wengine ambao ni wengi wanasumbuliwa tu na Kibri,
Kiburi cha Uzima, wakisha shiba Pilau na kulinywea maji baridi basi mabega juu, hata hawaulizi nani alitengeneza huo mpunga wa Pilau na Maji wanayo kula na kufulahi, na wala hawana wa kumshukuru kwa kuleta Pilau zaidi ya kumsifia aliye pika.
Wanaamini wao wapo duniani kwa miujiza tu, hakuna aliyewaumba.
Na mazingira yanayowalea kama, chakula, maji, Jua, hewa, nk, vipo kimiujizaijiza tu, hakuna aliyeviandaa kwa ajiri yao.
Pia wapo ambao wanapinga uwepo wa Mungu, lakini wanaujua ukweli kuwa Mungu yupo.

Usisumbuke mkuu dunia ina watu wa kila aina.

Wengine sifa yao ni Upinzani, yaani Wanapinga kila kitu, kiwe cha Ukweli au Uongo.

Ndivyo Walivyo.
kweli kabisa mkuu aisee
 
Dini si Mungu, wala Mungu si dini

Msahafu si Mungu, wala Mungu hajawahi kuwa Misahafu na haitatokea
 
Kama Mkuu Jose, umekomenti hivi basi ni kweli.
Mungu hadhihakiwi,

Kuna watu wanasema Mungu hayupo kwa sababu hawamjui na wala hawajawahi kupata taarifa zake.
Kuna wengine ambao ni wengi wanasumbuliwa tu na Kibri,
Kiburi cha Uzima, wakisha shiba Pilau na kulinywea maji baridi basi mabega juu, hata hawaulizi nani alitengeneza huo mpunga wa Pilau na Maji wanayo kula na kufulahi, na wala hawana wa kumshukuru kwa kuleta Pilau zaidi ya kumsifia aliye pika.
Wanaamini wao wapo duniani kwa miujiza tu, hakuna aliyewaumba.
Na mazingira yanayowalea kama, chakula, maji, Jua, hewa, nk, vipo kimiujizaijiza tu, hakuna aliyeviandaa kwa ajiri yao.
Pia wapo ambao wanapinga uwepo wa Mungu, lakini wanaujua ukweli kuwa Mungu yupo.

Usisumbuke mkuu dunia ina watu wa kila aina.

Wengine sifa yao ni Upinzani, yaani Wanapinga kila kitu, kiwe cha Ukweli au Uongo.

Ndivyo Walivyo.
Kumjua Mungu kuko katika kiini cha mtu -Kinachotokea ni kujitoa ufahamu pale mtu anapokua na kujitambua lakini Kumjua Mungu kuko pale pale ndio maana hata wasiomuamini humtaja kwa njia moja au nyingine iwe kwa kupinga au kwa ubaya kwa sababu Mungu yupo. Hata wanasayansi wameanza kukiri kuwa kuna wenyewe wanaita "inteligent Design" katika kila kilichotengenezwa duniani
 
Ni kweli mkuu.
Hao Wanasayansi hadi hii leo wameshindwa kutengeneza kitu chenye ubora wa Uumbaji wa Mungu.
Hawajawahi kutengeneza kitu chochote chenye uhai wala kukifufua, kama hicho chenye Uhai kikifa.
Pamoja na Sayansi yao hadi hii leo wameshindwa kulikaribia Jua, na hata leo Jua likifa au kuharibika hawajui watalitengenezaje ili liwe zima tena.
Pamoja na Sayansi yao hadi leo wameshindwa kuthibitisha ile nguvu inayoshikilia Sayari zisianguke, au kupoteza mzunguko wake yaani nguvu ya Gravity yenyewe inashikiliwa na nini hadi iwe imara.
Pamoja na sayansi yao wameshindwa kuelezea asili ya Binadamu, yaani chanzo cha chanzo cha binadamu.
Ajabu kubwa zaidi wameshindwa kutengeneza japo Spea ya viungo vyao vya mwili yaani, mkono ukikatika hawawezi kutengeneza mkono mwingine na kuurudishia mwilini.
Ajabu kubwa tena hao Wanasayansi wameshindwa kuzuia kifo hata kifo chao wenyewe.
Hawajui nani aliwaleta duniani, tena bila makubaliano yoyote na mtu yoyote, wamejistukia tu wapo.
Hawajui hatima yao na yetu baada ya kifo.
Cha ajabu wameshangaa sana kwa kuyakuta mazingira mazuri ya kuwalea, yaani Chakula, Maji, Hewa, Ardhi, Mafuta nk.
Kweli Wanasayansi hawana chochote cha kuwasifia katika dhana nzima ya uumbaji, na hawawezi chochote, hiyo dawa tu ya kutibu Ukimwi na Kansa wameshindwa kuigundua.

Watu walikuwepo duniani na maisha yalikuwepo kabla ya hao wanaojiita Wanasayansi.

Hata kama hakuna Wanasayansi maisha yapo.

Tumshukuru sana Mwenyezi Mungu Muumba Mbingu na Nchi kwa.
Kutuchagua sisi (baadhi yetu) ili tuishi duniani.
Kutuumba tukiwa na afya mjema.
Kutupa mahitaji yote muhimu kama chakula, maji nk.
Kutupa miongozo bora ya kuishi duniani.
Kutupa Neno lake.
Zaidi kutuahidi maisha mapya baada ya kifo ya milele ktk ufalme wake.

Amina.
 
Mmeanza vitisho vyenu kama wakati wa kuzika.. logic hamna kabisa.. mmeulizwa kila siku..kama huyu Mungu yupo..na ana akili sana..mbona hakutengeneza dunia nzuri sana isiyo na dhambi..wala makosa..nini kusudi lake..je alituumba akitegemea tutatenda dhambi ili atucheke na kutuchoma kama mnavyo dai.. hamuoni kwamba ni maigizo alifanya..yaani anatengeneza dhambi alafu anatukataza kufanya dhambi.. mtu/kiumbe yule yule mmoja..

pili mbona vitabu vyake vitakatifu..vina makosa sana tena primitive/vya kikale..na mambo yasiyo ya kibinadamu kama utumwa vimetamalaki.. tena mbaya zaidi vitabu havijui hata mambo ya wazi kabisa kama umbo la dunia..na kusema eti dunia ni ya flat.. huu ni ukale..
muandishi wake si mtu makini kama inavyo semwa bali ni mtu primitive..asiyekua na maarifa yakutosha
Duu your days are numbered. Labda utafuatia wewe. Kama siyp kufa basi jiandae na majanga mazito. Mungu hadhihakiwi na mtu akabaki salama. Bora ungekaa kimya. Pia kumbuka dhambi ya kumuudhi roho mtakatifu haisamehewi.
 
Mmeanza vitisho vyenu kama wakati wa kuzika.. logic hamna kabisa.. mmeulizwa kila siku..kama huyu Mungu yupo..na ana akili sana..mbona hakutengeneza dunia nzuri sana isiyo na dhambi..wala makosa..nini kusudi lake..je alituumba akitegemea tutatenda dhambi ili atucheke na kutuchoma kama mnavyo dai.. hamuoni kwamba ni maigizo alifanya..yaani anatengeneza dhambi alafu anatukataza kufanya dhambi.. mtu/kiumbe yule yule mmoja..

pili mbona vitabu vyake vitakatifu..vina makosa sana tena primitive/vya kikale..na mambo yasiyo ya kibinadamu kama utumwa vimetamalaki.. tena mbaya zaidi vitabu havijui hata mambo ya wazi kabisa kama umbo la dunia..na kusema eti dunia ni ya flat.. huu ni ukale..
muandishi wake si mtu makini kama inavyo semwa bali ni mtu primitive..asiyekua na maarifa yakutosha
Nina testimony ya watu kibao waliomkufuru Mungu na wakapata madhara moja kwa moja tens hayachelewi. Tubu dhambi zako.
 
Kama kweli hayupo nakuomba Leonard Robert baada ya wiki moja njoo hapa JF uje utoe ushuhuda kuwa hayupo. Pse ukitoa ushuhuda wako kuwa kweli hayupo ni mention ili nisiukose. Hebu tuanzie hapo naye MUNGU aliye mkuu ajidhihirishe kwako katika kipindi hicho.

Sent from my iPad using JamiiForums
ni zaidi ya miaka sasa
 
Back
Top Bottom